RAHAI

RAHAI WELCOME TO RAHAI ITS A MEDIA PLATFORM WICH PROVIDES YOU WITH LOCAL AND INTERNATIONAL NEWS. Reach us on +254 793 772 989

Timu ya wanawake ya Kenya Harambee Starlets imefuzu kushiriki fainali za kombe la kimataifa la wanawake Afrika WAFCON 20...
28/10/2025

Timu ya wanawake ya Kenya Harambee Starlets imefuzu kushiriki fainali za kombe la kimataifa la wanawake Afrika WAFCON 2026 kufuatia ushindi wa bao pekee la DOGO na kuifuta Gambia katika michuano hiyo.

Kufuatia ushindi huo Starlets wanafunga kibindoni shilingi milioni 1 kila mchezaji ambayo ni ahadi ya Rais wa Kenya William Samoei Ruto kuwapatia motisha.

Rais wa Kenya William Samoei Ruto anasema, awali ili kupata kitambulisho cha kitaifa ilihitajika uwe na shilingi 300 ila...
28/10/2025

Rais wa Kenya William Samoei Ruto anasema, awali ili kupata kitambulisho cha kitaifa ilihitajika uwe na shilingi 300 ila kuanzia sasa ni bure, lakini pia kubadilisha kitambulisho kilichopotea ilikua garama ya shilingi 1000 kuanzia leo serekali imeondosha malipo yote hayo.

Kiongozi Wa Vijana na seneta wa Siaya Hon. Dr. Oburu Oginga akaunti yake ya mtandao wa Facebook imedukuliwa.Oburu ambaye...
27/10/2025

Kiongozi Wa Vijana na seneta wa Siaya Hon. Dr. Oburu Oginga akaunti yake ya mtandao wa Facebook imedukuliwa.

Oburu ambaye pia ni kiongozi wa chama cha ODM aliyechukua nafasi hiyo baada ya kufariki kaka yake Raila Odinga, akaunti yake imefutwa kila kitu na kubadilishwa picha.

Kwa mara ya kwanza Nairobi United inatinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika CAFCC kwa ushindi wa penalty 7...
27/10/2025

Kwa mara ya kwanza Nairobi United inatinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika CAFCC kwa ushindi wa penalty 7-6 dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia.

Mara ya mwisho timu kutoka Kenya kufika hatua hiyo 2018 Gor Mahia iliposhinda mchezo wake na Yanga Sc ya Tanzania.

Mchezaji kutoka Kenya Duke Abuya na wenzake wa Yanga SC timu ya Tanzania wamefuzu kuingia hatua ya makundi ligi kuu ya A...
26/10/2025

Mchezaji kutoka Kenya Duke Abuya na wenzake wa Yanga SC timu ya Tanzania wamefuzu kuingia hatua ya makundi ligi kuu ya Afrika CAFCL katika mchezo huo wa kimataifa dhidi ya Silver Strikers ya Malawi.

Kupitia ushindi huo Yanga wamepokea shilingi milioni 10 kutoka kwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu ambayo ni zawadi inayoitwa “goli la mama”.

Timu ya wanawake ya Kenya Harambee Starlets wameibuka na ushindi katika mchezo wa kimataifa ligi ya mabigwa ya wanawake ...
24/10/2025

Timu ya wanawake ya Kenya Harambee Starlets wameibuka na ushindi katika mchezo wa kimataifa ligi ya mabigwa ya wanawake Afrika WAFCON dhidi ya Gambia katika mkondo wa kwanza.

Kupitia ushindi huo Starlets wamepata shilingi milioni 10 kutoka kwa Rais William Ruto, huku rais Ruto akiwaahidi shilingi milioni moja moja kwa wachezaji kama wakipata ushindi katika mchezo wa marudiano mkondo wa pili utakao pigwa Jumanne huko Senegal au nusu milioni endapo watapata sare.

Mechi kati ya Bengo Youth na Home Boys imekamilika.Bengo amekubali kichapo cha bao 1:2 dhidi ya Home Boys mechi iliyoche...
20/10/2025

Mechi kati ya Bengo Youth na Home Boys imekamilika.
Bengo amekubali kichapo cha bao 1:2 dhidi ya Home Boys mechi iliyochezwa kwa kiwango kizuri mno.

FT
BENGO YOUTH 1:2 HOME BOYS FC

Ligi ya Chilibasi Super Cup inaendelea tena leo kwa mchezo mwingine unaowakutanisha Bengo Youth dhidi ya Home Boys fc. M...
20/10/2025

Ligi ya Chilibasi Super Cup inaendelea tena leo kwa mchezo mwingine unaowakutanisha Bengo Youth dhidi ya Home Boys fc.

Mechi hiyo ambayo itachezwa uwanja wa Mgalla Ground majira ya saa 5:00 asubui saa za Afrika Mashariki.

Bengo Youth vs Home Boys FC
11:00 AM
Mgalla Ground

Gavana wa Homabay Gladys Wanga ameutangazia umma mbele ya William Samoei Ruto angependa ubadilishwe jina uwanja wa Talan...
19/10/2025

Gavana wa Homabay Gladys Wanga ameutangazia umma mbele ya William Samoei Ruto angependa ubadilishwe jina uwanja wa Talanta Sports Stedium ambao bado upo katika hali ya ujenzi badala yake uitwe Raila Odinga Stedium.

19/10/2025

Mwenyekiti wa kikundi cha kujitegemea cha bwana Peter Mupe Kenga anawaalika kwenye kungamano la linalotarajiwa kufanyika uwanja wa Dip Mkapuni tarehe 20 mwezi huu.

Kungamano hilo ni kwaajili ya mashindano ya kisanaa kupitia vipaji mbalimbali ikiwemo usanii wa aina zote, waruka sarakasi, wachekeshaji na category nyingine nyingi.

Tuzo mbalimbali zitatolewa kwa waibuka ushindi kwenye mashindano hayo.
Munaalikwa nyote kuja kuburudika na kushuhudia mengi zaidi.

Seneta wa Kisumu profesa Tom Ojienda amezichora jina lake ng’ombe ambazo amezitoa kwaajili ya sherehe ya mazishi ya aliy...
18/10/2025

Seneta wa Kisumu profesa Tom Ojienda amezichora jina lake ng’ombe ambazo amezitoa kwaajili ya sherehe ya mazishi ya aliyekuwa waziri mkuu hayati Raila Odinga

"Nimezuiliwa kusafiri kwenda Tanzania na Uganda. Nilifukuzwa baada ya kuingia katika mataifa yote mawili kwa sababu Muse...
17/10/2025

"Nimezuiliwa kusafiri kwenda Tanzania na Uganda. Nilifukuzwa baada ya kuingia katika mataifa yote mawili kwa sababu Museveni na Suluhu hawataki kuniona, ilhali wao wanataka kuja Kenya kupitia Uwanja wa Ndege wa JKIA ulioko katika jimbo langu. Katika moja ya ziara zao, nitaandaa maandamano kufunga barabara na kuwafukuza warudi kwao. Wanalazimika kuonyesha heshima kwa Wakenya na viongozi wetu wanapozuru nchi zao." Babu Owino

Address

Kilifi

Telephone

+254793772989

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when RAHAI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share