22/06/2025
Baada Ya kumaliza ziara yake nchini Uingereza, SIMBA 🦁 , anarudi tena jijini London kesho, tarehe 23 Juni 2025, katika show kubwa ya itakayofanyika maeneo ya King’s Cross 🇬🇧.
Diamond Anaungana Na Mastaa Wengine Wakubwa Duniani Waliowahi Kutumbuiza Kwenye Onesho Hili La Kimataifa La DjAgOnline K**a: Doja Cat 🇺🇸, Ed Sheeran 🇬🇧, Will Smith 🇺🇸, Ciara 🇺🇸, Rita Ora 🇺🇸, Burna Boy 🇳🇬, Wizkid 🇳🇬, Major Lazor, Mr Flavour 🇳🇬 Na Wengine Kibao.
Hii Inaonesha Uhitaji Umekuwa Mkubwa Zaidi (High Demand) Kwa Diamond Kuendelea Kufanya Show Nchini Uingereza Baada Ya Kuacha Historia Ukumbi Wa Royal Albert Hall Na Tamasha La Nchini Marekani Hivi Karibuni.
Hivyo Hii Ni Hatua Nyingine Kubwa Kwa Diamond, Kwani Kushiriki Katika Onesho Hili Kunamuweka rasmi kwenye ligi ya mastaa wa dunia, na kuthibitisha kuwa muziki wa Afrika Mashariki una nafasi kubwa kwenye jukwaa la dunia.