02/11/2025
Marekani: RAIS DONALD TRUMP WA MARZKANI ATISHIA KUISHAMBULIA KIJESHI NCHI YA NIGERIA./ Mahoye Madiba.
"""""""""""""""""""""""''''''''""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Rais Donald Trump wa Marekani, ameiagiza Wizara ya Ulinzi ya Nchi yake ‘Pentagon’ kujiandaa kwa uwezekano wa kuchukua hatua za Kijeshi nchini Nigeria, huku akiendelea kuishutumu nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa kufanya vitendo vya vurugu dhidi ya Wakristo — shutuma ambazo Nigeria imekanusha mara kadhaa.
Kupitia chapisho katika mitandao ya kijamii alilolielekeza kukosoa kile alichokiita “Mauaji makubwa ya Wakristo” nchini humo, Rais Trump aliandika kwamba Marekani “itasitisha mara moja misaada yote na usaidizi kwa Nigeria” na akaonya Serikali ya Nigeria “ichukue hatua haraka.”
Katika ujumbe wake mrefu, Trump alisema kuwa Marekani “huenda ikaingia katika nchi hiyo iliyopoteza heshima, ‘tukiwa tumebeba silaha,’ ili kuwaangamiza kabisa Magaidi wa Kiislamu wanaotekeleza uhalifu huu wa kikatili.”
“Ninaiagiza Wizara yetu ya Vita kujiandaa kwa hatua yoyote itakayohitajika,” aliandika Trump.
“Tukishambulia, itakuwa haraka — sawa na jinsi Magaidi hao wanavyowashambulia Wakristo! ONYO: SERIKALI YA NIGERIA ICHUKUE HATUA HARAKA!”
Tangazo hilo linakuja baada ya Trump kuishutumu Nigeria siku ya Ijumaa kwa kukiuka uhuru wa kidini, akidai kwamba “Ukristo uko katika hatari kubwa ya kutoweka nchini Nigeria” na kuitaja nchi hiyo k**a “Nchi ya Wasiwasi Maalum” chini ya Sheria ya Kimataifa ya Uhuru wa Kidini.