31/12/2025
IMPACT OF KUZA TALANTA 💔➡️❤️
Saba Saba – Malindi, Kwa Vumbi.
Wengi wetu tunajua hii area. Tunajua hadithi za Woza Woza. Tunajua mihadarati, vishawishi na mazingira ambayo hayako salama kwa watoto. Bila mentorship, bila mtu wa kushika mkono, mtoto wa Saba Saba anaweza potea kirahisi sana.
Lakini hapa ndipo KUZA TALANTA ilipoamua kusema HAPANA.
Kupitia KUZA TALANTA League na mentorship zake, METRO UNITED imeonyesha kuwa mpira si mchezo tu — ni kinga, ni matumaini, ni njia ya kuokoa maisha. Watoto ambao wangeingia barabarani leo wako uwanjani. Wale ambao wangeharibiwa na mihadarati leo wana ndoto, nidhamu na mwelekeo.
Hii si bahati.
Hii ni kazi.
Hii ni kujitolea.
Hii ni mapenzi ya kweli kwa jamii.
Tunapongeza sana entire coaching team wa METRO UNITED kwa moyo wenu, kwa uvumilivu wenu na kwa kusimama na watoto pale ambapo wengi wamewatelekeza. Mnafanya kazi ambayo huonekana kidogo sana, lakini impact yake ni kubwa sana.
KUZA TALANTA sio league tu.
Ni ulinzi wa watoto wetu.
Ni matumaini ya kizazi kijacho.
Ni ushahidi kwamba impact ya kweli huanzia ground.
👏👏👏