
10/07/2025
*🌲SOMO KUHUSU MARAFIKI 🙏🏽*
SIO KILA UNAYEMWITA RAFIKI NI RAFIKI WA KWELI.
WENGINE NI K**A VIVULI WANAONEKANA TU KUKIWA NA MWANGA.
WAKATI WA GIZA, HAWAPO!
Katika safari ya maisha, utagundua kwamba baadhi ya waliokuwa karibu yako hawakuwa marafiki, bali walikuwepo kwa sababu ya faida, si kwa sababu ya upendo wa kweli.
*RAFIKI WA KWELI*
- Hukusimamia hata ukianguka.
- Hukukosoa faraghani na kukusifia hadharani.
- Hushiriki mafanikio yako bila wivu na kushikamana nawe kwenye magumu bila kujivika sifa.
*MARAFIKI WANAFAKI*
- Hukusaliti kimya kimya.
- Hukutabasamia usoni na kukuchimba nyuma.
- Wanafurahia unaposhindwa, lakini wanakaa kimya unapofaulu.
*UJUMBE:*
Usihuzunike kwa kuwa umewapoteza watu waliokuwa na sura ya urafiki lakini hawakuwa na moyo wa urafiki.
Ni heri kuwa na marafiki wawili wa kweli kuliko kundi la wanafiki wanaovaa .....✍️✍️✍️