18/02/2025
DELCAT IDENGO
Alikuwa rasta aliyejichora tattoo ya Congo kwenye kuta za kifua chake. Kila kinywa chake kilipofunguka, msingi wa mahubiri yake ulijikita juu ya haki na Amani. Alikuwa mwanaharakati aliyeishi ndani ya falsafa na maono ya "Patrick Lumumba."
Alichukizwa kuona Congo DRC ina laana ya Rasilimali. Yaani utitiri wa madini katikati ya watu maskini. Hili lilimumiza sana.
Alikuwa mwanamuziki aliyeamini, kuimba mapenzi wakati Congo haina amani, ni kuionyesha dunia kiwango cha upumbavu unaopatikana ndani ya akili yako."
DELCAT IDENGO kila alipozama booth. Microphone ilitumika k**a nyenzo ya kuwasilisha hasira kali zinazoishi juu ya kifua chake.
Alikemea watawala dhulumati, na kufokea mabeberu wanaokwamisha amani ya Congo. Ujasiri wa kuimba kile ambacho jamii ina njaa ya kukisia. Ulimtengenezea jina, hadhi, na heshima kwenye mji wa Goma. Alikuwa ni mfalme wa kivu ya kaskazini."
Siku kadhaa zlizopita, aliingia booth akaachia wimbo wenye mahadhi ya rege akauita "bunduki." Wimbo ukikemea uwepo wa M-23 ndani ya Congo.
Baadhi ya mistari katika wimbo ule wenye mahadhi ya 'sweet rege' ni maneno haya.
Jambo wavamizi/
mmetufanya wakimbizi/
Najua mnatuogopa/
ila roho yenu ngumu imewaleta hapa/
Mtaishia hapa hapa/
Hiii ni nchi ya wa congo man/
Hapa ni macho kwa macho/
Hakuna kukimbia tena."
"DELCAT IDENGO." Hakujua anawatisha binadamu walioenda "Goma" wakiwa hai kimwili lakini kifkra walishajifia. Hakuna kitu hatari k**a kupambana na mwanadamu ambaye ni mfu wa fikra.
"Kuwatungia wimbo M-23. Ni k**a kukilazimisha kifo kije kazini wakati kimechukua likizo ya kuua."
Alfajiri ya leo goma imetikisika. Rastafarian, mwanamuziki, aliyeamini kwenye harakati za ukombozi wa Congo. Mdomo wa bunduki umehitimisha safari ya uwepo wake chini ya jua kikatili.
Ameuawa baada ya kupigwa risasi katika jiji la Goma na watu inaosadikika ni waasi wa M-23.
"DELCAT IDENGO" alitamani kuona siku moja Congo ina amani ya kudumu. Watu wana gonga cheer's huku wakitafuna kuku, wanapotazama kiuno cha "Fally Ipupa." Bahati mbaya amelala mauti, akiwa hajashuhudia ndoto aliyoitamani, ikigeuka kuwa simulizi ya kweli."
IMEANDIKWA NA Mufaridji Ngarambi Fei @