Pwani Media Network

Mwakilishi Wadi ya Ganda Hon. Oscar Wanje amekemea vikali hatua ya kunyanyaswa, kutishiwa na kudhulumiwa kwa wafanyibias...
02/06/2026

Mwakilishi Wadi ya Ganda Hon. Oscar Wanje amekemea vikali hatua ya kunyanyaswa, kutishiwa na kudhulumiwa kwa wafanyibiashara wa pombe ya mnazi Malindi, akitaja kwamba biashara hiyo ni chanzo kikubwa cha kipato kwa familia nyingi tangu jadi.

Kauli yake inajiri baada ya wafanyibiashara wengi wa Mbuzi Wengi, mjini Malindi kuk**atwa na maafisa wa polisi hapo jana, huku biashara yao ikipata hasara kubwa. Mheshimiwa Oscar Wanje katika kauli yake, amesema kwamba endapo ni swala la leseni, au sheria, basi swala hilo wafanyibiashara na jamii - watumizi, wahusishwe na kuelemishwa kwa njia ya mazungumzo ili kuhakikisha biashara hii ambayo ni kitega uchumi cha familia nyingi iendelee tu k**a biashara nyingine.

"Ikiwa kuna maswala ya liseni, au sheria, yashughulikiwe kwa njia ya mazungumzo na kufuata taratibu za kisheria, si kwa dhulma au matumizi mabaya ya mamlaka.'' ~ Oscar Wanje

Swala la unyanyasaji kwa wafanyibiashara hawa limezua hisia mseto huku wakazi wa Malindi na Pwani kwa jumla wakikosoa hatua ya kuk**atwa kwa wachuzi hao, na pia matumizi mabaya ya mamlaka dhidi yao.

Wengi wa wakazi wa Pwani wanauliza kwa nini biashara ya Mugoka isidhibitiwa k**a wanavyotaka biashara ya mnazi idhibitiwe vikali?

Kwa nini biashara ya mugoka inauzwa usiku na mchana bila kudhibitiwa?

Kwa nini wauzaji Mugoka na Miraa hawak**atwi usiku?

Wakazi wa Malindi na Pwani wamemuunga mkono kiongozi Oscar Wanje wakisema kwamba Mnazi si biashara tu, ni kitambulisho cha jamii ya pwani - kitambulisho cha uasili wa Wapwani.




Kesho, Hon. Oscar Wanje atakuwa anawasilisha rasmi hatimiliki ya ardhi (Title Deed) kwa wakazi wa Mtakatieni, Kijiwetang...
28/05/2026

Kesho, Hon. Oscar Wanje atakuwa anawasilisha rasmi hatimiliki ya ardhi (Title Deed) kwa wakazi wa Mtakatieni, Kijiwetanga.

Ardhi hiyo inajumuisha ekari 327.8. Kwa miaka mingi wakazi wa eneo hili wakuwa wakiteseka wakikosa mtu wa kumshika mkono kufikia hatua hii muhimu, licha ya uwepo wa viongozi. Hon. Oscar Wanje - MCA Ganda Ward alijizatiti, na kujitolea kuhakikisha anashirikiana na wenyeji wa eneo hilo kufikia hatua hii.

Kesho, Wakazi wa Mtakatieni wanatoka kwenye jina la Uskwota na kuwa wamiliki rasmi wa ardhi.

Hongera Mhe. Oscar Wanje.

"Ni safari tuliyoanza kitambo sana, tunashukuru Hon. Oscar Wanje kwa kutushika mkono kununua ardhi ya shule ya Amani na ...
22/05/2026

"Ni safari tuliyoanza kitambo sana, tunashukuru Hon. Oscar Wanje kwa kutushika mkono kununua ardhi ya shule ya Amani na pia sasa kutusaidia ujenzi wa madarasa haya."

Wakazi wa Mashamba

Mwakilishi wa Wadi ya Ganda Mhe. Oscar Wanje, kupitia ofisi yake, mnamo tarehe 21 Mei 2026 alizindua rasmi mradi wa ujenzi wa madarasa katika Shule ya Chekechea ya Amani ECDE iliyopo eneo la Masham…

Hon. Oscar Wanje Kuzindua mradi wa ujenzi wa madarasa kwa shule ya Chekechea ya Amani, Mashamba hapo kesho Tarehe 21 Mei...
20/05/2026

Hon. Oscar Wanje Kuzindua mradi wa ujenzi wa madarasa kwa shule ya Chekechea ya Amani, Mashamba hapo kesho Tarehe 21 Mei 2026, Saa tatu.

Hii ni hatua muhimu ya kuhakikisha wanafunzi wetu wanasoma katika mazingira yaliyosalama.

Mtetezi wa Maswala ya Ardhi Malindi.Baada ya wakazi wa Mtakatieni, Kijiwetanga Wadi ya Ganda, kupata changamoto kubwa kw...
20/05/2026

Mtetezi wa Maswala ya Ardhi Malindi.

Baada ya wakazi wa Mtakatieni, Kijiwetanga Wadi ya Ganda, kupata changamoto kubwa kwa zaidi ya muongo mmoja kupata hatimiliki halali ya ekari 327.8 za Plot 333, sasa shida hiyo wameizika kwa kaburi la sahau baada ya kumuhusisha Hon. Oscar Wanje

Mhe. Oscar baada ya kuona uzito wa swala hilo mwaka wa 2024, alilivalia njuga, kwa ujasiri na ushirikiano na wanajamii wa Mtakatieni, na asasi za kisheria kuhakikisha hatua zote za kisheria zinafuata ili kufua dafu kwenye mchakato mzima.

Mapema wiki hii, Mhe. Oscar Wanje aliweza kuwasilisha hatimiliki kwa wanak**ati wa ardhi hiyo, hatimiliki ambayo ilikuwa changamoto kubwa kuipata kwa muda mrefu licha ya kuwahusisha viongozi mbalimbali na kuwaacha raia bila jawabu wala kuonyesha nia ya kutafuta suluhu.

Mhe. Oscar Wanje alijukumika kupitia nafasi yake k**a mwakilishi wadi ya Ganda kusimamia swala la usoroveya na kuwekwa mipaka rasmi (Beaconing) hadi hatua hiyo kubwa ya kupata hatimiliki kuu ya ardhi hiyo. Hatua chache zimebaki kuhakikisha ugawaji wa Shamba na hatimiliki za ardhi kwa kila mwenye kipande cha ardhi kwenye ardhi hiyo ya Plot 333.

Oscar Wanje ameonesha nia, na uwezo mkubwa wa kuikomboa jamii kwa swala la Uskwota, hivyo kuwatunza wananchi kutokana na unyanyasaji wa kuvunjiwa manyumba, au hofu ya kufurushwa kwenye ardhi ambayo wako na haki rasmi ya kumiliki.

15/05/2026

Mhe. Oscar Wanje ameendelea kuonesha msimamo wake thabiti katika kutetea haki ya wananchi kumiliki ardhi, kupitia mapendekezo aliyoyawasilisha juzi kwenye Bunge la Kaunti ya Kilifi kuhusu mswada wa Ardhi Fund.

Katika hoja yake, alipendekeza kuwepo kwa asilimia maalum kutoka kwenye makusanyo ya Land Rates ya Kaunti ya Kilifi itakayowekezwa kwa ajili ya ununuzi wa ardhi katika maeneo ambayo wananchi bado wanaishi k**a maskwota.

Hatua hiyo imepokelewa vyema na wananchi, hususan wa eneobunge la Malindi, ambao wameielezea k**a mwanzo wa suluhu ya kudumu katika kupambana na changamoto ya uskwota. Wengi wamepongeza maono na jitihada za Hon. Oscar Wanje za kuhakikisha wananchi wanapata haki, usalama wa umiliki wa ardhi, na heshima ya maisha yao.

Eneobunge la Malindi limekumbwa na changamoto nyingi licha ya kuwa na uongozi ulio na fursa kubwa ya kuzishughulikia na ...
09/05/2026

Eneobunge la Malindi limekumbwa na changamoto nyingi licha ya kuwa na uongozi ulio na fursa kubwa ya kuzishughulikia na kuleta suluhu la kudumu kwa Wanamalindi.

Mojawapo ya changamoto kuu ni swala la Uskwota na Unyakuzi wa ardhi kwa wananchi wa Malindi. Hon. Oscar Wanje katika uwezo wake, amekuwa mstari wa mbele sana kwa ushirika mkuu na wananchi kuhakikisha kwamba swala la Uskwota na Unyakuzi wa ardhi katika eneowadi analotoka na maeneo mengine kwenye eneobunge linapungua.

Mh. Oscar Wanje aliweza kushirikisha viongozi mbalimbali, na licha ya kukosa ushirikiano wa kimaono mapana ya kumfaidi mwananchi, halikumsimamisha hilo, na hatimaye alifika kwenye bunge la Seneti, akawasilisha kilio cha wananchi kwa Kamati ya Seneti kwa maswala ya Ardhi, hatua iliyoisukuma k**ati hiyo kufika Wadi ya Ganda na kuendeleza mchakato mzima wa kutafuta haki kwa wananchi ambao ardhi zao zimenyakuliwa na kutoa muongozo mwafaka wa kujikomboa kutoka swala la Uskwota.

Hulka hii ya Mh. Oscar Wanje ya kuweka maswala ya kuboresha maisha ya wananchi kipaumbele, ndio uongozi ambao wanamalindi wamekuwa wakiuhitaji kwa muda sasa.

Wakati umefika wa watu wa Malindi kujikomboa, kwenye lindi la Dhulma za kihistoria za haki ya kumiliki ardhi, kujitoa kwenye lindi la umaskini, kuboresha Miundombinu ya elimu, barabara, usalama na kuwawezesha vijana kupitia nafasi za ajira na ujuzi pamoja na kina mama.


Maandamano Kilifi.Wakaazi kutoka kila pembe za kaunti ya Kilifi wajitokeza kwenye Maandamano ya kupigania haki na usalam...
06/05/2026

Maandamano Kilifi.

Wakaazi kutoka kila pembe za kaunti ya Kilifi wajitokeza kwenye Maandamano ya kupigania haki na usalama kwa jinsia ya k**e, huku wengi wakionekana wakishika mabango yenye ujumbe wa kukomesha Dhulma za Kijinsia.

Hatua hii inajiri siku chache tu baada ya tukio la kutamausha huko Kilifi ambalo liliacha msichana Keziah Matuki (7) akiwa marehemu huku uchunguzi ukibainisha kwamba alinyongwa na kunajisiwa.

Kutoka kwetu Pwani Media Network, tunaungana na msimamo kuwa kila mtu mbali na utofauti wa kijinsia, anafaa kupata haki na hafai kudhulumiwa kwa namna yoyote ile.



//Picha Kwa Hisani - King Lastborn & Shampuz Media//

Gavana wako je?Huku ni gatuzi la Kiambu, kaunti inayoongozwa na Kimani Wamatangi. Utoaji huduma za dharura kupitia ambul...
04/05/2026

Gavana wako je?

Huku ni gatuzi la Kiambu, kaunti inayoongozwa na Kimani Wamatangi. Utoaji huduma za dharura kupitia ambulensi umewezeshwa kwa uwepo wa ambulensi 19 zilizowekwa vifaa vyote muhimu, pamoja na wahudumu wakutosha.

Hali ikoje kwenye sekta hii katika idara ya afya kwenye kaunti yako?

Hon. Oscar Wanje anaendelea kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wakazi wa eneobunge la Malindi huku maandalizi ya uc...
02/05/2026

Hon. Oscar Wanje anaendelea kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wakazi wa eneobunge la Malindi huku maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2027 yakizidi kushika kasi.

Mhe. Oscar Wanje anaendelea kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wakazi wa eneobunge la Malindi huku maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2027 yakizidi kushika kasi. Asilimia kubwa ya wananchi wanamta…

Address

Malindi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Pwani Media Network posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share