ELIMU NI NURU Informations de contact, plan et itinéraire, formulaire de contact, heures d'ouverture, services, évaluations, photos, vidéos et annonces de ELIMU NI NURU, Site web d’actualités, Uvira.

06/05/2025

اَلسَلامُ عَلَيْكُم وَرَحْمَةُ اَللهِ وَبَرَكاتُهُ‎

Alhamdulillah, Natumai muwazima na Allah ametuhuisha tena.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema mwingi wa ukarimu.

*40. Na wa kwanza wao watasema kwa wengine wao: Basi ninyi pia hamkuwa na fadhili kuliko sisi! Kwa hiyo onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyachuma.*

[7. SURA AL-A'RAAF:40]

Yaa Rabbi! Utuongoze njia iliyonyooka, njia ya wale Uliowaneemesha; sio ya (wale) waliokasirikiwa, wala ya (wale) waliopotea.

*Ameen!!!*

14/04/2025

اَلسَلامُ عَلَيْكُم وَرَحْمَةُ اَللهِ وَبَرَكاتُهُ‎

Alhamdulillah, Natumai muwazima na Allah ametuhuisha tena.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema mwingi wa ukarimu.

*11. Na bila shaka Tumewakalisheni katika ardhi na Tumewawekeeni humo vitu vya maisha. Ni shukrani ndogo tu mnazotoa.*

[7. SURA AL-A'RAAF:11]

Yaa Rabbi! Utuongoze njia iliyonyooka, njia ya wale Uliowaneemesha; sio ya (wale) waliokasirikiwa, wala ya (wale) waliopotea.

*Ameen!!!*

﷽*Maana sahihi ya kuimba kwa Qur-aan**Swali:* Kuna mtu anaimba Qur-aan k**a mtindo wa muziki. Je, anakufuru kwa kitendo ...
07/02/2025



*Maana sahihi ya kuimba kwa Qur-aan*

*Swali:* Kuna mtu anaimba Qur-aan k**a mtindo wa muziki. Je, anakufuru kwa kitendo hicho?

*Jibu:* Hili halijuzu. Lakini huenda amefahamu makosa:

“Si katika sisi yule ambaye haimbi kwa Qur-aan.”

Maana yake ni kuboresha sauti. Haina maana kwamba anaiimba kwa tungo za mashairi na nyimbo, hapana. Ni kosa. Azinduliwe ya kwamba ni kosa. Hakufuru kwa kitendo hicho. Lakini afundishwe ya kwamba jambo hilo ni kinyume na Sunnah na ni kosa na kwamba kuimba kwa Qur-aan kunamaanisha kuifanya sauti na kisomo kuwa kizuri.

*Muhusika:* Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
*Tarjama:* Firqatunnajia.com
*Marejeo:* https://binbaz.org.sa/fatwas/25140/ما-حكم-من-يغني-بالقران-على-لحن-الموسيقا
*Imechapishwa:* 06/02/2025"
https://firqatunnajia.com/maana-sahihi-ya-kuimba-kwa-qur-aan/ #

⤵️
https://t.me/joinchat/R0tP2s5sF0G3Q8N6

Uislamu kwa ufahamu wa Salaf

﷽*Ni wajibu kuwatahadharisha ndugu zetu na sikukuu za makafiri*Ni wajibu kutukana sikukuu za makafiri, kutahadharisha ju...
09/01/2025



*Ni wajibu kuwatahadharisha ndugu zetu na sikukuu za makafiri*

Ni wajibu kutukana sikukuu za makafiri, kutahadharisha juu yazo, tusiziridhie na tuwafunze ndugu zetu wajinga wapumbavu ya kwamba haijuzu kushirikiana na makafiri katika sikukuu zao. Kuridhia kufuru kunakhofiwa kumwingiza yule mwenye kufanya hivo ndani ya kufuru. Je, hivi kweli wewe unaridhia kufanywe sherehe za kufuru na wewe ukashirikiana nazo? Hakuna muislamu yeyote anayeridhia hili. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah), ambaye ni mwanafunzi kigogo wa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, amesema:

“Yule mwenye kushirikiana na watu hawa katika sikukuu zao, akawapongeza kwazo, ikiwa hakufanya kufuru, basi angalau kwa uchache amefanya tendo la haramu. Hili halina shaka yoyote.”

Amesema kweli (Rahimahu Allaah). Kwa ajili hiyo ni wajibu kwetu kuwatahadharisha ndugu zetu waislamu kushirikiana na makafiri katika sikukuu zao. Kwa sababu kushirikiana nao katika sikukuu zao, kuwapongeza kwazo, kwa mfano kusema “Sikukuu njem!”, “Allaah akupongezeni kwa sikukuu!” na mfano wa maneno k**a hayo, hakuna shaka yoyote juu ya kwamba ni kuridhia desturi za kufuru – tunaomba kinga kwa Allaah.

*Mhusika:* Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
*Mfasiri:* Firqatunnajia.com
*Marejeo:* Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/356-357)
*Imechapishwa:*
08/01/2025

⤵️
https://t.me/joinchat/R0tP2s5sF0G3Q8N6

Uislamu kwa ufahamu wa Salaf

29/12/2024

اَلسَلامُ عَلَيْكُم وَرَحْمَةُ اَللهِ وَبَرَكاتُهُ‎

Alhamdulillah, Natumai muwazima na Allah ametuhuisha tena.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema mwingi wa ukarimu.

*41. Sema: Niambieni! k**a ikiwafikieni adhabu ya Allah au iwafikieni saa ile, je, mtamwita yeyote asiyekuwa Allah ikiwa ninyi ni wakweli?.*

*42. Bali Yeye ndiye mtamwita, naye Atawaondoleeni mnayomwitia, Akipenda, na mtayasahau mnayoshirikisha.*

[6. SURA AL-AN'AAM:41-42]

Yaa Rabbi! Utuongoze njia iliyonyooka, njia ya wale Uliowaneemesha; sio ya (wale) waliokasirikiwa, wala ya (wale) waliopotea.

*Ameen!!!*

20/12/2024

اَلسَلامُ عَلَيْكُم وَرَحْمَةُ اَللهِ وَبَرَكاتُهُ‎

Alhamdulillah, Natumai muwazima na Allah ametuhuisha tena.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema mwingi wa ukarimu.

*28. Na ungeona watakaposimamishwa juu ya Moto, ndipo watasema; Laiti tungerudishwa na kutozikadhibisha Aya za Mola wetu na kuwa miongoni mwa waaminio.*

[6. SURA AL-AN'AAM:28]

Yaa Rabbi! Utuongoze njia iliyonyooka, njia ya wale Uliowaneemesha; sio ya (wale) waliokasirikiwa, wala ya (wale) waliopotea.

*Ameen!!!*

﷽*Ni batili, batili na zaidi**Swali:* Je, swalah kwa kuelekea makaburi ni batili?*Jibu:* Ndio, batili, batili na zaidi y...
16/12/2024



*Ni batili, batili na zaidi*

*Swali:* Je, swalah kwa kuelekea makaburi ni batili?

*Jibu:* Ndio, batili, batili na zaidi ya hivo.

*Swali:* Vipi kuhusu kuswali kando ya njia?

*Jibu:* Kumepokelewa Hadiyth hii ambayo ni dhaifu. Bora ni kuepuka kufanya hivo. Kumepokelewa katika baadhi ya mapokezi mengine kuepuka… kando ya njia, kwa sababu ni kimbilo la wanyama waharibifu. Bora ni kuepuka kukaa na kuswali, kwa sababu ni jambo la khatari.

*Mhusika:* Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
*Mfasiri:* Firqatunnajia.com
*Marejeo:* *https:*//binbaz.org.sa/fatwas/24824/حكم-الصلاة-الى-القبور-وفي-قارعة-الطريق
*Imechapishwa:* 15/12/2024
https://firqatunnajia.com/ni-batili-batili-na-zaidi/

⤵️https://t.me/joinchat/R0tP2s5sF0G3Q8N6

Uislamu kwa ufahamu wa Salaf

24/11/2024

JINSI ZINAA INAVYO VURUGA NDOA ZA WATU.

Wote ni wazinifu lakini wazinifu hawa ni hatari sana.

(1) Ikiwa mke kafanya zinaa na akapata ujauzito na mtoto akahesabika wa ndani ya ndoa na akapewa haki zote na baba lakini siku ikibainika ndoa hiyo haina amani tena na mtoto huyo hanogi tena machoni hata k**a ni mtoto wa kitanda au k**a wasemavyo Waswahili Kitanda hakizai haramu.

(2) Ikiwa mwanaume kazaa nje ya ndoa akiwa ndani ya ndoa na akamchukua mtoto ili alelewe na mkewe wa ndani ya ndoa nalo linavunja amani kabisa na mara nyingi wanawake huwa ni sababu tosha ya kulipiza kisasi kwa sababu akijiuliza "Kwani mtoto huyu kampataje?" Maumivu yake hayaelezeki.

(3) Kuna kuoana halafu wanandoa mmoja wao au wote walizaa nje ya ndoa kabla ya kuoana na watoto hao wanaishi nao pamoja halafu kila mmoja iwe mzazi mwenziye wa zinaa anakuja kwako kumtembelea mtoto wake napo panakera sana.

(4) Kuna mtindo wa kumdhania mtu ni shemeji yako iwe ni rafiki wa mwenza wako au ndugu wa mwenza wako au kuna wanao jitangaza "Huyu nimesoma nae" Kumbe sivyo unazungukwa siku ikijulikana tayari mambo yameharibika hapanogi tena hapo.

(5) Kuna wengine kichaka chao basi huyu ni mtumishi mwenzangu au bosi wangu au mfanya biashara mwenzangu na mpaka nyumbani unamkaribisha kumbe ni majanga siku ukigundua ni hatari hata mate shingoni hayapiti.

(6) Kuna wengine utaambiwa huyu ni daktari wangu na kweli ni daktari ila kuna mambo yanaendelea siku ukijua na jinsi unavyo mnyenyekea na kumthamini maumivu yake hayaelezeki.

(7) Kuna wengine wanatumia mgongo wa ujirani ikawa kusaidiwa ni wepesi kabisa hata ukisafiri utaambiwa "Tilulikwama kweli bila jirani yetu tungeumbuka nawe ukamtolea shukrani na kumuombea dua kumbe ni fisadi mkubwa siku ikigundua utatamani kuhama mtaa.

(8) Kuna hawa tunao waamini kutusomeshea vijana wetu tukawafanya watoto wetu kabisa kumbe wanatugeuka nasi tumewaamini wanaingia majumbani mwetu bila kizuizi siku ukibaini utatamani kumnyonga mtu.

(9) Kuna hawa wasichana wa kazi akianza

﷽*Thawabu mara mbili**Swali:* Kujitolea matumizi kuwapa jamaa wa karibu ni kuunga kizazi?*Jibu:* Ni swadaqah na kuunga k...
29/09/2024



*Thawabu mara mbili*

*Swali:* Kujitolea matumizi kuwapa jamaa wa karibu ni kuunga kizazi?

*Jibu:* Ni swadaqah na kuunga kizazi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Swadaqah kumpa masikini ni swadaqah na kuwapa jamaa inakuwa [thawabu] mara mbili; swadaqah na kuunga kizazi.”

*Mhusika:* Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
*Mfasiri:* Firqatunnajia.com
*Marejeo:* https://binbaz.org.sa/fatwas/24324/ما-فضل-الانفاق-على-الاقارب
*Imechapishwa:* 28/09/2024
https://firqatunnajia.com/thawabu-mara-mbili/ #

⤵️
https://t.me/joinchat/R0tP2s5sF0G3Q8N6

Uislamu kwa ufahamu wa Salaf

﷽*Dhambi kwa asiyetahiri?**Swali:* Asiyetahiri anapata dhambi?*Jibu:* Wanazuoni wengi wanaona kuwa inapendeza. Ahmad (Ra...
24/09/2024



*Dhambi kwa asiyetahiri?*

*Swali:* Asiyetahiri anapata dhambi?

*Jibu:* Wanazuoni wengi wanaona kuwa inapendeza. Ahmad (Rahimahu Allaah), Ibn ´Abbaas na kikosi cha wanazuoni wengine wanaona kuwa ni wajibu.

*Swali:* Asiyetahiri anapata dhambi?

*Jibu:* Wale ambao wanaona kuwa ni wajibu anapata dhambi. Wale ambao wanaona kuwa inapendeza hapati dhambi. Hata hivyo mtu anatakiwa kufanya hivo, k**a alivosema Ibn ´Abbaas na akatilia mkazo wa hilo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaambia baadhi ya Maswahabah waliposilimu:

”Ondosha nywele za ukafiri na tahiri!”

Hata hivyo katika cheni ya upokezi kuna unyonge.

*Mhusika:* Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
*Mfasiri:* Firqatunnajia.com
*Marejeo:* https://binbaz.org.sa/fatwas/24282/هل-ياثم-من-لم-يختتن
*Imechapishwa:* 23/09/2024
" https://firqatunnajia.com/dhambi-kwa-asiyetahiri/ #

⤵️
https://t.me/joinchat/R0tP2s5sF0G3Q8N6

Uislamu kwa ufahamu wa Salaf

15/09/2024

*BAADHI YA MAMBO MUHIMU AMBAYO MUISLAMU ANAPASWA KUYAJUA*

*Nguzo za Uislamu*
*1. Shahada*
*2. Sala*
*3. Zaka*
*4. Saumu (Funga)*
*5. Hija*

*Nguzo za Imani*
*1. Kumuamini Allah*
*2. Kuamini Malaika*
*3. Kuamini Vitabu*
*4. Kuamini Mitume*
*5. Kuamini Siku ya Mwisho*
*6. Kuamini Qadari*

*Vitabu vinne vya Allah*
*1. Taurati*
*2. Zaburi*
*3. Injili*
*4. Quran*

*Miezi ya Kiislamu*
*1. Muharram*
*2. Safar*
*3. Rabi'ul Awwal*
*4. Rabi'ul Akhir*
*5. Jumadal Uula*
*6. Jumadal Akhirah*
*7. Rajab*
*8. Sha'aban*
*9. Ramadan*
*10. Shawwal*
*11. Dhul-Qa'adah*
*12. Dhul-Hijjah*

*Miezi minne mitukufu*
*1. Dhul-Qa'adah (mwezi wa 11)*
*2. Dhul-Hijjah (mwezi wa 12)*
*3. Muharram (mwezi wa 1)*
*4. Rajab (mwezi wa 7)*

*Misikiti mitatu mitakatifu*
*1. Masjid Haraam (Makkah)*
*2. Masjid Nabawi (Madina)*
*3. Masjid Aqsa (Quds, Palestina)*

*Sala Tano za Kila Siku*
*1. Fajr (subhi) - Rakaa 2*
*2. Dhuhr - Rakaa 4*
*3. Asr - Rakaa 4*
*4. Magharibi - Rakaa 3*
*5. Ishaa - Rakaa 4*

*Majina ya Mitume waliotajwa katika Quran*
*1. Adam*
*2. Idris*
*3. Nuh*
*4. Hud*
*5. Salih*
*6. Ibrahim*
*7. Lut*
*8. Ismail*
*9. Is-haq*
*10. Yaqub*
*11. Yusuf*
*12. Ayyub*
*13. Shu'aib*
*14. Musa*
*15. Harun*
*16. Dhul-Kifl*
*17. Dawud*
*18. Suleiman*
*19. Ilyas*
*20. Alyasa'*
*21. Yunus*
*22. Zakaria*
*23. Yahya*
*24. Isa*
*25. Muhammad*

*Mitume watano Ulul-'azm*
*1. Nuh*
*2. Ibrahim*
*3. Musa*
*4. Isa*
*5. Muhammad*

*Maswahaba kumi waliobashiriwa Pepo*
*1. Abubakar Swiddiq*
*2. Umar bin Khattab*
*3. Uthman bin 'Affan*
*4. Ali bin Abi Talib*
*5. Talha bin Ubaidillah*
*6. Zubeir bin Awwam*
*7. Abdul-Rahman bin* *Awf*
*8. Sa'ad bin Abi* *Waqqas*
*9. Said bin Zaid*
*10. Abu 'Ubaidah bin* *Jarrah*

*Makhalifa wanne waongofu*
*1. Abubakar Swiddiq*
*2. Umar bin Khattab*
*3. Uthman bin 'Affan*
*4. Ali bin Abi Talib*

*Maimamu wanne wa Fiqhi*
*1. Abu Hanifa Nu'man* *bin Thabit*
*2. Malik bin Anas*
*3. Muhammad bin Idris *Al-Shafi*
*4. Ahmad bin Hanbal*

*Maimamu sita wa Hadithi*

﷽*Fanya matendo kwa kiasi na uwezo wako*Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:*142* – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´an...
11/09/2024



*Fanya matendo kwa kiasi na uwezo wako*

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

*142* – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kuwa:

*أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم دخل عَلَيْهَا وعِندها امرأةٌ، قَالَ: (مَنْ هذِهِ؟) قَالَتْ: هذِهِ فُلاَنَةٌ تَذْكُرُ مِنْ صَلاتِهَا. قَالَ: (مهْ، عَلَيْكُمْ بِمَا تُطِيقُونَ، فَواللهِ لا يَمَلُّ اللهُ حَتَّى تَمَلُّوا، وكَانَ أَحَبُّ الدِّينِ إِلَيْهِ مَا دَاوَمَ صَاحِبُهُ عَلَيهِ) مُتَّفَقٌ عَلَيه*

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia kwake na yuko pamoja na mwanamke [mwenzake]. Akamuuliza: “Nani huyu?” Akamwambia: “Huyu ni fulani. Akataja kuhusu swalah zake [anavoswali sana].” Akamwambia: “Koma!” Fanyeni mnachoweza. Ninaapa kwa Allaah kuwa Allaah hachoki mpaka nyinyi mchoke. Kinachopendeza zaidi Kwake ni kile ambacho mwenye nacho anadumu juu yake.”[1]

Maana ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha mwanamke huyu akome na kufanya matendo mengi ambayo yanaweza kuja kumkuia mazito. Matendo ambayo yanaweza kumkuia magumu na akashindwa huko mbele na hivyo asidumu kwayo. Kisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaamrisha tufanye matendo kwa kiasi na tunavyoweza:

“Fanyeni mnachoweza.”

Bi maana msizikalifishe nafsi zenu. Mtu akiikalifisha nafsi yake na kupambana nayo huchoka na kupunguza na halafu hatimaye anaacha.

*[1] al-Bukhaariy na Muslim*

*Mhusika:* Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
*Mfasiri:* Firqatunnajia.com
*Marejeo:* Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/212-213)
*Imechapishwa:* 10/09/2024"
https://firqatunnajia.com/fanya-matendo-kwa-kiasi-na-uwezo-wako/ #

⤵️
https://t.me/joinchat/R0tP2s5sF0G3Q8N6

Uislamu kwa ufahamu wa Salaf

Adresse

Uvira

Site Web

Notifications

Soyez le premier à savoir et laissez-nous vous envoyer un courriel lorsque ELIMU NI NURU publie des nouvelles et des promotions. Votre adresse e-mail ne sera pas utilisée à d'autres fins, et vous pouvez vous désabonner à tout moment.

Partager