29/06/2026
Inasikitisha kuona kwamba kiapo wanachokula viongozi cha kuwahudumia wananchi wote kwa usawa kimegeuzwa kuwa kiapo cha ubaguzi, chuki na uhasama.
Misaada inayotolewa na wafadhili hailengi kuwanufaisha watu wa upande fulani wa kisiasa au familia fulani, bali hulenga kuwafikia wananchi wote wanaohitaji bila ubaguzi.
Hata hivyo, ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya viongozi wakitumia fursa hiyo vibaya kwa kugawa msaada wa chakula uliotolewa na marafiki wetu kutoka Uturuki kwa misingi ya ubaguzi wa kisiasa, kuwatenga baadhi ya vijiji na kuwanyima wananchi wasiounga mkono upande wao wa kisiasa.
Taarifa zimeonyesha kuwa baadhi ya wananchi, hususan kutoka Kipendi na Maroni, waliondolewa kwenye orodha ya wanufaika kwa madai yanayohusishwa na tofauti za kisiasa.
Misaada ya kibinadamu haipaswi kamwe kutumiwa k**a chombo cha siasa. Kila mwananchi anastahili kuheshimiwa, kutendewa haki na kupata huduma bila kujali msimamo wake wa kisiasa. Uongozi wa kweli hujengwa juu ya usawa, haki na kuwahudumia wananchi wote bila ubaguzi.