22/10/2025
Muungano wa Upinzani (United Opposition) umekataa kauli na msamaha wa Gavana wa Nyeri, Mutahi Kahiga, kufuatia matamshi yake kuhusu kifo cha Waziri Mkuu wa zamani, Raila Amolo Odinga.
Msemaji wa upinzani, Dkt. Mukhisa Kituyi, amesema kauli za aina hiyo zinahatarisha umoja wa kitaifa na kusisitiza kuwa viongozi wanapaswa kudumisha viwango vya juu vya maadili katika usemi na mienendo yao.