
24/06/2025
“Miaka 10 iliyopita ulikataa kuchukua pesa kutoka kwangu kwa ajili ya collabo, ulijitolea kuifanya bure.” – Diamond Platnumz
“Nilipokuwa nikijaribu kupata nafasi huko Nigeria miaka 10 iliyopita, ulitoa beti (verse) ambayo ilibadilisha kabisa maisha yangu ya muziki. Ulilipia nauli yako mwenyewe, ukaja Tanzania tukarekodi. Tulipouliza kuhusu malipo, ukasema hakuna shida – ni sawa tu. Kila wakati kwako imekuwa ni kuhusu kukuza wengine. Unapenda kuwaona wengine wakikua, na ndiyo maana umekuwa mkubwa zaidi – 001 wa Afrika. Wanasema hakuna mtu mzuri, lakini wewe ni mzuri ndugu yangu. Hakuna anayeweza kujifanya kuwa mzuri kwa miaka 10. Mungu aibariki familia yako.” – Amesema Diamond Platnumz
Omo, si leo tu bwana – miaka 10 iliyopita? Dah! Kumbe 001 amekuwa akiinua wengine toka zamani. Ni miaka 10 na bado anaendelea kufanya hivyo.
Funzo: Davido anastahili kila kitu kizuri anachopata.