
11/08/2025
CAF imesitisha mauzo ya tiketi kwa mechi zote zijazo zitakazochezwa katika Uga wa Kasarani, ikiwemo mchezo wa Jumapili ijayo kati ya Kenya na Zambia, kufuatia ukiukaji mkubwa wa taratibu za usalama na ulinzi uliojitokeza wakati wa mchezo wa Harambee Stars dhidi ya Morocco.
Matukio hayo, kabla na wakati wa mechi, yalihusisha kuvunjwa kwa lango, mashabiki kuingia bila tiketi, idadi ya watu kuzidi uwezo wa uwanja, kuvamiwa kwa kituo cha wanahabari, na matumizi ya gesi ya machozi.
Kamati za nidhamu na usalama za CAF zinachunguza suala hili na zitaamua hatua zinazofuata.