04/10/2025                                                                            
                                    
                                                                            
                                            Rais wa Madagascar Andry Rajoelina alisema siku ya Ijumaa yuko tayari kusikiliza malalamishi ya vijana wa GEN Z wanaoandamana kote nchini kutafuta suluhu la matatizo yanayokabili taifa hilo. Hata hivyo, Rajoelina alipuuza wito wa kumtaka ajiuzulu kutoka kwa waandamanaji.
"Hakuna anayefaidika na uharibifu wa taifa. Niko hapa, nimesimama hapa tayari kusikiliza, tayari kunyoosha mkono wa usaidizi na zaidi ya yote, tayari kuleta suluhisho kwa Madagascar," Rajoelina alisema katika hotuba iliyotangazwa kwenye ukurasa wake wa Facebook.
 !