
30/07/2025
Naamini kwa watu.
Sio tu kwa yale wanayoweza kufanya, bali kwa vile walivyo.
Miaka imenifundisha kuwa watu si sehemu ya safari , watu ndio safari yenyewe.
Nimeona kuwa unapowekeza kwa watu kwa muda wako, upendo, ushauri, na uhusiano wa kweli unajenga kitu cha milele.
Nathamini watu kuliko vitu, kwa sababu watu hubeba ndoto, vipawa, na maagizo ya Mungu.
Nimeamua kutembea na watu, sio mbele yao.
Nimeamua kujenga mahusiano, sio majukwaa.
Maana majukwaa hupita, lakini watu hubaki.
Hii ndiyo imani yangu.
Na kadri Mungu anavyoendelea kuniinua, nitazidi kuinua wengine.
Presenter Ambasa
Singing To The Heavens