24/06/2025
🌹Nilimpenda tangu siku ya kwanza nilipomwona. Alikuwa na mdomo wa upole na macho ya faraja. Alinijua nikiwa bado naishi kwa dada yangu. Nikiwa bado najitafuta. Alinichukua. Akanivisha nguo. Akanifundisha maisha. Akanipa jina. Nilijua ndiye mume wangu wa milele. Nilijua nimepata, basi.
Tulifunga ndoa ya kimya kimya. Ndani ya nyumba ya kupanga, lakini yenye upendo mwingi.
Baada ya miezi sita ya ndoa, alinipa wazo “Ningependa ukaonane na daktari wangu wa afya ya uzazi, ili tujipange mke wangu”
Nilikubali kwa upofu wa mapenzi. Nilienda naye hospitali moja kubwa. Alizungumza na daktari kwa lugha ya kimombo mie sikujua kizungu. Mimi nilikaa kimya. Niliambiwa ni sindano za kupanga uzazi ili tuanze maisha vizuri. Nilisema “sawa.” Nilipewa dozi ya sindano na vidonge. Niliamini.
Miaka miwili ikapita. Sina mtoto. Kila nikimuuliza, anasema bado mapema. Anasema tufurahie kwanza maisha yetu ya mwanzo. Nikaanza kuwa na wasiwasi. Watu wakaanza kuniuliza, “Mlikuwa harusi mwaka gani? Mbona kimya?” Nikaanza kuona wivu moyoni. Marafiki walizaa. Madada zangu walizaa. Mimi nilikuwa tu kimya.
Alipoona nasumbuka, akanambia, “Usijali mpenzi wangu, tukitaka mtoto tutazaa.” Nikamwamini tena. Kwa mara ya pili.
Lakini nikaanza kuhisi mwili wangu hauna mzunguko wa kawaida. Nikajipeleka hospitali ya kawaida bila yeye kujua. Nilipopewa majibu ya vipimo, daktari aliniangalia macho kwa huruma.
Akanambia“Ulisema lini uliwahi kufanyiwa operesheni ya uzazi?” Nikastuka. Nikauliza, “Operesheni gani?” Daktari akashusha macho.
“Uliwahi kufungwa mirija ya uzazi. Umewekewa kifaa cha kuzuia mimba cha maisha bila taarifa?”
Nilihisi kufa. Nilitetemeka. Nilikuwa na hasira, huzuni, na mshangao kwa wakati mmoja. Nilimwambia daktari “Sijawahi kufanyiwa kitu chochote. Mume wangu tu ndio alinituma kwa daktari wake.”
Nilitoka pale kliniki nikiwa na maumivu ya aina nyingine. Si ya mwili. Ya roho. Nilimsubiri arudi usiku. Nikamwonyesha ripoti. Nikamuuliza moja kwa moja “Kwa nini ulifanya hivi bila ridhaa yangu”