K.P.C MEDIA

K.P.C MEDIA K.P.C MEDIA ni jukwaa la Habari, Siasa, Uongozi na Maendeleo ya Kaunti ya Kilifi.
(1)

HOSPITALI YA KISASA YA MARIAKANI YAENDELEA KWA KASI - UJENZI WAFIKA GHOROFA YA PILIUjenzi wa Hospitali ya kisasa ya Mari...
15/07/2026

HOSPITALI YA KISASA YA MARIAKANI YAENDELEA KWA KASI - UJENZI WAFIKA GHOROFA YA PILI

Ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya Mariakani unaendelea vizuri, huku kazi zikiwa zimefikia ghorofa ya pili. Hii ni kulingana na taarifa iliyotolewa na Gavana wa Kaunti ya Kilifi, Gideon Maitha Mung'aro.

Picha zilizopigwa eneo la mradi zinaonyesha maendeleo makubwa, nguzo za chuma (steel bars) zikiwa zimesimamishwa tayari kwa floor ya pili, crane ikifanya kazi eneo la mradi, na muundo wa jengo ukionekana wazi kutoka angani ukiwa na sehemu mbalimbali za majengo.

Kulingana na Gavana Mung'aro, mradi huu ukikamilika utaboresha pakubwa utoaji wa huduma za afya kwa wakazi wa , Kilifi kwa jumla na hata kaunti jirani.

KIMBILIO RESCUE CENTRE, KIBARANI!!Kaunti ya Kilifi jana ilishuhudia hafla muhimu ya uzinduzi na makabidhiano rasmi ya Ki...
15/07/2026

KIMBILIO RESCUE CENTRE, KIBARANI!!
Kaunti ya Kilifi jana ilishuhudia hafla muhimu ya uzinduzi na makabidhiano rasmi ya Kimbilio Rescue Centre, kituo kilichojengwa eneo la Fumbini, Kibarani Ward. Kituo hiki kitatoa hifadhi salama kwa waathiriwa wa Ukatili wa Kijinsia (GBV) kutoka sehemu mbalimbali za Kaunti ya Kilifi.

Mradi huu umefadhiliwa na Children's Investment Fund Foundation (CIFF) na kutekelezwa na Shining Hope for Communities (SHOFCO) kwa ushirikiano na Serikali ya Kaunti ya Kilifi. Kituo kitatoa huduma za ushauri nasaha, matibabu, malazi ya muda, mafunzo ya ujuzi, na sehemu maalum za watoto ili kuwasaidia waathiriwa kujijenga upya kwa heshima.

Sehemu mpya zilizokamilika kwenye kituo ni pamoja na eneo la mapokezi, kituo cha muuguzi, chumba cha ushauri nasaha, chumba cha mafunzo ya ujuzi, eneo la kulia chakula, jiko la kisasa, eneo la michezo ya watoto, na vyoo. Sehemu hizi zitaungana na bweni lililopo tayari, hivyo kufanya Kimbilio Rescue Centre kuwa kituo kamili chenye ulinzi, matunzo, na fursa za maisha mapya kwa waathiriwa.

Serikali ya Kaunti ya Kilifi ilisema kulinda watu walio hatarini zaidi katika jamii ni jukumu la pamoja, na iliahidi kuendelea kuunga mkono mipango inayoimarisha mifumo ya ulinzi wa jamii, kurejesha matumaini kwa waathiriwa, na kuhakikisha hakuna mtu anayekabiliana na ukatili au dharura peke yake.

Hafla hii ya uzinduzi ilihudhuriwa na Ms. Anne Wang'ombe, PS wa State Department for Gender and Affirmative Action; H.E. Flora Mbetsa Chibule, Deputy Governor wa Kilifi; Women Rep wa Kilifi Hon. Gertrude Mbeyu Mwanyanje; pamoja na maafisa wengine wa Serikali ya Kaunti na Kitaifa, wadau wa maendeleo, na wananchi.

KILIFI COUNTY LEADERS FACE UNCERTAIN 2027, AS NEW RANDOM POLL EXPOSES WIDE GAPS IN RE-ELECTION CONFIDENCE‼️A new opinion...
15/07/2026

KILIFI COUNTY LEADERS FACE UNCERTAIN 2027, AS NEW RANDOM POLL EXPOSES WIDE GAPS IN RE-ELECTION CONFIDENCE‼️

A new opinion poll we conducted has revealed sharply divided fortunes among Kilifi County's ten most prominent elected leaders, with confidence in re-election ranging from a commanding 90 percent to a troubling 25 percent, just over a year before Kenyans go to the polls in 2027.

The poll, which sampled public and online sentiment across the county's constituencies, placed Kilifi North MP Owen Baya Cbs at the top of the list with a 90 percent re-election rating, followed by Ganze MP Hon. Kenneth Charo Kazungu Tungule at 70 percent and Rabai MP Hon. Anthony Kenga Mupe at 60 percent.

The trio's strong numbers reflect sustained visibility and delivery on development pledges within their respective constituencies.

The picture grows more competitive in the middle tier. Malindi MP Hon. Amina Mnyazi polled at 50 percent, while Kaloleni MP Hon.Paul Katana - PK followed closely at 45 percent.

Perhaps the most striking figure in this bracket belongs to Governor Gideon Maitha Mung'aro , who registered only 40 percent, a number that places the county's chief executive below three sitting MPs, despite presiding over the entire devolved unit.

At the lower end of the spectrum, the poll paints a difficult picture for four leaders. Kilifi South MP Hon. Richard Ken Chonga
stood at 35 percent, while Woman Representative mama Hon Gertrude Mbeyu Cbs and Magarini MP Hon Harrison Garama Kombe were tied at 30 percent each.

Bottom of the list was Senator Hon. Stewart Madzayo,EGH,MP. , who polled at just 25 percent, the lowest confidence rating of any leader surveyed, despite serving his third term.

The results point toward a potentially turbulent 2027 cycle for Kilifi County, particularly at the gubernatorial and senatorial level, where incumbents typically enjoy greater name recognition and resource advantage.

NOTE ‼️ K.P.C MEDIA notes that these figures represent a snapshot of current public sentiment and remain subject to change as campaigns intensify and party alignments take shape ahead of the election. We will continue to track these numbers as the 2027 race develops.

GANZE: WAKAAZI WANALIKWA KWENYE MIKUTANO YA PUBLIC PARTICIPATION YA NG-CDFWakaazi wa Ganze wanaalikwa kushiriki mikutano...
15/07/2026

GANZE: WAKAAZI WANALIKWA KWENYE MIKUTANO YA PUBLIC PARTICIPATION YA NG-CDF

Wakaazi wa Ganze wanaalikwa kushiriki mikutano ya hadhara ya NG-CDF itakayoongozwa na Mbunge Hon. Kenneth Kazungu (Tungule), kuanzia wiki hii katika wadi zote nne za Ganze.

Ratiba ni k**a ifuatavyo:
🔴 GANZE WARD – Alhamisi 16/7/2026, saa nne (10:00am) asubuhi, DCC Board Room

🟢 SOKOKE WARD – Alhamisi 16/7/2026, saa nane (2:00pm) mchana, ACC Grounds

🔴 JARIBUNI WARD – Ijumaa 17/7/2026, saa nne (10:00am) asubuhi, Mwapula Secondary

🟢 BAMBA WARD – Ijumaa 17/7/2026, saa nane (2:00pm) mchana, First Vision Hall

Wananchi wanahimizwa kuhudhuria kwa wingi ili kutoa maoni yao juu ya matumizi ya fedha za NG-CDF katika wadi zao

K**A WEWE NI BOYCHILD, PLEASE USIPITE HII POST BILA KUSOMA. Leo tufunguane macho. Most men usually say, “No man should b...
14/07/2026

K**A WEWE NI BOYCHILD, PLEASE USIPITE HII POST BILA KUSOMA. Leo tufunguane macho.

Most men usually say, “No man should be forced to provide for a child he did not consent to conceive.” Na hapo ndipo wanaume wengi hukosea. Zaidi ya 90% ya wanaume hukosa kuelewa point hii kila wakati.

WACHA LEO TUJIFUNZE KITU KUHUSU BABY MAMA DRAMA. When a baby mama takes you to court for child upkeep, si mama ndiye anakushtaki. Ni mtoto. Mtoto hawezi kuongea wala kufungua kesi mwenyewe, ndio maana mama anafanya hivyo on behalf of the child. Ndio maana kwa court papers utaona imeandikwa: “The mother suing on behalf of the child.”

KUMBUKA, wakati ulikuwa na mrembo kitandani ukienjoy, huyo mtoto hakuwepo. Kwa umakini au uzembe wenu, mtoto akaja miezi 9 baadaye. Sasa ni haki yake kudai malezi kupitia kwa mama yake.

Wanaume wengi hudhani ni mwanamke ndiye anawahangaisha. Hapana. Hata ndugu au mtu mwingine wa inje anaweza kufungua child maintenance case kwa niaba ya mtoto. Na hii pia inaenda pande zote. Baba anaweza kumshtaki mama kwa niaba ya mtoto. Haki hiyo ya mtoto iko ndani ya katiba na hakuna mtu anaweza kuiondoa.

Article 53(1)(e) inasema: “Every child has a right to parental care and protection, which includes equal responsibility of the mother and father to provide for the child, whether they are married to each other or not.”......Soma hizo words za mwisho tena: “Whether they are married to each other or not.”

Article 53(2) inasema: “A child’s best interests are of paramount importance in every matter concerning the child.”...... Best interest ya mtoto. Sio ya mama.

Kwa hivyo mwanaume yeyote anayesoma hii, ukipelekwa kotini juu ya upkeep ya mtoto, kumbuka si baby mama wako anakushtaki. Ni mtoto wako mwenyewe anadai haki yake.

No man should bring a child into this world alafu akatae responsibility. Be responsible. Tumia CD k**a ni lazima uonje sambusa. Ama uoe tu.
By K.P.C MEDIA

SUPERMARKET MPYA YA CARREFOUR  KUFUNGULIWA RASMI KESHO, KIBAONI, KILIFI
14/07/2026

SUPERMARKET MPYA YA CARREFOUR KUFUNGULIWA RASMI KESHO, KIBAONI, KILIFI

KILA MTU MWENYE SHIDA ATAENDA KWA PRESIDENT??
14/07/2026

KILA MTU MWENYE SHIDA ATAENDA KWA PRESIDENT??

KWAMBOX AWASHAURI WALAJI WA JABA KULIOSHA KWA MAJI YA MOTO KABLA YA KUTAFUNA ‼️Kwambox amewashauri watu wanaotafuna Jaba...
14/07/2026

KWAMBOX AWASHAURI WALAJI WA JABA KULIOSHA KWA MAJI YA MOTO KABLA YA KUTAFUNA ‼️

Kwambox amewashauri watu wanaotafuna Jaba (Miraa na Mugokaa) kuliosha kwa maji ya moto kabla ya kuanza kutafuna, akisema hiyo itasaidia kuondoa mabaki hatari ya dawa za kuulia wadudu (pesticides) zinazoweza kuwa zimebaki kwenye majani wakati wa kilimo.

Wataalamu wa afya kwa muda mrefu wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa kuosha mazao yanayoliwa yakiwa mabichi kabla ya matumizi, ili kupunguza hatari ya sumu na vijidudu vinavyoweza kusababisha madhara mwilini.

Je, wewe k**a mlaji wa Jaba, utafuata ushauri huu wa kuliosha kwa maji moto kabla ya kutafuna ama KUFA dereva KUFA abiria?

Fikirini Jacobs “Mimi k**a PS, nafanya hii  kazi kwa bidii sana na najituma, nawaahidi sitawaangusha jamii yangu ya Miji...
14/07/2026

Fikirini Jacobs
“Mimi k**a PS, nafanya hii kazi kwa bidii sana na najituma, nawaahidi sitawaangusha jamii yangu ya Mijikenda. MaPS hapa Kenya ni 57, lakin kwa jamii ya Mijikenda niko mimi pekeangu”

POLITICAL ANALYSIS || KWA NINI BEN KAI AMEAMUA KUGOMBEA UGAVANA KILIFI, 2027Habari mpya zinazoendelea kutikisa siasa za ...
14/07/2026

POLITICAL ANALYSIS || KWA NINI BEN KAI AMEAMUA KUGOMBEA UGAVANA KILIFI, 2027

Habari mpya zinazoendelea kutikisa siasa za Kaunti ya Kilifi ni kwamba Ben Kai Chilumo, CEO wa Huduma Centre, ametangaza nia yake ya kugombea kiti cha Ugavana wa Kilifi mwaka 2027.

LAKINI KWA NINI SASA?
Ben Kai ni mmoja wa watu wanaojulikana kuwa karibu sana na Hon. Aisha Jumwa Katana, mgombea wa UDA. Aisha Jumwa alishatangaza kitambo kwamba mgombea mwenza wake (deputy) atatoka jamii ya Chonyi, na kwa kuwa Ben Kai anatoka jamii hiyo, wengi waliamini ni yeye ndiye angekuwa deputy wake.

Kwa Ben Kai kutokea sasa na kutangaza azma yake ya kugombea Ugavana, hii haiwezi kuwa bahati mbaya....ni mkakati wa kisiasa.

Inawezekana Ben Kai ametangaza nia hii ili kujijengea msingi wake wa kisiasa (political base). Ajenda yake kuu inaweza kuwa kuwaunganisha wapiga kura wa Chonyi, ajijengee "backing" ya kutosha nyumbani, ili wakati muda ukifika, kambi yake pamoja na ile ya Aisha Jumwa ziweze kwa urahisi kumshinda Mung'aro.

Huu unaweza kuwa mkakati wa muda mrefu kutoka kwa Aisha Jumwa mwenyewe. Kumbuka Gavana Mung'aro ana deputy kutoka Rabai, na ikiwa Aisha Jumwa naye atakuja na deputy wa Chonyi... vita hivi vitakuwa vya kuvutia sana.

Address

80108
Kilifi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when K.P.C MEDIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share