20/10/2025
Binadamu wanachagua kudharau vizuri na kufanya au kuwaaminisha wengine kuwa havipo. Usifiche ulichojaaliwa kwa faida ya kuonekana na wanaopenda pamoja na watakao heshimu neema yako, ubunifu au zawadi kutoka kwa aliyekuumba. Ukiondoka duniani maskini kwa kutegemea vile ulivyoaminishwa kuwa ndo utajiri kesho utajutia kwanini hukutumia neema, ujuzi au ubunifu wako sababu tu ulikatishwa tamaa na watu weye husda au wasiokuwa na taaluma ya kuelewa tunu yako na wale ambao uliwaamini kuwa bila wao kukushauri wewe hufanyi lolote. Ukiendelea kuishi hivyo, utapitwa kimaendeleo, kimanufaa, kiubora na watu ambao wanafanya chini ya kiwango au daraja aliyokuinua nayo Mungu na utaona wanafanikiwa we unakaa kinyonge. Kisha hao hao ambao waliokuaminisha cha kwako ni cha kawaida sana na kukukatisha tamaa, wakisifie cha mwingine ambacho sio bora k**a chako mradi tu kukufanya uwe muoga wa kutojiamini na kuthubutu kufanya. Acha dunia ione ubunifu wako na ubora na heri au tunu aliyokupa Mungu kwa ubunifu au taaluma binafsi sababu kweli mficha uchi hazai.