DAKIKA MEDIA Informations de contact, plan et itinéraire, formulaire de contact, heures d'ouverture, services, évaluations, photos, vidéos et annonces de DAKIKA MEDIA, Chaîne de télévision, Tanganyika, Lubumbashi.
(1)

Kwa maoni, ushauri na maswali
Wht Chanel : https://whatsapp.com/channel/0029Vb9tu50AInPmpK5dWd2c

TikTok, Instagram, YouTube, whatsapp, telegram, twitter: DAKIKA MEDIA

Trump : Personne ne sait qui dirige l'Iran.Le président américain Donald Trump a déclaré qu'il existait une incertitude ...
08/10/2026

Trump : Personne ne sait qui dirige l'Iran.
Le président américain Donald Trump a déclaré qu'il existait une incertitude concernant les dirigeants iraniens, affirmant que les principaux responsables du pays ainsi qu'un second groupe de dirigeants avaient disparu, et que personne ne sait avec certitude qui prend les décisions dans ce pays.
Trump a fait ces déclarations ce mardi 6 octobre 2026, lors d'une allocution lors d'un événement organisé par l'entreprise Anduril Industries à Sparrows Point, dans le Maryland, aux États-Unis. Cette déclaration intervient alors que la guerre entre les États-Unis, Israël et l'Iran se poursuit dans un climat d'incertitude autour de la direction de Téhéran.
Trump a déclaré : « Leurs dirigeants sont partis, leur deuxième groupe de dirigeants est également parti, et le plus gros problème que j'ai est que personne ne sait qui dirige réellement la nation. »
Ces propos ont reçu une réponse du ministère iranien des Affaires étrangères, qui a affirmé que les États-Unis savent très bien qui représente l'Iran et comment fonctionne le système de prise de décision dans le pays.
Le porte-parole du ministère iranien des Affaires étrangères, Esmaeil Baghaei, a déclaré que le problème ne réside pas dans une prétendue méconnaissance de la direction iranienne, mais plutôt dans ce qu'il a qualifié de positions contradictoires et de déclarations confuses de la part des responsables américains.
Les propos de Trump surviennent après la mort de l'ayatollah Ali Khamenei lors du premier jour de la guerre déclenchée le 28 février. Son fils, Mojtaba Khamenei, lui a succédé, mais il n'aurait jamais été vu en public depuis qu'il a été blessé lors de l'attaque qui a coûté la vie à son père, bien que les responsables iraniens affirment que leur Guide suprême est en sécurité et poursuit ses fonctions normalement.

Trump: Hakuna anayejua anayeiongoza Iran.Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuna sintofahamu kuhusu uongozi wa Iran...
08/10/2026

Trump: Hakuna anayejua anayeiongoza Iran.

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuna sintofahamu kuhusu uongozi wa Iran, akidai kuwa Viongozi wakuu wa nchi hiyo pamoja na kundi jingine la Viongozi wameondoka na kwamba hakuna anayejua kwa uhakika ni nani anayefanya maamuzi nchini humo.

Trump alitoa kauli hiyo Jumanne, Oktoba 6, 2026, wakati akizungumza katika hafla ya kampuni ya Anduril Industries iliyofanyika Sparrows Point, Maryland, Marekani. Kauli hiyo imekuja wakati vita kati ya Marekani, Israel na Iran vikiendelea huku kukiwa na hali ya sintofahamu kuhusu uongozi wa Tehran.

Trump alisema: "Viongozi wao wameondoka, kundi lao la pili la Viongozi pia limeondoka, na tatizo kubwa nililonalo ni kwamba hakuna anayejua ni nani anayeliendesha taifa.”

Kauli hiyo imejibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, ambayo imesema Marekani inafahamu vizuri ni nani anayewakilisha Iran na namna mfumo wa kufanya maamuzi nchini humo unavyofanya kazi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, alisema tatizo halipo katika kutokujulikana kwa uongozi wa Iran, bali katika kile alichokiita misimamo inayokinzana na kauli zinazochanganya kutoka kwa Afisa wa Marekani.

Kauli za Trump zimekuja baada ya Ayatollah Ali Khamenei kuuawa katika siku ya kwanza ya vita vilivyoanza Februari 28. Mwanawe, Mojtaba Khamenei, alirithi nafasi hiyo, lakini inasemekana hajawahi kuonekana hadharani tangu alipoumia katika shambulio lililomuua Baba yake licha ya Viongozi wa Iran kusema kwamba Kiongozi Mkuu wao yupo salama na aendelea na majukumu yake k**a kawaida.


MASTER UVA AJA NA MRADI MPYA AKISHIRIKIANA NA MAREHEMU MR GAVE, MIEZI KADHAA BAADA YA KIFO CHA MSANII HUYO NGULIMsanii M...
03/10/2026

MASTER UVA AJA NA MRADI MPYA AKISHIRIKIANA NA MAREHEMU MR GAVE, MIEZI KADHAA BAADA YA KIFO CHA MSANII HUYO NGULI

Msanii Master Uva anatarajiwa kuja na mradi mpya uitwao “NIKO SAWA”, ambao amefanya akiwa na marehemu mwanamuziki nguli Mr Gave, miezi kadhaa baada ya msanii huyo kuaga dunia.

Hata hivyo, swali linaloibuka ni: Je, Master Uva tayari amemalizana na mikataba pamoja na usimamizi (management) wa marehemu Mr Gave?

Swali hili linaibuka kutokana na tukio la awali ambapo msanii mmoja aliyekuwa ametoa wimbo wa pamoja na Mr Gave alikumbana na vikwazo kutoka kwa management ya msanii huyo, na baadaye kulazimika kuushusha wimbo huo kutokana na masuala yanayohusiana na haki za watunzi na hakimiliki (droit d’auteur).

Katika ujumbe wake, Master Uva ameandika:

“Wanafamilia, habari njema kwenu ni hii hapa… Ungana na channel yangu mapema kabla ya wimbo huu kuteremshwa.

with iko YouTube, tunasubiri tu siku ifike 🫀.”

🔗 KIUNGO CHA WIMBO:
https://youtube.com/watch?v=H6nv3keAPfY&si=myWWmrviP6NFGlxz

Mimi ni Rabi Jeremie OG, hii ni Dakika Media — zaidi ya habari.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limempa mwezi mmoja wa uangalizi Msanii wa Bongo Fleva, Rajab Abdul Kahali maarufu k**...
03/10/2026

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limempa mwezi mmoja wa uangalizi Msanii wa Bongo Fleva, Rajab Abdul Kahali maarufu k**a Harmonize, baada ya kutekeleza masharti aliyokuwa amepewa kabla ya kuendelea na shughuli zake za sanaa.

Katika taarifa iliyotolewa na BASATA, Baraza hilo limesema Harmonize alifika BASATA Oktoba 2, 2026 na kutekeleza masharti hayo, lakini ataendelea kuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha mwezi mmoja.

BASATA imeonya kuwa haitasita kuchukua hatua dhidi ya Harmonize endapo hatatekeleza masharti aliyowekewa katika kipindi hicho.

Aidha, Baraza hilo limewataka Wasanii kuendelea kuzingatia Sheria, Kanuni, miongozo na maadili yanayosimamia shughuli za sanaa Nchini, ikiwemo katika uzalishaji na usambazaji wa kazi za sanaa.

 Mchekeshaji kutoka nchini Tanzania, Mr. Mwanya, amesema kuwa kuwa staa mkuu Diamond Platnumz si kazi rahisi na inahitaj...
02/10/2026


Mchekeshaji kutoka nchini Tanzania, Mr. Mwanya, amesema kuwa kuwa staa mkuu Diamond Platnumz si kazi rahisi na inahitaji moyo thabiti, kwani anakabiliwa na vita kubwa inayomuandama.
Mr. Mwanya amesema Diamond amekuwa akijitoa kwa asilimia kubwa kuwasaidia watu wengi, lakini malipo anayoyapata kutoka kwa jamii ni tofauti kabisa na kile anachokifanya.
Ameeleza kwa undani kuwa, licha ya misaada mbalimbali anayoitoa makanisani na misikitini, bado watu wengine wanamchukulia k**a shetani, jambo ambalo si sawa kabisa.
Mr. Mwanya ameongeza kuwa ndio maana Diamond aliwahi kusema kuwa, endapo mtu angeamua kutaka kuwa k**a yeye kwa sasa, angempa "u-Diamond" huo ndani ya masaa machache tu angefariki dunia kwa kushindwa kuhimili vita anazopigwa.
"Mmmmmh, oya jamani, kuwa Diamond kunataka moyo mmmh! Ndio maana kuna siku aliongea akasema, yaani wewe hapo ukisema uwe Diamond sasa hivi, unakufa k**a mzembe mzembe, unakufa!" amesema Mr. Mwanya.

 Mfanyabiashara maarufu wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo na mkewe, Lucy ‘Lulu’ Muteke, wanatarajiwa kuzikwa katika kaburi m...
02/10/2026


Mfanyabiashara maarufu wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo na mkewe, Lucy ‘Lulu’ Muteke, wanatarajiwa kuzikwa katika kaburi moja katika Kijiji cha Gandami, wilayani Chikomba, ambalo ndiko lilipo chimbuko la familia ya Chivayo.
Uamuzi wa kuwazika pamoja umefikiwa na familia ya Chivayo baada ya kupata ridhaa kutoka kwa ndugu wa upande wa Lucy, kwa mujibu wa msemaji wa familia, Herbert Chivayo.
Mazishi hayo yanatarajiwa kufanyika Gandami, ambako wanandoa hao walikuwa wakijenga makazi yao ya kifahari kabla ya kufariki katika ajali ya helikopta iliyotokea Jumatano jioni, Septemba 30, 2026, katika eneo la Marondera.
Herbert amesema uamuzi huo umefanyika kutokana na uhusiano wa karibu wa wanandoa hao, huku familia zote mbili zikikubaliana miili yao ipumzishwe pamoja.
Kwa sasa, wataalamu wa uchunguzi wanaendelea na taratibu za utambuzi wa miili kwa kutumia vipimo vya vinasaba (DNA) jijini Harare. Hatua hiyo imekuwa muhimu baada ya miili ya waliokuwamo kwenye helikopta kuungua vibaya katika ajali hiyo.
Ajali hiyo ilitokea Jumatano majira ya saa 11 jioni katika Shamba la Kudenga, Kijiji cha Marondera, baada ya helikopta waliyokuwa wakisafiria kuanguka na kushika moto.

Mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (RDC), Achillian, ameachia video ya nyimbo za injili (Gospel) yenye ...
02/10/2026

Mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (RDC), Achillian, ameachia video ya nyimbo za injili (Gospel) yenye maneno (lyric video) ya wimbo wake mpya unaoitwa , ambayo sasa ipo tayari YouTube! Jifunze neno kwa neno.
Huyu mwamba anastahili kupewa kiti cha heshima; yaani anajua mpaka basi!
Tukutane YouTube kupitia familia ya Dakika Media.
Mungu akubariki! 🙌🏾✝️

21/09/2026

🚨 “KITAMATA” YA FALLY IPUPA YAFUTWA KWENYE YOUTUBE NA KWENYE ALBAMU YAKE

 — Mwendesha baiskeli wa Kongo, Miguel Masaisai, amefariki dunia siku ya Ijumaa katika ajali ya barabarani huko Kabos, k...
19/09/2026

— Mwendesha baiskeli wa Kongo, Miguel Masaisai, amefariki dunia siku ya Ijumaa katika ajali ya barabarani huko Kabos, karibu na mpaka kati ya Congo-Brazzaville na Cameroun.

Baada ya baiskeli yake kuharibika, aliomba msaada kwa dereva wa teksi ili amsaidie kupata sehemu ya kutengeneza baiskeli hiyo. Gari hilo, ambalo lilikuwa limebeba watu wanne, baadaye lilihusika katika ajali iliyosababisha vifo.

Mwili wake umehifadhiwa katika mochwari ya Ouesso. Hata hivyo, familia yake iliyowasiliana huko Goma Jumamosi asubuhi bado haijathibitisha taarifa hiyo iliyotolewa na vyanzo vya eneo hilo.

14/09/2026

DUNIA SEASON 02 (Ep 50)

Adresse

Tanganyika
Lubumbashi

Téléphone

+243900490407

Site Web

Notifications

Soyez le premier à savoir et laissez-nous vous envoyer un courriel lorsque DAKIKA MEDIA publie des nouvelles et des promotions. Votre adresse e-mail ne sera pas utilisée à d'autres fins, et vous pouvez vous désabonner à tout moment.

Contacter L'entreprise

Envoyer un message à DAKIKA MEDIA:

Raccourcis

Partager