08/12/2025
πͺππ£πππππππ πͺππ πππ ππ§π π π§π¨ππ¨π ππͺπ π ππ¨π¨ πͺπ πͺπππ πͺπ πππππͺπ πππ ππ ππ‘π
Maafisa wa upelelezi wamemnasa mtuhumiwa mkuu wa wizi wa kahawa katika eneo la Kimimini na kurejesha shehena kubwa ya kahawa iliyokuwa imeibwa.
Wizi huo ulifikia kilele usiku wa Novemba 25, 2025, baada ya genge la takriban wahalifu 50 kuvamia kiwanda cha Sowek Kenya Company Limited, kukata uzio, kuwafunga walinzi na kutoroka na magunia tisa ya kahawa.
Siku moja kabla, majambazi wengine walivamia Kiwanda cha Ushirika wa Wakulima wa Kiungani na kuiba takribani magunia 25 ya kahawa ya P1 baada ya kutoboa ukuta na kupenya kwenye eneo la kukausha.
Kupitia uchunguzi wa kisayansi, polisi walimk**ata Gregory Kingasia Wekesa, anayejulikana kwa kununua kahawa kutoka vyanzo visivyo halali. Alik**atwa na jumla ya magunia 18 ya kahawa, yakiwemo kilo 500 ndani ya nyumba yake na kilo 1,300 nyingine zikiwa nje zikikauka.
Mtuhumiwa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kimimini huku akitarajiwa kufikishwa mahak**ani.