25/07/2023
💏MY BABY 💏
💔 PART ONE 💔
MARA ya kwanza ambapo Jared alionyesha kumtamani Victoria marafiki zake walimuonya."Huyo dem ni psycho bro! Anakuwanga kisirani!",walijaribu kumuonya lakini aliwapea jibu simple,"Watu ni kuelewana 😊".Hata marafiki zake walipoona kuwa ashapenda waliachana na yeye huku wakiamini ataachwa mataani.
Jared naye hakuwai kubali kufishwa moyo.Hivo basi alimfuata yule Victoria,hata ingawa alisumbuka sana,mpaka dakika ya mwisho Victoria akamkubali.Hakuelewa k**a ilikuwa kupofushwa na mapenzi ama ni marafiki zake walikuwa wakimdamganya ile Jared hakuona kisirani yoyote kwake Victoria.Alijikaza akampemda Vicky kwa dhati na hata Vicky akaonekana kumpenda pia.
Mapenzi yao yalipopamba moto walikubaliana wakakomboa nyumba kule Donholm,nyumba simple tu kwa ghorofa.Pesa hazikuwa stress ju Jared alikuwa job.Shida ilianzia pale ambapo Vicky alipata mimba🤰.Alikuwa tu kisirani karibu kila saa,ila Jared akajiambia labda akijifungua atatulia.So kwa ule muda ambapo Vicky alikuwa mjamzito Jared alijikaza kabisa asije akamkasirisha.
Basi miezi tisa zikatimia, Vicky akapelekwa hospitalini na kule akajifungua msichana mrembo sana.Hapo na hapo mapenzi yake Jared kwake Vicky yakaongezeka mara dufu.Alimtunza Vicky k**a malkia,ama k**a yai ambalo hangetaka lianguke na kuvunjika.Chochote Vicky angeitisha alipewa.Ikaendelea hivo mpaka alipomaliza kunyonyesha 🤱.
Siku moja Jared alifika nyumbani usiku ikielekea saa tatu.Alimpata Vicky ameketi pale sebuleni akiwa amenuna 😐. Alipojaribu kumuongelesha msichana aliamka tu na kwenda kulala.Siku iliyofuata, vile vile.Siku baada yake,vile vile.Aiii, Jared akaona ipo shida.So baada ya wiki moja aliamua lazima ajue chanzo cha kununiwa...
JARED:Baby?
VICTORIA:(Hakumuangalia wala kumjibu.Aliamka tu na kuanza kuelekea kwa chumba cha kulala.Jared naye alikimbia na kusimama mbele yake kisha akamshika uso)
JARED: Baby,ni nini mbaya?Mbona hivi siku hizi?
VICTORIA:(Bila kumtazama)Mbona nini 😏?
JARED:Hivi...Ona hata hutaki kuniangalia.N