03/01/2024
Warahisishie kazi unaowaomba msaada, usiwape kazi ya kuwaza majibu au njia ya kukusaidia. Nenda ukiwa na majibu pengine wao watabaki kukusaidia.
Mfano 1:
Una kipaji cha mziki, unaenda kwa mtu unamuambia “Naomba unishike mkono”. Unampa yeye kazi tena ya kuwaza kukushika mkono’ ni nini?. Omba huo msaada mahususi, eleza bayana namna unayotaka usaidiwe mtu aone k**a anaweza au hawezi. Unaweza kusema “Naomba niongezee pesa ya kwenda studio / Naomba nisaidie kufikisha nyimbo zangu redio au jambo lingine.
Mfano 2:
Unatafuta kazi, unaniambia kaka “Nitafutie kazi yoyote”. Bro kazi yoyote ni kitendawili, kwa sababu ukweli ni kwamba kuna kazi huwezi kufanya. Rahisisha kwa kueleza angalau kazi kadhaa unazoweza kufanya, ikiwezekana niambie ofisi fulani kuna nafasi na anayehusika ni fulani (tafuta mawasiliano yake ikiwezekana).