22/10/2025
                                            CARTELS WA SABABISHA BALAA LA MAJI KILIFI COUNTY!!
Kwakweli ni jambo la kusononesha jinsi ambavyo bidhaa hii muhimu kwa maisha ya kila siku ya binadamu kukosekana. Tunasema maji ni uhai na anayekunyima maji ni sawa tu anakutakifa kifo!
Je, tatizo ni nini hasa?? Mbona maji yatoke Sabaki hadi Mombasa na sisi tukose maji??
Cartels wamejaa kwenye hizi ofisi za Serikali ya Kaunti na washikadau wote wa huduma za maji. Wakubwa wanamwaga pesa maji ya fungwe ndio boashara zao ya kuuza maji kwenye magari inoge. Huku kwetu Kaloleni kunaye mfanyibiashara mmoja aliyefadhili kampeni za Mung'aro 2022 na yupo kwenye hii biashara. Wakati huo, tulikua tukijionea magari yaliyopakazwa Mung'aro na ODM huko chini karibu na stage ya mwisho wa lami. Sahii tunajua Gavana anaregesha mkono ila mbona atuumize sisi wanyonge?? Maji, "just a basic need" tunakosa ๐ข
Baadhi yetu wanalazimika kutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kujijenga kimaisha ๐
Inakata maini pale unapoletewa bill ghushi ya kukuumiza wakati hata maji hayakuwa yakitoka, mifereji inatoa upepo na wanakulazimisha kulipa.
Vidzasinya Asena!!