10/09/2026
FINALLY! VIDEO YA “MURIHE” YA MONIA FLEUR YATOKA RASMI
Hatimaye Video mpya ya “MURIHE” ya Monia Fleur imetoka rasmi, na ni miongoni mwa kazi zilizokuwa zikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa muziki wa Burundi.
Kutoka kwa jina la wimbo hadi kwenye video yenyewe, Monia Fleur ameendelea kuwapa mashabiki wake sababu nyingine ya kuendelea kumfuatilia. Kutolewa kwa video hii kunakuja wakati ambapo jina la msanii huyo limekuwa likizungumziwa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Katika siku za hivi karibuni, kulikuwa na tetesi zilizozagaa kuhusu Monia Fleur kuwa mjamzito, jambo lililozua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wafuasi wake.
Sasa macho na masikio yote yako kwa video ya “MURIHE” je, Monia Fleur amewapa mashabiki kile walichokuwa wakikisubiri? 👀🔥
Video imetoka rasmi. MURIHE ipo hewani!
Gusa Link kwa comment