
20/06/2025
Gavana wa Jiji kuu la Nairobi Johnson Sakaja amekanusha madai kuwa alitoa shilingi milioni 2 kwa aliyekuwa Rais wa Bunge la Mwananchi Calvince Okoth maarufu Gaucho.
Ripoti ziliibuka kuwa kabla ya maandamano ya jumaatano, gavana huyo alikutana na viongozi kadhaa, akiwemo Gaucho na jamaa mmoja maarufu Swaleh, na kuwapa Shilingi milioni 2 fedha za kuwafadhili wahuni kwenye maandamano hayo.
Katika kujieleza kwa haraka, Sakaja amejitenga na tuhuma hizo na kufafanua kuwa siku hiyo hakuwepo Jijini, akitoa ushahidi, bosii huyo wa Jiji kuu la Kenya amefichua kwamba alikuwa amesafiri kule Lugari na hakuitisha mkutano huo unaodaiwa.
"Uongo huo wa wazi. Jumapili, nilikuwa Lugari kwa Kanisa na nikarudi Nairobi Jumatatu alasiri kupitia Kitale. Sijaona Gaucho tangu alipohudhuria Uzinduzi wa Mukuru Housing au Swaleh kwa miezi mingi," Sakaja alifafanua.