13/01/2025
: Hivi umewahi kukaa chini ukashangaa kwanini kila ndugu, jamaa, au rafiki zako wanafanikiwa katika mipango yao k**a walivyopanga? Wanapata kazi nzuri, wanafanikiwa kwenye biashara zao, wanaoa/wanaolewa na watu waliowapenda?
Kimsingi wanafanikiwa kwa kila jambo. Lakini wewe ume-stuck, mambo yako hayaendi na upo pale pale!!
Tafadhali, usipoteze matumaini. Sababu kubwa ni kwamba wao wapo kwenye msimu wao. Wala usiwaonee wivu, wala usijisikie vibaya. Isipokuwa, furahi kwa ajili yao. Mungu aliewafungulia milango wao, atakufungulia na wewe.
Mti wa Muembe hauna hofu endapo mti wa machungwa ukizaa matunda, mti wa muembe unajua fika kwamba msimu huo ni wa machungwa, msimu wake wa kuzaa maembe bado.
Hata wewe rafiki yangu unaenisoma hapa kila siku, msimu wako utakapofika, hakuna kikwazo chochote kitachosimama mbele yako kikakuzuia kufanikiwa.
Simba anaetembea kwa kunyata sio kwamba amechoka au ni dhaifu, ni kwamba anafanya mahesabu ya hatua za kuk**ata windo lake.
Usikasirike, usijisikie k**a umeshindwa na wala usikate tamaa endapo watu wako wa karibu wanafanikiwa na wewe haufanikiwi. Kimbia mbio zako na muamini MUNGU katika uelekeo wako huku ukiwatakia kila la kheri kwa moyo mweupe usio na mawaa wale waliokutangulia!
Ukweli ni kwamba, hali yako ya sasa hivi sio ya kudumu, uelekeo wako ni wenye kuleta tija. Kumbuka, suala sio kujenga nyumba kwa haraka, issue kubwa nyumba hiyo itaweza kuhimili mikiki mikiki ya kimbunga na upepo mkali?
Basi, uwe na moyo wa ujasiri. Tulia uiejenge nyumba yako imara ambayo haitatikisika kamwe!
Endelea kutembea kwa imani, utafanikiwa katika kazi zako za shambani na Mjini, utapona maumivu unayopitia, utaoa/utaolewa na atakayekupenda na you will live happily ever after...God’s time is the best...💯💯
Copied from