16/10/2025
Afisa wa zamani wa magereza amezua mjadala mkubwa nchini baada ya kufichua hadharani kuwa anapitia kipindi kigumu cha madeni, msongo wa mawazo na kutengwa kijamii miezi kadhaa baada ya kufutwa kazi kwa kushiriki maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha.
Kupitia ujumbe wa kihisia alioweka kwenye mitandao ya kijamii, alieleza kuwa maisha yake yamebadilika kabisa, amepoteza ajira, hana uwezo wa kulipa bili, anatishiwa kuk**atwa kutokana na madeni, na anahisi amefikia hatua ya chini kabisa maishani.
“Nina deni, nimepigwa mnada, nina hati ya kuk**atwa, siwezi kulipa bili zangu wala kumtunza binti yangu. Nimejaribu kuwa imara, lakini maisha yamekuwa mazito sana,” aliandika.
Rafiki… ukiwa kwenye nafasi k**a hii, unaeza acha kazi yako ili kupigania Haki za taifa lako?