06/06/2025
Asubuhi njema mashabiki wangu wapendwa,
Leo nataka kusema jambo moja la kweli—kutetea jina langu, kazi yangu, na hadhi ya studio yangu Annointmediastudios, ambayo tumeijenga kwa jasho, maumivu, na maombi.
Kuna ujumbe unazunguka mitandaoni ukidai kuwa nimeharibu ndoa ya mtu, eti nimeingilia akaunti zake au nilitaka uhusiano wa karibu. Ukweli ni huu:
Tulifanya kazi ya muziki pamoja kwa makubaliano kwamba mimi nisimamie upande wa audio, yeye asimamie video. Pia tulikubaliana kuwa kila mmoja atakuwa huru kuweka kazi hiyo kwenye chaneli yake, au mmoja akigharamia vyote basi tupeane link rasmi. Hilo halikutimizwa k**a ilivyopangwa.
Kuhusu madai ya uhusiano wa karibu—ni kweli alinitaka kwa njia hiyo, lakini nilikataa kwa heshima kwa sababu yeye ni mke wa mtu. Niliheshimu ndoa yake na nikaweka mipaka. Tangu hapo mambo yalibadilika. Kazi zimefutwa, nimezuiwa, na sasa kuna juhudi za kunichafulia jina mitandaoni.
Lakini nasema kwa moyo wangu wote: mimi ni yatima. Sina baba, sina mama. Kila hatua niliyoipiga ni kwa juhudi zangu mwenyewe. Hakuna mtu aliyenijenga—Mungu alinisaidia, na nimepambana mwenyewe hadi leo.
Annointmediastudios si jina la mtaa—ni kazi ya miaka, ni jasho halali, na ni baraka.
K**a mtu anafikiri ataangusha jina langu kwa maneno ya uongo, hawezi. Tuko hapa kwa sababu ya neema ya Mungu na bidii ya kweli.
Na mwisho kabisa, nataka kuwaambia:
"Mtoi mwenye tunda ndiye hurushiwa mawe."
Mimi nitaendelea na kazi yangu. Sitabishana. Najua ukweli wangu, na najua nyinyi mnaounga mkono mnaona kazi yetu ya kweli.
Ahsanteni sana. Mbarikiwe.