RCFI. FM La radio communautaire Fizi FM,

DRCONGO: Kivu - Kaskazini/ Maandamano dhidi ya Monusco.RAÏA WAANDAMANA DHIDI YA UMOJA WA MATAÏFA( UN ) NA JESHI LA MONUS...
26/07/2022

DRCONGO: Kivu - Kaskazini/ Maandamano dhidi ya Monusco.

RAÏA WAANDAMANA DHIDI YA UMOJA WA MATAÏFA( UN ) NA JESHI LA MONUSCO/ by Madiba Mahoye.
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Watu watano wameuawa baada ya kupigwa risasi wakati wengine wapatao 50 wamejeruhiwa wakati wa maandamano ya kupinga uwepo wa vikosi vya walinda usalama wa umoja wa mataïfa katika eneo la Goma, mashariki mwa Jamuhuri ya Kifemokrasia ya Kongo, imethibitisha taarifa yake msemaji wa serikali ya Patrick Muyaya.

Jumatatu ya wiki hii, mamia ya waandamanaji wamefunga baadhi ya barabara mjini Goma kabla kuvamia makao makuu ya walinda amani wa umoja wa mataïfa.

Inasadikiwa kuwa watu hao wenye hasira walivunja vio na kuiba vitu vya thamani kutoka ufisi hizo.

Wafanya kazi wa umoja wa mataïfa wameondolewa katika majengo hayo kwa kutumia ndege za helikopta wakati polisi wakitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji.

Machafuko hayo yameendelea kushuhudiwa mapema asubuhi jumanne hii tariki 26 Jully 2022 nje ya makao ya UN.

Ujumbe wa umoja wa mataïfa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, unao tambuliwa k**a MONUSCO , ni moja wapo ya vikosi vikubwa vya walinda amani duniani .

Kwa muda sasa raïa wa DRC wamekuwa wakiwatuhumu walinda amani hao MONUSCO wamekua wakizembea kazini wakati wamauaji dhidi ya raïa yakitekelezwa na makundi ya wanamgambo.

Zaïdi ya makundi 120 ya wanamgambo wenyekumiliki silaha yametajwa yanaendeleza operesheni nchini ,huku milioni wakilazimika kuyahama makazi yao na kutorokea ambapo kunausalama.

RDCONGO/ Rutshuru/Kivu - Kaskazini/ Usalama/ FARDC/M23 - RDF.FARDC YAGOMBOA VIJIJI KADHA WILAYANI RUTSHURU VILIVYOKUA VI...
28/06/2022

RDCONGO/ Rutshuru/Kivu - Kaskazini/ Usalama/ FARDC/M23 - RDF.
FARDC YAGOMBOA VIJIJI KADHA WILAYANI RUTSHURU VILIVYOKUA VIMETEKWA NA M23/ by Madiba Mahoye.
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Majeshi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo FARDC yamuamka yanapambana na magaïdi wa M23 wanaodhiminiwa na Rwanda mapema asubuhi ya jumaïne hii tare 28 Juni 2022 ndani ya kitongoji cha Bweza, wiyani Rutshuru , Jimbo la Kivu ya Kaskazini . Duru zetu zimetuarifu kua waasi wa M23 wamejaribu kuzishambulia ngome za jeshi la serikali kwa kupitia eneo la Ruvumu katika kitongoji cha Kisigari mapema asubuhi majira ya saa kumi asubuhi ambapo raïa walikua wa kwanza kuwaona na kutoa taarifa kwa FARDC. Duru hizo zimeendelea kusema kua magaïdi hao wameanza kwa kuzunguka vituo vya FARC kwa kupita vijiji vya Nyaruhondo, ilitobowe kwa kuingilia katika vijiji vya Buchandaba,Ruseke na kwenye muinuko wa Bikona ambapo magaïdi hao wakaanza mashambulizi dhidi ya vituo vya kijeshi.

Hatimae majira ya saa mbili asubuhi mizinga na silaha nzito bila kusahau silaha sa m rashasha zilisikika kando na kilima cha Bikona ambacho ni muhimu baada ya kilima cha Mbuzi, k**a zilivyo arifu duru zetu. Rutsiro kwenye ulbali wa kilometa 11km Kusini - Mashariki na Rutsuru waasi wa M23 wamewaziwia raïa kutoka katika vijiji vyao wakati walipo jaribu kuyakimbia mapigano. M23, wamekua wakizidi mashambulizi sehembali mbali za Tutsuru kwa kuwaania kuzubiti wilaya hiyo ili waasi hao wauzibiti mji wa Rumangabo ambao pia nao ni mji muhumu sababu kunapatika kituo kikubwa cha mafunzo ya kijeshi.

Wakati mapigano hayo yakiarifiwa katika maeneo hayo, vijiji vya Kabaya/ Rumangabo na pembezuni mwake ambavyo vimesalia kuwa na usalama na raïa wanaendelea na shughuli zao k**a kawaïda ni vijiji muhimu katika eneo hilo duru zetu zimetaja.

FARDC, imewashikisha adabu M23, hadi kutimka.

Vyanzo vyetu vimeendelea kusela kua mapigano hayo yamesababisha raïa wa vijiji vya Ntamugenga , kitongoji cha Bweza, Bugina na Tanda wamekimbia

DRCONGO: Usalama / Ituri / by Madiba Mahoye----------------------------------------RAÏA 17 WAARIFIWA KUPOTEZA MAÏSHA BAA...
06/01/2022

DRCONGO: Usalama / Ituri / by Madiba Mahoye
----------------------------------------
RAÏA 17 WAARIFIWA KUPOTEZA MAÏSHA BAADA YA KUSHAMBULIWA NA WANAMGAMBO WA ADF/ NALU KIJI CHA WALESE VONKUTU.
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
*Shirika la raïa la Walese Vonkutu limejulisha kua mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022 wanamgambo wa ADF wametekeleza mauaji ya raïa 17. Shirika hilo la raïa linaiomba serikali kuzidisha harakati za kuwasaka manamgambo hao kusini mwa Irumu.*

Harakati za vitendo vya kigaïdi za kundi la wanamgambo wa ADF zaendelea kuyagharimu maïsha ya raïa wa mashariki ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo japokua zimeanzishwa operesheni kabambe za kuwasa wanamgambo hao tangu mikoa ya Ituri na Kivu ya Kaskazini litengwe kwenye hali ya dharura. Watu 17 wote wakiwa ni raïa ndio ambao wamekwisha uawa tangu tare 1 Januari hadi tarehe 3. Mauawaji hayo yametokea kwenye vijiji vya Lihaye na Israëli. Shirika la raïa la Walese Vonkutu lasema kua ni idadi kubwa ya raïa waliouawa na ADF katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka wa 2022. Mashambulizi hayo yametokea kwenye umbali wa kilometa 30Km na mji wa Komanda na kitongoji hicho cha Walese Vonkutu.

Tukio hayo yanajiongeza kwenye vitendo vya utekaji nyara wa watu 13 katiyao kukiwemwo watu 12 wakiwa ni wahanga wa vitendo vya kuchomewa majumba, uporwaji wa mifugo ni miongoni mwa vitendo vilivyo tekelezwa na magaïdi hao. Kimejulisha chanzo kimoja ambacha hakikupenda kudhihirika.

Ingawa hivo mkuu wa shirika la raïa eneo hilo la Walese Vonkutu ametaja kurizishwa na juhudi za na jeshi kwa kuwalinda raïa mitaani, lakini asikitishwa na hali ya ulinzi mdogo kwa raïa wanapo jielekeza mashambani hushambuliwa na waasi. Hivo kiongozi huyo wa shirika la raïa analiomba jesha la serikali kuendesha operesheni ya kuwasa maaduwi kutoka kando ya miji hadi misituni ( opérations de ratissage ).

'' _Sisi ni wakulima, tumeïshiwa na chakula apa kwetu Idaho. Watawala wetu wanapashwa kufanya kila namna kwakuzidisha mapambano dhidi ya wanamgambo. Vijiji kwetu ulinzi umeimarika,lakini mashambani kwetu tunapo endesheya shughuli hatuko salama._ Amesema hivo bwana'' Dieudonné Malangai.

Kiongozi wa shirika la raïa Walese Vonkutu pekee amesema kua mauaji hayo ni mauaji ya kikatili ambayo yametekelezwa na kundi hilo la magaïdi wa ADF tarafani Irumu katika kipindi cha siku tatu pekee za mwanzo wa mwaka. Amewatolea wito wakuu wa mamlaka kuzidisha mapambano dhidi ya wanamgambo wa ADF kwa operesheni za pamoja kwa ushirikiano baïna ya jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo FARDC na jeshi la ulinzi wa watu wa Uganda UPDF.

DRC: Usalama/ Ituri/ Kivu Kaskazini.WANAMGAMBO 7 WA ADF WAMALIZIWA MAÏSHA NA SILAHA NYINGI ZA KAMATWA NA VIKOSI VYA FARD...
28/12/2021

DRC: Usalama/ Ituri/ Kivu Kaskazini.

WANAMGAMBO 7 WA ADF WAMALIZIWA MAÏSHA NA SILAHA NYINGI ZA KAMATWA NA VIKOSI VYA FARDC./ By Madiba Mahoye
"""""''""""""""""""""""""""""""""""""""""""

Vikosi vya jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimetangaza( FARDC ), vimetangaza siku ya jumatatu tare 27 Desemba 2021i kua vimetia nguvuni waasi 7 wa allied demokratic forces ADF katika kijiji cha bandibese kwenye umbali wa karibu kilometa 18 na eneo la Komanda, tarafa la Irumu, jimbo la Ituri.

Katika mazungumzo na vyombo vya habari luteni Jules NGONGO msemaji wa jeshi la Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo FARDC jimboni Ituri, amesema kua silaha mbili za aïna ya AK47 na mabomu ya kienyeji yamek**atwa na jeshi la serikali ya Congo toka mikono ya wanamgambo wa ADF.

Asisitiza kwa kusema kua silaha hizo zimek**atwa na vikosi vya usalama baada ya mapambano yalio dumu kwa muda wa masaa kadhaa dhidi ya wanamgambo wa ADF.

DRCONGO: Muziki/ GENERAL DEFAO AÏAGA DUNI AKIWA NA UMRI WA MYAKA 63./ By Madiba Mahoye."""""""""""""""""""""""""""""""""...
28/12/2021

DRCONGO: Muziki/ GENERAL DEFAO AÏAGA DUNI AKIWA NA UMRI WA MYAKA 63./ By Madiba Mahoye.
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""

AMETUACHA ... Lolendo Matumona almaarufu '' Général Defao'' akiwa na umri wa myaka 63 ya kuzaliwa.

Asadikiwa kua ameiyaga dunia kwa maradhi ya kisukari na msongo wa virusi vya Covid - 19. Defao alikua nchini Cameroun kwa malengo ya tamasha lamuziki ambalo alikua amelianda kwa kuwaburudi mashabiki zake. Ghafla hali ya afya yake ilibadilika hivo ikalazimika apelekwe katika hospitali ya laquintini ya mjini Douala, ambapo hatmae umauti umemkuta usiku wa jumatatu tariki 27 Desemba 2021.

Lolendo Matumona amezaliwa mjini Kinshasa, mwezi Desemba 1958.

Akiwa kijana mdogo mwaka 1976 Defao alipenda kucheza muziki katika vikundi chipukizi vya muzi amavyo vilikua vinawajumuisha vijana katika mitaa ya jiji la Kinshasa. Hatimae mwaka 1981 Lolendo Matumona alijiunga na bendi ya muziki ya '' Le Grand Zaïko Wawa'' bendi ambayo ilikua ikiongozwa na mpiga gita mashuri enzi zile Félix Manuaku. Maraka ya kwanza wakaaji wa jiji la Kinshasa waligudua kipaji kisicho cha kawada cha kijana huyo mwenye mvuto wa kipekee na mtanashati ambapo alivutia wengi kwa sauti yake nyororo na mwenye madaha wakati akilisakata densi.

Myaka miwili baadae aliachana na Félix Manuaku na kujiunga na bendi ya ''Choc Stars'' ambapo alidumu kwa kipindi cha myaka 7 akishirikiana na nguli mwengine wa muziki wa Congo Bozi Boziana. Ezi hizo alipatafursa ya kujitokeza kwenye vipindi vya télévision kituambacho kulimzidishia umaarufu. Akiendelea kujizolea sifa rukuki mwanamuziki Lolendo Matumona Defao aliamua kuanzisha kundi lake binafsi.

1991, mwanamuziki huyo aliibuka na bendi yake ambayo aliibatiza jina la '' The Big Stars'', huku akijiwekea malengo ya kua mwanamuziki nyota ya Afrika.

Katika kipindi cha myaka mitano ya awali bendi ya ''Big Stars '' ilipata mafanikio makubwa kwa kutoa album ya nyimbo ambazo ziliwavutia mashabiki na wapenzi wa mwan**iki Defao, usoni mwa wazaïre wengi kijana huyo alionekana mfano bora kwa tasnia ya muziki. Umaarufu huo ulitokana na sauti yake yenye mvuto wakipekee. Nyimbo zake zilizingatiya asili ya mitindo ya rumba, sebene na hasa madoido na vidokezo kwenye uimbaji wake.

Mwaka 1994, Defao aliangusha kibao alicho kiita ''Famille Kikuta'' ambacho kilizidi kuzikonga nyoyo za mashabiki zake na kuzidi kujizolea umaarufu mkubwa. Kibao hicho cha ''Famille Kikuta'' kilishika nafasi ya kwanza katika hit parade ya muziki wa Zaïre enzi zile. Kibao hicho ''Famille Kikuta'' kinazungumzia mwanamke aliechwa na mumewe akimsihi mume arudi nyumbani.
Katika myaka ya 2.000, aliondoka nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuhamia katika nchi za Afrika mashariki ( Tanzania, na hatmae nchini Kenya ambapo alieshi kwa myaka mingi ). Nchini Kenya alieshi kwa kipindi kigumu ambapo alikabiliwa na matatizo ya kiuchumi hadi kupelekea kukosa hata pesa ya kulipa viza ( Visa ).

Mwaka 2019, Defao aliamua kurudi nyumbani nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kueshi ughaïbuni karibu myaka 20.
MWENYEZIMUNGU amlipe kadri na matendo yake!

FIZI: Usalama/ GUMINO YASHAMBULIA KITUO CHA FARDC HUKO KAMOMBO NA RAÏA WAKIMBIA MISITUNI/ By Madiba Mahoye."""""""""""""...
27/12/2021

FIZI: Usalama/ GUMINO YASHAMBULIA KITUO CHA FARDC HUKO KAMOMBO NA RAÏA WAKIMBIA MISITUNI/ By Madiba Mahoye.
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""

Mapigano makali yameripotiwa mapema asubuhi ya jumatatu tare 27 Desemba 2021, tarafani Fizi kijiji cha Kamombo, sekta ya Tanganyika groupementi Balala Kaskazini ( Balala Nord ).

Wapiganaji wanaodhaniwa kua ni wanamgambo wa Gumino na wash*tika wao wamekivamia mapema asubuhi vituo vya Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC ) vinavyopatikana katika vijiji vya Kamombo, Namara na Tchakira kwenye umbali usiozidi kilometa 17Kms mahariki na kijiji cha Mikenge. Duru nyingi zenyekuaminika zathibitisha kua vijiji hivyo vitatu vimetekwa na wanamgambo wa Gimino wanaongozwa na kanali muasi Michel Rukunda akijulikana kwa jinamaarufu MAKANIKA. Upande wa msemaji wa sekta ya operesheni Sokola ya pili kanda ya kusini mwa jimbo la Kivu Kusini Meja Dieudonné Kasereka kwa ush*tikiano na mkuu wa sekta ya Tanganyika John Mulondani wamethibitisha taarifa hizo lakini bilakutoa idadi ya vilivyo haribika.

Wanamgambo hao wa Gumino wameteleza mashambulio hayo dhidi ya vituo vya FARDC mapema alfajiri majiri saa kumi kwa kush*tukiza ambapo wanamgambo hao wamekilenga kituo cha wanajeshi wa bataliani ya 122 ya FARDC ikiongozwa na kanali YAUNDE ambao walikua wametia kambi sehemu hiyo hivi karibuni. Taarifa ambazo zimetufikia za eleza kua kiongozi wa bataliani hiyo kanali YAUNDE ameiyaga dunia kwenye mapambano hayo.

Kwa mujibu wa duru zetu kutoka Kamombo zasema kua raïa wamekimbilia msituni huku baadhi yao wakikimbilia Mikenge na Mikalati maeneo ya Itombwe katika tarafa la Mwenga wakiyatoroka makabiano.
>, ametaja hivo mkuu wa sekta ya Tanganyika bwana John Mlondani Mwimiwa.

Hadi mdahuu tunaandika taarifa hii, hali ya sintofahamu inaendelea kuripotiwa Minembwe - Centre, ambapo taarifa zaendelea kutujia zikisema kua wanamgambo wa Gumino wanaendelea kusonga mbele wakielekea kwenye makao makuu ya jeshi la FARDC brigade ya 12 inayo patikana Minembwe.

Kwa upande mwengine taarifa kutoka kwenye vyanzo vya kiusalama za eleza kua kikosi cha 121 cha bataliani ya makomando imekua mbiyoni kwa kujielekeza Mikenge eneo la Kamombo

Kivu - Kusini/ Usalama - FiziWANAMGAMBO WA GUMINO WATEKELEZA MAUAJI MAPYA KIJIJINI MIKENGE SEKTA YA ITOMBWE./ By Madiba ...
15/11/2021

Kivu - Kusini/ Usalama - Fizi

WANAMGAMBO WA GUMINO WATEKELEZA MAUAJI MAPYA KIJIJINI MIKENGE SEKTA YA ITOMBWE./ By Madiba Mahoye.
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""

Wapiganaji wa muungano wa vikundi vya wanamgambo wa Gumino / Twigwaneho, Androïde na Ted Tabara waasi wa Burundi wametekeleza mauaji dhidi ya raïa usiku wa tariki 15 Novemba 2021majira ya saa tano, katika kijiji cha Mikenge kinachopatikana ndani ya sekta ya Itombwe Kitongoji cha Bashimukinji 1er) tarafa la Mwenga jimboni Kivu Kusini.

Watu watano ndio wameuawa na wengine tisa wamejeruhiwa, huku nyumba kadhaa zimechomwa moto. Duru za mahali zimearifu.

Shirika jipya la raïa wa Congo NSCC eneo la Kusini mwa jimbo la Kivu limelaani washambulizi hayo huku likilaumu jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo FARDC na vikosi vya jeshi la umoja wa taïfa MONUSCO kwa kutokutoa msaada na kuwahami raïa.

André Byadunia Mashaka mwenyekiti wa shirika hilo jipya la raïa wa Congo jimboni amesema kua wanamgambo hao wametekeleza mauaji hayo karibu na kunako patikana kituo cha vikosi vya usalama .> amesema hiyo.

Duru hizo zinaïyomba serikali ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kurahisisha ili kuoatikane uwezekano wakuwafikisha raïa walio jeruhiwa kwenye hospitali kuu ya Bukavu ili wapate matibabu.

Hakuna taarifa ambayo imekwisha tolewa na maafisa wa kijeshi kutokana na uvamizi huo dhidi ya raïa wa kijiji cha Mikenge.

Eneo la nyanda za kati na juu zinazo inukia milima ya matarafa ya Mwenga, Fizi na Uvira yamekua uwanja wa vurugu ambazo zinayo ya gharimu maïsha ya raïa wasio na hatiya.

MAPIGANO MAKALI YA RIPOTIWA KATI YA JESHI LA JAMUHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO DHIDI YA WAASI WA M23./ By Madiba Mahoye....
09/11/2021

MAPIGANO MAKALI YA RIPOTIWA KATI YA JESHI LA JAMUHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO DHIDI YA WAASI WA M23./ By Madiba Mahoye.
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""

Idadi kubwa ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaoendelea kuingia Uganda kufuatia mapigano yaliozuka tangu usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu taree 08 Novemba 2021, imeleta mashaka kuhusu jinsi watakavyoshughulikiwa.
Huku serikali ya Uganda ikithibitisha mapigano hayo kutokea kwenye maeneo ya mji wa Bunagana kwenye mpaka wa Kusini Magharibi, shirika la umoja mataifa UNHCR pamoja na lile la Msalaba mwekundu wanahofia kuwa hawataweza kuwahudumia mamia ya wakimbizi hao wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Mamia ya wakimbizi wanaongia Uganda wanaelezea kuwa wanayakimbia mapigano yaliyozuka nchi kwao. Kulingana na msemaji wa jeshi la Uganda hadi sasa haijathibitishwa mapigano hayo ni kati ya majeshi ya serikali na kundi gani la wapiganaji, licha ya uvumi kuwepo kwamba ni wapiganaji wa M23.

Msemaji huyo Brigadier Flavia Bywekwaso amesema "Tumezungumza na watu walioko huko na wamethibitisha kuna mapigano kati ya majeshi ya DRC na kundi la wapiganaji lisilojulikana na hatuwezi kulitambua kwa sasa mapigano yalianza jana jioni na wakimbizi wamezifi kuingia kwa sababu yanaendelea."

Kwa upande mwengine afisaa muandamizi wa jeshi la FARDC, akiwa ni msemaji wa gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini Jemadari Syvain Kenge amesema kua jeshi la Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo limefaulu kuviteka vijiji vya Chanzu na Runyonyi ambavyo vilikua vimek**atwa na waasi hao wa M23, na kusema kua mapigano hadi sasa yanaendelea kuripotiwa kati pande zote mbili.

DRC: BURUNDI YA FICHUA NJAMA YA RWANDA DHIDI RDCONGO / by Madiba Mahoye-------------------------------------------------...
19/10/2020

DRC: BURUNDI YA FICHUA NJAMA YA RWANDA DHIDI RDCONGO / by Madiba Mahoye
-----------------------------------------------------------------------------
Waziri wa ulinzi wa Burundi na wapiganaji wa zamani injinia Alain Tribert MUTABAZI, ameïshutumu Rwanda kwa kuwasajili kijeshi vijana wa Burundi kwa malengo ya kuihujumu kijeshi nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Zowezi hilo limekua likiendeshwa na Rwanda tangu mapigano mapya ya zuke huko katika nyanda za juu za vilima vya Fizi - Minembwe, Uvira - Bijimbo na Mwenga, kwa malengo ya kuwasaïdia wanamgambo wa Gumino ikiwa ni watutsi wenye asili ya Rwanda k**a inavyo daïwa na raïa wa Congo.
Taarifa hizo pia zimezunguziwa kwenye kikao cha mawaziri wa ulinzi wa nchi za jumuia ya ukanda wa maziwa makuu, kikao kilicho fanyika tare 14 Oktoba mwaka huu kwa njia ya vidéoconférence, kikiendeshwa na waziri wa ulinzi wa Congo-Brazzaville akiwa ndie mwenyekiti wa baraza hilo.
Nchi za Zambia ,Uganda, Burundi, Tanzania, Rwanda , Angola , Afrika ya kati, Sudani Kusini zilikuwa wenyeji katika mkutano wa nchi hizo zikiwa zimewakilishwa na mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo.

Katika mkutano huo wa mawaziri wa ulinzi,swala na mbinu za kumaliza uvunjifu wa amani katika ukanda wa maziwa makuu limepewa kipau mbele na kutafuta mbinu m'badala ili amani idumu. Mawaziri hao wa ulinzi pia wametizamia kwa pamoja jinsi ya kuongezea uwezo kwa kikosi cha kiukanda,FIB, ambacho kinatarajiwa kushika nafasi ya jeshi la MONUSCO linalo hudumu nchini DRC likiwa linamaliza muhula wa kusimamia amani nchi humo ifikapo Desemba mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumzia katika kikao hicho waziri Aimé NGOI MUKENA, waziri wa ulinzi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amekumbusha mawaziri wenzake wa ulinzi wa nchi za ukanda huu kufanya iwezekanavyo kwa kuziba pengo katika nyazifa zinazo baki kwenye ofisi hiyo n**i zote zifanyike k**a inavyo tarajiwa, huku waziri huyo akikazia kuimarishwa kwa kitengo kinacho husika na amani na usalama. Waziri NGOI MUKENA amependekeza DRC kuchukua tena nafasi ya uwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwenye muhula mwengine.

Rwanda imekua ikishotwa kidole mara kadha kwa kuyafadhili makundi ya watutsi wa kinyamulengo wenye malengo ya kujipatia nchi huru kutoka sehemu ya ardhi ya DRC tangu wakati wa uasi wa RCD Goma,iliokua ikiongozwa na Azarias RUBERWA myaka ya 1998 ambae ni waziri wa serikali za vijiji nchini. Kundi ambalo linalo fadhiliwa na Rwanda, ni kundi kundi la Gumino linalo ongozwa na kanali Michel Rukunda alias Makanika akishirikiana na waasi wa Burundi wa Red Tabara ambao wanayumbisha usalama siku hizi nchi Burundi kwa ushirikiano na Wanyarwanda, k**a zinazo ripoti duru zetu.

Itafahamika kuwa polisi ya Burundi imenya msako siku za hivi karibuni katika mikoa ya Gitega na Makamba na kuwak**ata mamia ya wanyamulenge ambao wamebainika kua ni wahamiaji haramu ambao wanaeshi bila vitambulisho nchini Burundi.

Wakuu wa mamlaka nchini Burundi wamekuwa na hofu dhidi ya watu wenye kuongea lugha ya kinyarwanda kutokana na uhusiano mdogo wa kidiplomasa kati ya nchi hizo mbili ulio haribika tangu wakati hayati raïsi Pierre NKURUNZIZA wa Burundi ajitangaze k**a mgombea kiti cha uraïsi katika uchaguzi wa mwaka wa 2015.

Burundi na Rwanda zimekua majirani wenye uhasamu mukubwa.

*BURUNDI NA RWANDA ZAANZA MAZUNGUMZO YA KUREJESHA MAHUSIANO* .Maafisa wa usalama wa Burundi na Rwanda wameanza mazungumz...
26/08/2020

*BURUNDI NA RWANDA ZAANZA MAZUNGUMZO YA KUREJESHA MAHUSIANO* .

Maafisa wa usalama wa Burundi na Rwanda wameanza mazungumzo ya kurejesha uhusiano, ikiwa ni mara ya kwanza mazungumzo kufanyika ndani ya kipindi cha miaka mitano wakati nchi hizo zikiwa kwenye mkwamo wa kisiasa.

Mazungumzo hayo yaliyosimamiwa na Idara ya Usalama ya Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) yalifanyika kwenye mpaka wa Nemba ulioko mashariki mwa Rwanda kwenye eneo ambalo halimilikiwi na Rwanda wala Burundi.

Ulikuwa mkutano ulioukutanisha ujumbe mzito kutoka kila upande huku maafisa wa idara ya ujasusi kutoka pande hizo tatu - Rwanda, Burundi na ICGLR - ukitangaza mtazamo wake juu ya mkutano huo wa kwanza ndani ya kipindi cha miaka mitano tokea nchi mbili hizo zilipoingia kwenye mzozo wa kidiplomasia.

Mkuu wa ujumbe wa Rwanda, Brigedia Jenerali Vincent Nyakarundi, alisema nchi yake "inathamini nafasi ya ICGLR katika kutatua mizozo, na kujituma kwa wajumbe wake ambao hufanya kila jitihada za kurejesha usalama kwenye eneo hili la maziwa makuu na siku zote kupambana ili hali ya ujirani mwema na kuaminiana kwenye mataifa hayo iendelee kuwepo."

"Hii ndiyo sababu kuu yetu sote kukutana hapa hii leo na namini baada ya mkutano huu, wote tutakuwa tumekwishatambua chanzo cha ukosefu wa amani unaosababishwa na makundi yenye silaha ya CRND na FNL yanayoisumbua Rwanda kupitia msitu wa Kibira upande wa Burundi.'' Alisema Nyakarundi, ambaye pia ni mkuu wa idara ya ujasusi kwenye jeshi la Rwanda.

*Burundi yataka ushirikiano urudi*

Kwa upande wake, mkuu wa ujumbe wa Burundi, Kanali Ernest Musaba, alisema hali mbaya iliyopo ilikuwa ikichochewa pia na hali ya usalama kwenye eneo la mashariki mwa DRC, hususan katika mpaka unaozitenganisha nchi za Rwanda na Burundi, ambayo si nzuri.

*Rais Paul Kagame wa Rwanda*

"Mkutano huu kwa hiyo ni fursa nzuri kwetu sote kuzungumza kwa uwazi juu ya sababu zinazochangia usalama huo mdogo na tunaamini kuwa hakutakuwepo na upendeleo wowote, ili ukweli uwe

Beni: Un militaire condamné à la peine capitale après avoir été reconnu coupable du meurtre d’un civil******************...
15/08/2020

Beni: Un militaire condamné à la peine capitale après avoir été reconnu coupable du meurtre d’un civil
********************************************



Le tribunal militaire de garnison de Beni Butembo qui siégeait en audience foraine et en flagrance à Kantine en territoire de Beni a condamné ce samedi 15 août 2020, le militaire M’putu Kanka Jeremie à la peine capitale.

Cet élément Fardc a été reconnu coupable du meurtre d’un jeune garçon Kakule Silwamughuma alliance Lofo, tué le 13 août dernier à Kantine. L’homme doit aussi payer 100 mille dollars americains, selon ce jugement.

A la question de savoir si le prévenu peut subir une sanction penale et une peine exemplaire, à la majorité de voix de ses membres a repondu par oui par consequent le condamne à la peine de mort et le condamne à la peine complementaire qui est la degradation donc il ne peut plus porter la tenue militaire ni nos insignes” peut-on lire dans ce jugement.

Ce cas de meurtre avait provoqué ce vendredi un soulevement populaire à Kantine. D’ailleurs, la société civile annoncait des actions de grandes envergures pour pousser la justice à se saisir de ce dossier.

*WANAMGAMBO WENYE MFUNGAMANO NA DAESH WAMETEKA BANDARI MUHIMU NCHINI MSUMBIJI.* Vyombo vya usalama nchini Msumbiji vimet...
13/08/2020

*WANAMGAMBO WENYE MFUNGAMANO NA DAESH WAMETEKA BANDARI MUHIMU NCHINI MSUMBIJI.*

Vyombo vya usalama nchini Msumbiji vimetangaza kuwa, wapiganaji wa kundi lenye mfungamano na kundi la kigaidi la Daesh wameiteka na kuidhibiti bandari moja muhimu kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa vyombo vya usalama wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi jana walifanikiwa kudhibiti bandari muhimu yenye utajiri wa gesi katika mji wa Mocimboa da Praia uliopo kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, wanamgambo hao ambao wanajiita Ahlu Sunnah Wa-Jamaa wamefanikiwa kuidhibiti bandari hiyo yenye utajiri baada ya mapigano na mashambuluo ya wiki katikaa baina yao na vikosi vya serikali.

Wakati huo huo vikosi vya ulinzi na usalama vya Msumbiji (FDS) vimetangaza kuwa, vimewaua magaidi 59 katika wikki za hivi karibuni katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado kufuatia operesheni za vikosi hivyo dhidi ya wanamgambo wa Ahlu Sunnah Wa-Jamaa.

Uasi wa wanamgambo nchini Msumbiji umeibuka na kuwa vita vya wazi katika miaka ya ya hivi karibuni, huku kukiwa na ripoti za mauaji, watu kukatwa vichwa na kutekwa kwa miji miwili katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado.

Vijiji vya mkoa huo wa Cabo Delgado ulioko kaskazini mwa Msumbiji tangu mwezi Oktoba mwaka 2017 vimekuwa vikishuhudia mashambulizi ya umwagaji damu ya wanachama wa kundi linalojiita Ahlu Sunna Wal Jamaa, ambao wakazi wa maeneo hayo wanawatambua kwa jina la al-Shaabab.

Kundi hilo la kigaidi limekuwa likifanya mashambulizi hayo licha ya serikali ya Msumbiji kutuma wanajeshi na polisi katika maeneo hayo ambayo yapo katika mpaka wa nchi hiyo na Tanzania.

Adresse

La Radio Communautaire Fizi FM, Est Situé à L'est De La République Démocratique Du Congo Au Sud Est De La Province Du Sud Kivu, Sur Le Litoral Du Lac Tanganyika
Baraka

Téléphone

+243819492635

Site Web

Notifications

Soyez le premier à savoir et laissez-nous vous envoyer un courriel lorsque RCFI. FM publie des nouvelles et des promotions. Votre adresse e-mail ne sera pas utilisée à d'autres fins, et vous pouvez vous désabonner à tout moment.

Partager