24/05/2025
💞Kuna tofauti kubwa sana ya “Kuwa na Mtoto” na “Single Mother”, kuwa na mtoto ni ile hali ya mwanamke kuzaa, lakini kuwa Single Mother ni ile hali ya mwanamke, kwanza kuzaa, kuishi na mtoto wake, kumhudumia kwa kila kitu na hata k**a anapata msaada wa mwanaume aliyezaa naye lakini hayuko na huyo mwanaume na anabeba majukumu ya Mama na Baba kwa mtoto wake.
Mwanamke unapokutana na mwanaume, ukamuambia una mtoto akakubali akakuambia kuwa hamna shida labda hata akakuambia kuwa na mimi nina mtoto usichekelee kwanza. Ni lazima ujiulize kuwa kakukuta na mtoto au single mother? Labda nifafanue, unaweza kuwa na mtoto lakini huishi naye, umemuacha kijijini kwa Mama yako, au anaishi na Baba yake. Hapa ni k**a una mtoto lakini kiuhalisia ni k**a vile huna tu ni mwanamke ambaye hajazaa.
Kwamba mwanaume akikukuta katika hali hii anaweza hata kusahau k**a una mtoto, anaweza kuja kwako wakati wowote, mnaweza kutoka wakati wowote bila kuwaza nyumbani au dada wa kazi, anaweza kuamka asubuhi akakuambia twende zandibar, unaweza kutoka kazini ukapitia kwake ukakaa wiki bila kurudi kwako ni simu unampigia tu Mama yako au X wako kuulizia hali ya mtoto.
Lakini single mother, unaishi na mtoto wako, huwezi mleta leta tu mwanaume kizembe zembe kwako, huwezi toka tu ukasafiri wiki na mwanaume, huwezi toka tu kazini ukapitia baa ukarudia kwa mwanaume ukakaa wiki bila kurudi nyumbani. Kila kitu utakachokifanya lazima uangalie mwanao kala, kavaa, anaumwa, ameenda shule, kaoga, yaani unakua Mama.
Hata k**a hamuishi na huyo mwanaume au haji kwako kabisa, lakini zile pilikapilika za umama anaziona, wakati mwingine mnataka kupiga mechi dada wa kazi anapiga simu mtoto anawaka moto mnalazimisha kuacha mechi mnaondoka. Sasa unaona utofauti, mwanaume anapokuambia sijali k**a una mtoto jiulize ni k**a hajali kwakua umezaa au hajali kwakua ni single mother. Usifurahie kichwa kichwa kwani kuna wengine hawajui majukumu.
Unaingia kwenye ndoa akiona pilika pilika za kuwa Mama ananza kuhisi humpendi, anaanza kukuona k**a mchafu flani, anaanza kuhisi kuwa labda mtoto ni kikwazo. Mara anakuambia simtaki mtoto mpeleke kwa Mama yako! Lakini ishu inakuja je wewe unajikubali k**a single mother au mwanamke tu mwenye mtoto? Sijui k**a mmenielewađź•´đź•´đź•´
UCHANGANUZI WA MASUALA NYETI YANAYO FUNGAMANA NA MAISHA MAMBO LEO