Sauti ya dunia Newsweek

01/07/2024
17/05/2024

Qu'en pensez-vous ? 🙄

28/04/2024

Silencing my haters ,🤫

16/12/2021

Baraza la Usalama la UN laombwa kujadili Korea Kaskazini.

Baadhi ya wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa ikwemo Japan, wamewaomba wenzao miongoni mwa wanachama 15 kwenye baraza hilo kufanya kikao cha faragha ili kuzungumzia hali inayoendelea ya ukiukaji wa haki za binadamu Korea kaskazini.

Balozi wa Marekani kwenye baraza hilo Linda Thomas Greenfield wakati akizungumza kwa niaba ya Marekani,Uingereza, Estonia, Ufaransa, Ireland, Japan na Norway ambao wote ni wanachama isipokuwa Japan,amesema kwamba ni lazima mwenendo wa Korea kaskazini wa kukiuka haki za binadamu pamoja na matumizi ya silaha nzito upewe kipaumbele na kukomeshwa kwa kuwa unahatarisha usalama wa kimataifa.

Mwaka 2014, ripoti kutoka kwa tume maalum ya uchunguzi iliyobuniwa na baraza hilo ilifichua hali halisi ya ukatili mkubwa dhidi ya binadamu, unaoendelea kutekelezwa Korea kaskazini. Tangu wakati huo , baraza hilo limekuwa likizungumzia hali hiyo kila Decemba licha ya baadhi ya wanachama kusema wamba halifai kushikilia jukumu hilo.

16/12/2021

Bunge la Marekani laidhinisha kikomo cha ongezeko la deni la taifa.

Baraza la Wawakilishi lilipitisha kikomo cha ongezeko la deni, mapema Jumatano kwa kura 221 kwa 209 na kura moja pekee ya Republican iliyounga mkono.

Uidhinishaji wa Seneti ulikuja Jumanne kwa kupitishwa na Wademocrat 50 kwa kura ya “Ndio” huku Warepulikan 49 wakipinga.

Bunge la Marekani limeidhinisha hatua ya kuongeza kiwango cha deni la taifa na kupigia kura ili kuepuka kushindwa kulipa deni. Rais Joe Biden bado anahitaji kutia saini sheria hiyo hatua ya mwisho katika mchakato huo ambao umewagawa waDemocrats na waRepublicans kwa miezi kadhaa.

Baraza la wawakilishi lilipitisha kikomo cha ongezeko la deni, mapema leo jumatano kwa kura 221 kwa 209 na kura moja pekee ya Republican iliyounga mkono. Uidhinishaji wa seneti ulikuja Jumanne kwa waDemocratic 50 kupiga kura ya “Ndio” na waRepuplican 49 wakipinga.

16/12/2021

Biden aahidi msaada kwa watu walioathirwa na dhoruba Kentucky.

Rais wa Marekani Jumatano ametembelea jimbo la Kentucky ili kujionea mwenyewe hasara iliyosababishwa na vimbunga kadhaa vya nguvu sana na kuacha takriban watu 74 wamekufa huku maelfu wengine wakiwa hawana makazi mwishoni mwa juma.

Ijumaa na Jumamosi liyopita, Biden aliarifiwa kuhusu hali ilivyokuwa kuhusu juhudi za uokozi kutoka na dhoruba ambayo ilipiga vibaya jimbo la Kentucky na majimbo jirani. Alitembea kwa helikopta majimbo yaliyokumbwa na dhoruba ambako alishuhudia majengo yalioporomoka pamoja na manusura waliokuwa wakitembea barabarani.

Kiongozi huyo wakati wa ziara ya Jumatano ameahidi msaada kutoka serikali kuu akisema kwamba kutokana na uharibifu uliotokea, baadhi ya miji italazimika kujengwa upya. Gavana wa jimbo la Kentucky Andy Beshear amesema Jumanne kwamba zaidi ya watu 100 hawajulikani walipo jimboni humo na hasa kwenye mji mdogo wa Dawson Springs wenye takriban 3,000.

Msemaji wa ikulu ya Marekani Karine Jean Pierre aliwaambia wanahabari waliokuwa ndani ya ndege ya rais kwamba ujumbe wa rais ulikuwa wa kuwahakikishia watu walioathirika kwamba serikali yake itafanya kila iwezalo kuhakikisha wamerudi kwenye hali ya kawaida ya maisha.

16/12/2021

Serikali ya Israel kuchangia chanjo milioni 1 za virusi vya corona kwa mpango wa COVAX.

Serikali ya Israel siku ya Jumatano imesema itachangia chanjo milioni 1 za virusi vya corona kwa mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wa COVAX.

Serikali ya Israel siku ya Jumatano imesema itachangia chanjo milioni 1 za virusi vya corona kwa mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wa COVAX.

Wizara ya Mambo ya Nje ilisema chanjo za AstraZeneca zitahamishwa katika wiki zijazo, uamuzi ambao ulikuwa sehemu ya kuimarisha uhusiano wa Israeli na nchi za Kiafrika.

Nimefurahi kuwa Israeli inaweza kuchangia na kuwa mshirika katika kutokomeza janga hili ulimwenguni, Waziri wa Mambo ya nje Yair Lapid alisema.

Tangazo hilo lilisema kuwa chanjo hizo zitafikia karibu robo ya nchi za Afrika, ingawa haikutoa orodha. Israel ina uhusiano wa karibu na mataifa kadhaa ya Afrika, yakiwemo Kenya, Uganda na Rwanda. Israel pia ilianzisha uhusiano na Sudan mwaka jana k**a sehemu ya mfululizo wa mapatano yaliyosimamiwa na Marekani.

15/12/2021

Hali ya ukame yaendelea kudorora Somalia.

Ona maoni

Hali ya ukame nchini Somalia inasemekana kudorora licha ya kuwepo kwa mvua katika baadhi ya maeneo kulingana na afisa wa ngazi ya juu kwenye huduma za kibinadamu.

Kulingana na Ian Ridley anayeongoza ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya masuala ya kibinadamu, nchini Somalia, wakati wa mahojiano na VOA amesema mvua za hivi karibuni hazitoshi na kwamba ukame umeendelea kushuhudiwa.

Ridley amekuwa akitembelea maeneo yalioathiriwa zaidi katika wiki za karibuni. Wakati akizungumza kutoka mji mkuu wa Mogadishu, Ridley amesema kwamba visima vilivyoko tayari vimeanza kukauka na kwa hivyo kuongeza hitaji la visima vyenye kina kirefu.

Ameongeza kusema kwamba hali iliyoko imelazimisha watu kuhama makwao, baadhi wakisafiri umbali wa kati ya kilomita 30 na 40 kutoka maeneo ya mashambani hadi kwenye maeneo ya mijini.

Amesema pia kwamba kuna hatari kubwa ya kutokea kwa magonjwa k**a vile kipindupindu huku surua ikisemekana kuongezeka miongoni mwa watu walioko kwenye makambi.

15/12/2021

Utafiti unasema chanjo ya Pfizer-BioNTech inafanyakazi kiasi kuzuia Omicron Afrika Kusini.

logo
Jumatano, Desemba 15, 2021 Local time: 20:13
HABARI
Utafiti unasema chanjo ya Pfizer-BioNTech inafanyakazi kiasi kuzuia Omicron Afrika Kusini
15 Desemba, 2021

Ona maoni

Utafiti mmoja umeonyesha chanjo ya Covid-19 ya Pfizer-BioNTech inafanyakazi kiasi nchini Afrika Kusini katika kuwalinda watu wasipate maambukizi ya virusi nje ya hospitali toka aina mpya ya virusi Omicron kugunduliwa.

Utafiti huo uliofanyika kiuhalisia na matokeo yake kuchapishwa Jumanne, unaonyesha kati ya Novemba 15 mpaka Desemba 7 watu ambao walikuwa wamepata dozi mbili za chanjo walikuwa na asilimia 70 ya kuwawezesha wasilazwe hospitali ikiwa chini ya asilimia 93 kulingana na takwimu za wimbi la maambukizo ya virusi vya Delta.

Inapokuja suala la kujiepusha maambukizo kwa pamoja utafiti uliofanywa na taasisi ya bima binafsi ya Afrika Kusini, Discovery Health, umeonyesha kwamba ulinzi dhidi ya maambukizi ya Covid-19 umeshuka mpaka asilimia 33 kutoka asilimia 80 ya awali.

Takwimu kutokana na uchambuzi uliofanyika kiuhalisia ni za kwanza kuonyesha namna chanjo zinaweza kufanyakazi dhidi ya virusi vipya vya Omicron nje ya tafiti za kimaabara ambazo mpaka sasa zimeonyesha kupungua uwezo katika kukabiliana na virusi.

Matokeo ya utafiti yalitegemea uchambuzi wa taasisi ya Discovery ya utafiti wa kitabibu na timu za wataalamu wakishirikiana na baraza la utafiti wa kitabibu la Afrika Kusini.

Afrika Kusini iliufahamisha ulimwengu mwezi Novemba uwepo wa virusi vipya ya Omicron, na kutoa ishara kwamba vinaweza kusababisha wimbi lingine la maambukizi duniani, na kusabaisha kuwekwa marufuku za kusafiri kwenda kusini mwa Afrika.

Maambukizi ya Afrika Kusini kwa siku yameongezeka mpaka zaidi ya 20,000, huku asilimia 35 ya vipimo vikirejea na maambukizo katika viambatanisho vya Jumanne na zaidi watu ya 600 wakilazwa na vifo vikiwa 24.

15/12/2021

Afrika yalegea katika utoaji wa chanjo za Covid-19.

Shirika la afya duniani WHO Jumanne limesema kwamba huenda Afrika isifikie lengo lake la kutoa chanjo kwa asilimia 70 ya watu wake bilioni 1.3 dhidi ya COVID kufikia nusu ya pili ya 2024, lengo ambalo tayari mataifa mengi tajiri yamefikia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, onyo hilo limetolewa wakati ulimwengu ukikabiliana na aina mpya ya virusi vya omicron. Baadhi ya mataifa tajiri yameidhinisha dozi ya tatu ya booster kwa watu wake, wakati chini ya asilimia 8 ya watu wa Afrika wakiwa wamepokea chanjo kamili.

Flavia Senkubuge ambaye ni mkuu wa chuo cha dawa cha Afrika kusini wakati akizungumza na wanahabari kwenye kikao cha WHO, amesema kwamba tatizo hilo haliwezi kumalizika k**a ulimwengu hautashirikiana pamoja.

Ni mataifa 20 pekee kati ya 54 barani Afrika ambayo yametoa chanjo kamili kwa takriban asilimia 10 ya watu wake wakati mataifa 10 pekee yakiwa yametoa chanjo chini asilimia 2 kwa watu wake barani humo. Kufikia sasa Afrika imepokea takriban dozi milioni 434 wakati 910,000 zikisemekana kuharibika kwenye mataifa 20.

15/12/2021

Mahak**a kuu ya Afrika kusini imeamuru Rais wa zamani nchini humo Jacob Zuma arudi gerezani baada ya kutengua uamuzi wa kumwachilia kwa msamaha wa kiafya, uamuzi wa mahak**a ulionyeshwa Jumatano.

Jacob Zuma mwenye umri wa miaka 79 alianza msamaha wa matibabu mwezi Septemba na anatumikia kifungo cha miezi 15 kwa kuidharau mahak**a baada ya kupuuza maagizo ya kushiriki katika uchunguzi wa rushwa.

Zuma mwenye umri wa miaka 79 alianza msamaha wa matibabu mwezi Septemba na anatumikia kifungo cha miezi 15 kwa kuidharau mahak**a baada ya kupuuza maagizo ya kushiriki katika uchunguzi wa rushwa. Katika mwezi huo huo mahak**a kuu ya Afrika kusini ilitupilia mbali ombi lake la kutengua hukumu hiyo. Michakato ya kisheria dhidi ya Zuma kwa madai ya rushwa wakati wa utawala wake wa miaka tisa inatazamwa na wengi k**a mtihani wa uwezo wa Afrika kusini baada ya enzi ya ubaguzi kuhusu uwezo wake kuimarisha utawala wa sheria hasa dhidi ya watu wenye madaraka na wenye uhusiano na uongozi.

Zuma alikwenda mwenyewe hapo Julai 7 kuanza kifungo chake na kusababisha ghasia mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini Afrika kusini katika kipindi cha miaka kadhaa huku wafuasi wa Zuma waliokuwa na hasira wakiingia mitaani.

Adresse

Muhungu
Bukavu

Téléphone

+243970863452

Site Web

Notifications

Soyez le premier à savoir et laissez-nous vous envoyer un courriel lorsque Sauti ya dunia publie des nouvelles et des promotions. Votre adresse e-mail ne sera pas utilisée à d'autres fins, et vous pouvez vous désabonner à tout moment.

Contacter L'entreprise

Envoyer un message à Sauti ya dunia:

Partager

Type