18/03/2025
Kiongozi wa Al-Hikma Foundation, Sheikh Nurdeen Kishk, amesema kuwa taasisi hiyo itafungisha ndoa 200 mwaka huu katika juhudi zake za kusaidia vijana kuingia katika ndoa.
Akizungumza katika Mashindano ya 25 ya Qur’an Tukufu yanayofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Sheikh Kishk amesema kati ya ndoa hizo, 100 zitafungwa Tanzania na 100 nyingine Burundi.
Ameeleza kuwa Al-Hikma Foundation itagharamia mahari, majoho, vilemba, ukumbi pamoja na chakula kwa wanandoa hao siku ya harusi k**a ambavyo imefanya siku za nyuma.
Mwaka jana, taasisi hiyo ilifanikisha ndoa 100 nchini Tanzania.
'anCompetition
✍️ .lims
📸