29/07/2025
KISA CHA JUHA NA MFALME
Siku moja Juha alikuwa ameketi katika baraza la mfalme. Mfalme alitaka kumdhalilisha juha na kuwachekesha waliokuwepo, hivyo Mfalme akamwambia Juha kwa kejeli:
—“Je, unaweza kumfundisha punda wangu kusoma na kuandika?”
Kwa majivuno na ujasiri, Juha alijibu kwa kujiamini:
— “Ndiyo, naweza… lakini kwa masharti kwamba unipe muda wa miaka kumi nikiwa namfundisha ndani ya miaka hiyo mpaka ajue kusoma na kuandika”
Mfalme alikubali sharti hilo, akaamuru Juha alipwe mshahara kila mwezi kwa muda wote huo.
Baada ya kutoka kwenye kasri, rafiki yake mmoja alimkimbilia juha na kumwambia kwa mshangao:
— “Ewe Juha! Je, umechanganyikiwa? Ulikubali vipi jambo lisilowezekana kabisa?!”
Juha akatabasamu kwa utulivu na kusema:
— “Rafiki yangu tulia usipanic mimi nina akili nyingi kuliko unavyo dhania, iko hivi, katika kipindi cha miaka kumi: ama mimi nitakuwa nimekufa, au mfalme atakuwa amekufa, au punda atakuwa amekufa… sasa ni nani mjinga kati yangu na Mfalme?”😃
Rafiki akabaki akicheka kwa furaha alipojua kumbe Juha hajakurupuka bali alitumia akili nyingi sana.
Mafunzo katika kisa hiki ni kwamba:
1.Subira na Busara Ni Silaha ya Mwerevu:
Juha hakujibu kwa hasira wala kukataa kwa hofu, bali alitumia busara na kutoa jibu la kijasiri lenye masharti ya muda mrefu. Alielewa kuwa muda unaweza kubadilisha hali yoyote.
2.Matatizo Makubwa Hukabiliwa kwa Utulivu: Badala ya kuogopa ombi la mfalme lililoonekana kuwa gumu au lisilowezekana, Juha alilichukulia kwa utulivu na akaligeuza kuwa fursa (kupokea mshahara wa miaka kumi).
3.Mambo Magumu Hayahitaji Kukimbiliwa, Bali Kucheleweshewa:
Juha alijua kuwa hakuna anayeweza kudhibiti maisha au kifo, hivyo akaweka muda mrefu kwa jambo lisilowezekana, akitegemea hali itabadilika kabla ya kufika mwisho wake.
4.Kufikiri Mbali (Long-Term Thinking):
Mwenye akili hufikiria mbali kabla ya kuchukua hatua. Juha alitumia hekima kutathmini hatima ya jambo hilo kwa miaka kumi ijayo badala ya kuchukulia kwa haraka.
5.Watu We