06/06/2026
Je, wajua siri iliyopo nyuma ya makumbusho makubwa zaidi duniani? ποΈβ¨
Kutoka moyoni mwa Cairo, Misri inafungua milango ya Makumbusho Makuu ya Misri (GEM), kito cha kipekee kinachounganisha historia ya kale na teknolojia ya kisasa.
Hii si historia ya Misri pekee, bali ni Urithi wa Pamoja wa bara zima la Afrika! Tangu zamani za kale, Mto Nile umekuwa shariani ya heri na mawasiliano, ukisafirisha utamaduni na biashara kutoka vyanzo vyake huko Malkia wa Maziwa (zamani Lake Victoria) hadi Mediterania. Safari za kihistoria kuelekea nchi ya "Punt" (Afrika Mashariki) ni thibitisho tosha la undugu wetu wa damu na utamaduni.
Ndani ya makumbusho haya, hazina kamili ya Mfalme Tutankhamun na athari za kale za Kiafrika zinakusubiri kushuhudia ukuu wa mababu zetu.
Karibuni Misri β Nyumbani kwa Historia, Amani na Maendeleo! πͺπ¬π€π
π¬ Swali la leo: Je, ni athari gani ya kale ya Misri unayotamani zaidi kuiona kwa macho yako katika makumbusho haya mapya? Tuandikie kwenye maoni!