SBS RADIO 94.4 FM

SBS RADIO 94.4 FM SBS 94.4 is a commercial regional radio station based in Kilifi town. It broadcasts in Swahili langu

🚨HABARI MTAMBUKA:Boniface Kariuki, mchuuzi wa barakoa aliyepigwa risasi na polisi katikati mwa mji mkuu wa Kenya Nairobi...
30/06/2025

🚨HABARI MTAMBUKA:

Boniface Kariuki, mchuuzi wa barakoa aliyepigwa risasi na polisi katikati mwa mji mkuu wa Kenya Nairobi, wakati wa maandamano juu ya marehemu Albert Ojwang' amefariki dunia.

Familia inalilia haki ya mwanao.


.4

🚨HABARI MTAMBUKASpika wa bunge la Kaunti ya Kilifi Teddy Ngumbao Mwambire amebanduliwa mamlakani.Kiasi cha madiwani 40 w...
30/06/2025

🚨HABARI MTAMBUKA

Spika wa bunge la Kaunti ya Kilifi Teddy Ngumbao Mwambire amebanduliwa mamlakani.

Kiasi cha madiwani 40 wameunga mkono hoja iliyowasilishwa na kiongozi wa wachache katika bunge hilo na diwani wa Tezo Thomas Chengo.

Madiwani 10 kati ya 50 wamepinga hoja hiyo.

Kiongozi wa wengi katika bunge hilo, Ibrahim Matumbo ameambia wanahabari kwamba hatua hiyo inalenga kurejesha uadilifu, haki na usahali wa shughuli za bunge.

Hoja hiyo imetaja matumizi mabaya ua ofisi yake, ukiukaji wa haki na usawa wakati vikao vya bunge.


.4

Dabaso, Kilifi: Rais William Samoei Ruto na aliyekuwa Waziri mkuu Raila Odinga  wamejumuika na mamia ya maelefu ya waomb...
25/06/2025

Dabaso, Kilifi:
Rais William Samoei Ruto na aliyekuwa Waziri mkuu Raila Odinga wamejumuika na mamia ya maelefu ya waombolezaji kwenye hafla ya maziko ya Mzee Baya Mung'aro Kaskazini mwa Kaunti ya Kilifi.

Mzee Baya ni baba mazazi wa Gavana Gideon Mung'aro wa Kilifi.

Mwili wa Babake Gavana wa Kilifi Gideon Maitha Mung'aro umefika nyumbani Kwake Dabaso, Kilifi Kaskazini kwa maziko kesho...
24/06/2025

Mwili wa Babake Gavana wa Kilifi Gideon Maitha Mung'aro umefika nyumbani Kwake Dabaso, Kilifi Kaskazini kwa maziko kesho Jumatano.Viongozi wengine wengi wa serikalini tayari washafika pia.

.4

🔴HABARI MTAMBUKA: NGUGI WA THIONG'O AMEFARIKI DUNIAMwandishi bingwa wa fasihi kutoka nchini Kenya Profesa Ngũgĩ wa Thion...
28/05/2025

🔴HABARI MTAMBUKA: NGUGI WA THIONG'O AMEFARIKI DUNIA

Mwandishi bingwa wa fasihi kutoka nchini Kenya Profesa Ngũgĩ wa Thiong'o amefariki dunia .

Kwa mujibu wa binti yake Wanjiku Wa Ngugi, Ngugi amefariki dunia hii leo Jumatano asubuhi, 28 Mei, 2025.

"Aliishi maisha yake, amevipiga vita vilivyo vyema. K**a alivyoomba, tusherehekee maisha na kazi yake." Ameandika.

Ngugi atakumbukwa kwa vitabu vyake vilivyoleta mapinduzi katika tasnia ya fasihi na kubadili maisha ya watu wakiwemo wanafunzi k**a vile Weep Not, Child (1964), The River Between (1967), A Grain of Wheat (1967) miongoni mwa vingine vingi.

Je unakumbuka kitabu gani chake ulichowahi kukisoma?


.4

The Premier League Liverpool sasa ni rasmi ndio mabingwa wa ligi kuu ya soka ya Uingereza kwa mara ishirini sawa na Manc...
25/05/2025

The Premier League
Liverpool sasa ni rasmi ndio mabingwa wa ligi kuu ya soka ya Uingereza kwa mara ishirini sawa na Manchester United. Hongera Liverpool.

Harusi tunayo hatuna:Hatimaye muunda maudhui kutoka Kwale, kusini mwa Pwani ya Kenya Beka Ruga wa Jimbo Media ameasi uka...
25/05/2025

Harusi tunayo hatuna:
Hatimaye muunda maudhui kutoka Kwale, kusini mwa Pwani ya Kenya Beka Ruga wa Jimbo Media ameasi ukapera rasmi. Hongera sana kaka, karibu kwenye chama.

The Eagle flies high to the Europa League:Crystal Palace ndio mabingwa wa kombe la FA nchini Uingereza. Ushindi huu ni t...
17/05/2025

The Eagle flies high to the Europa League:
Crystal Palace ndio mabingwa wa kombe la FA nchini Uingereza. Ushindi huu ni tiketi ya kukipiga Europa league msimu ujao. Ushindi huu pia unamanisha Palace imekuwa na msimu mzuri zaidi kuliko Arsenal. Hongera sana Palace.

.4

Pigo:Papa Leo wa XIV ametangaza kwamba kanisa Katoliki litabariki ndo kati yamwamume na mwanamke pekee kwa maana ndoa ni...
17/05/2025

Pigo:
Papa Leo wa XIV ametangaza kwamba kanisa Katoliki litabariki ndo kati yamwamume na mwanamke pekee kwa maana ndoa ni Muungano kati ya mwanaume na mwanamke na ndiyo inayokubalika mbele za Mungu.
Kwa maana hiyo ametangaza kwamba Sasa Kanisa Katoliki halitabariki tena ndoa za mashoga.

Papa Leo XIV maeyasema haya jana Mei 16, 2025 katika hutuba yake ya kwanza kwa mabalozi wa Vatican..

Papa Leo XIV pia amesisitiza msimamo wa Kanisa dhidi ya kuavya mimba na yuthanasia, akivitaja kuwa sehemu ya "utamaduni wa kutupa" wa kisasa.

Lakini pia amewakaribisha watu wa LGBTQ+ Kanisani ila mafundisho rasmi kuhusu ndoa na vitendo vya ushoga havijabadilika.


.4

Picha I hisani

17/05/2025

Wamunyoro, Nairobi.
Kwa kauli hii unahisi Rigathi Gachagua anafaa kuk**atwa kwa misingi ya kuchochea na kuvunja Amani nchini Kenya.
Disclaimer: Hii ni kauli na maoni binafsi ya Naibu Rais wa Zamani Rigathi Gachagua na haihusiani kivyovyote na maadili ya ya utendakazi wa SBS Radio.
Video I hisani

Nairobi, KenyaKanisa la Freemason lafungwa kwa kukosa kulipa kodi jijini Nairobi, Kenya.Unaonaje hili...    .4Picha I hi...
15/05/2025

Nairobi, Kenya
Kanisa la Freemason lafungwa kwa kukosa kulipa kodi jijini Nairobi, Kenya.
Unaonaje hili...

.4

Picha I hisani

Nairobi, KenyaAliyekuwa Naibu Rais wa Serikali ya awamu ya tano Rigathi Gachagua amezindua Chama Kipya Cha kisiasa kiitw...
15/05/2025

Nairobi, Kenya
Aliyekuwa Naibu Rais wa Serikali ya awamu ya tano Rigathi Gachagua amezindua Chama Kipya Cha kisiasa kiitwacho Democracy for Citizen Party (DCP) kikiwa na kauli mbiu 'Skiza Wakenya’.

Chama hicho kinatarajiwa kushiriki chaguzi ndogo kadha wa kadha zijazo pindi tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC itakaporejelea shughuli zake kamili.

Wachambuzi wa siasa za taifa hili la Afrika Mashariki wanasema hatua hii inaashiria kurejea kwa Gachagua kisiasa na mkakati mpya.

Je, unahisi hii ni njia sahihi ya Gachagua kurejea ulingoni? Tupe maoni yako.


.4

Picha I hisani

Address

1013
Kilifi
80108

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when SBS RADIO 94.4 FM posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to SBS RADIO 94.4 FM:

Share

Category