Sauti Ya Pwani Fm

Sauti Ya Pwani Fm MOMBASA 94.2 FM || a fully audio-visual Swahili radio station dedicated to serving the coastal region of Kenya and beyond.
(1)

🌍 Leo ni siku ya mazingira! 🌱Tuchukue hatua kulinda nyumba yetu ya pamoja dunia. Panda mti leo, linda mazingira, na tuwe...
10/10/2025

🌍 Leo ni siku ya mazingira! 🌱
Tuchukue hatua kulinda nyumba yetu ya pamoja dunia. Panda mti leo, linda mazingira, na tuweke pwani safi kwa vizazi vijavyo. πŸŒ΄πŸ’§

πŸ“’ Taarifa Rasmi,Mawasiliano Mapya!Wapendwa wasikilizaji, wadau na wateja wetu, tunapopiga hatua katika kuboresha huduma ...
09/10/2025

πŸ“’ Taarifa Rasmi,Mawasiliano Mapya!
Wapendwa wasikilizaji, wadau na wateja wetu, tunapopiga hatua katika kuboresha huduma zetu na mfumo wa kidijitali, Sauti ya Pwani FM inapenda kuwataarifu kuhusu mabadiliko ya mawasiliano rasmi ya kituo chetu. Tafadhali tumia tu mawasiliano yaliyo kwenye tangazo hili unapowasiliana nasi kwa masuala yote ya matangazo, ushirikiano au huduma za kituo.
βœ… Mawasiliano Rasmi:
🌐 www.sautiyapwanifm.co.ke
πŸ“§ [email protected]
πŸ“ Dedan Kimathi Avenue, Mombasa, Kenya
πŸ“ž +254 782 942 666
πŸ“± Mitandao:

Asanteni kwa kuendelea kuwa sehemu ya familia ya Sauti ya Pwani FM 94.2!

09/10/2025

🌍 Kitu kikubwa kinakuja!
We’re taking Sauti ya Pwani FM beyond the airwaves into the digital world! 🎧 New website www.sautiyapwanifm.co.ke will bring you closer to your radio anytime, anywhere.

πŸ“» Sauti ya Pwani FM bado inasikika wazi, 94.2 FM Kwale!
08/10/2025

πŸ“» Sauti ya Pwani FM bado inasikika wazi, 94.2 FM Kwale!

πŸ“» Tuko hewani k**a kawaida, 94.2 FM Mombasa! Kule nyuma ya pazia tunaendelea kuboresha kila kitu kwa ajili yako.
06/10/2025

πŸ“» Tuko hewani k**a kawaida, 94.2 FM Mombasa! Kule nyuma ya pazia tunaendelea kuboresha kila kitu kwa ajili yako.

STANDARD CHARTERED MARATHON YAANDIKISHA REKODI MPYA YA UDHAMINI.Mashindano ya mbio za marathon za Nairobi Standard Chart...
03/10/2025

STANDARD CHARTERED MARATHON YAANDIKISHA REKODI MPYA YA UDHAMINI.

Mashindano ya mbio za marathon za Nairobi Standard Chartered yaandikisha rekodi ya udhamini mkubwa wa zaidi ya shilingi milioni 233.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Oktoba 26, 2025 katika bustani ya Uhuru, Nairobi, na tayari yamevutia washiriki 30,000 kutoka mataifa 92.
Benki ya Standard Chartered imetoa mchango mkubwa wa zaidi ya shilingi milioni 130, huku wadhamini wengine wakiwemo KWAL (Milioni 10), Prudential (milioni 9.5), Anta Sports (milioni 5), EABL (milioni 3.2) na UNDP (milioni 3.2).

SERIKALI YA KAUNTI YA MOMBASA KUTOA TAMKO RASMI KUHUSU MKANGANYIKO UNAOZINGIRA SHUGHLI YA UTOAJI BASARI! SERIKALI ya Kau...
23/09/2025

SERIKALI YA KAUNTI YA MOMBASA KUTOA TAMKO RASMI KUHUSU MKANGANYIKO UNAOZINGIRA SHUGHLI YA UTOAJI BASARI!

SERIKALI ya Kaunti ya Mombasa Kupitia wizara ya Elimu inatarajiwa Kutoa taarifa Kamili Kuhusu sintofahamu inayogubika utoaji wa hundi za Basari Kwa wanafunzi wa Kaunti hiyo.

Akizungumza mnamo siku ya Jumatatu, waziri wa Elimu Kaunti hiyo Dkt. Mbwarali Kame alifichua kwamba Kaunti hiyo sawia na Kaunti nyingine nchini inakumbwa na changamoto ambayo imetatiza pakubwa zoezi la utoaji wa Basari Kwa wanafunzi wa Kaunti hiyo K**a ilivyopangiwa.

Waziri Kame aliwahimiza wazazi, walimu pamoja na wanafunzi kuwa na subira huku Idara yake ya Elimu ikijiandaa Kutoa taarifa Kamili Kuhusu suala hilo mnamo siku ya Jumanne au Jumatano, wiki hii.

"Kumekuwa na wasiwasi mkubwa Kuhusu utoaji wa hundi za Basari Kwa wanafunzi wetu Muhula wa tatu.Ni Kweli hatujaweza Kpeleka Basari Katika shule zilizokusudiwa."

"Tunafahamu kwamba Kumekuwa na malalamishi mengi Kutoka Kwa wazazi wanaotaka kujua mbona serikali ya Kaunti haijatoa hundi hizo za Basari Kwa wanafunzi"

"K**a serikali ya Kaunti tumekumbwa na changamoto k**a Kaunti nyingine kote nchini.Hali hiyo imeathiri pakubwa zoezi na mchakato mzima wa utoaji wa Basari Kwa wanafunzi wetu.

"Ninawahimiza walimu, wazazi pamoja na wanafunzi kuwa na subira. Tutakuwa tunatoa taarifa yetu Kuhusu suala hilo siku ya Jumanne au Jumatano,wiki hii."

Wakati uo huo waziri Kame alisema serikali ya Kaunti ya Mombasa imekamilisha ujenzi wa jengo jipya pamoja na vyoo vya wanafunzi wa shule za chekechea (ECD ) Katika mojawapo ya shule, eneo Bunge la Likoni akiongeza Kwamba Idara yake ya Elimu tayari imefungua rasmi majengo hayo ili yatumika na wanafunzi wa ECD.

"Idara ya Elimu imefungua jengo jipya pamoja na vyoo Katika mojawapo ya shule eneo Bunge la Likoni vitakavyotumiwa na wanafunzi wa Chekechea, ECD."

"Ujenzi K**a huo inatarajiwa Kufanyika Katika shule nyingine Kaunti ya Mombasa."

"Tunatarajia Kufungua Miradi mingine Mingi ambayo ujenzi wake umeanza Katika shule mbali mbali".

Kauli ya waziri huyo inajiri huku Karo ya Muhula wa tatu ikisalia Kuwa Kero Kwa wanafunzi wa Kaunti hiyo hali ambayo huenda ikaathiri pakubwa masomo Yao Muhula watatu.


USAJILI WA STAKABADHI MUHIMU WATAJWA KUWA DONDA SUGU.Usajili wa stakabadhi muhimu limetajwa kuwa kidonda kisichotibika l...
22/09/2025

USAJILI WA STAKABADHI MUHIMU WATAJWA KUWA DONDA SUGU.

Usajili wa stakabadhi muhimu limetajwa kuwa kidonda kisichotibika licha ya Rais Ruto kufutilia mbali vikwazo vya usaili yaani vetting.

Hata hivyo, kwenye kongamano lililowakutanisha wanahabari wa kutoka kaunti za pwani leo, pamoja na wanaharakati limeangazia vigezo muhimu na namna za kutoa msukumo kwa serikali ili kuondoa baadhi ya maswala kadhaa ambayo kulingana na wao yamekuwa kizingiti kikubwa kwa wakazi wa pwani.

Warsha hiyo ya siku mbili, imeandaliwa kwenye hotel moja jijini Mombasa na shirika la Haki Centre ambalo limekuwa katika msitari wa mbele kutetea haki za raia wa Kenya pamoja na wakazi wengine ambao hawajawahi tambuliwa rasmi na serikali na kukosa kupewa uraia.

Kulingana na Andrew Ocholla mratibu mkuu wa miradi ya shirika hilo, serikali imekuwa ikiwapa nafuu wakenya kutumia kushoto na kuwanyanyasa kutumia mkono wa kulia.

Hata hivyo washiriki na wachangizi wa mjadala huo walitoa maoni yao ambayo yatapewa kipaumbele kwenye uwasilishaji wa maombi yao katika mamlaka husika.

Baadhi ya mapendekezo ni; kuhakikisha stakabadhi zote zinafaa kuwekwa kwenye mfumo wa kidijitali kwa kila hatua ya maisha ya raia mkenya kuanzia kuzaliwa hadi upatikanaji wa kitambulisho. Pili, ada ya kupata kitambulisho, cheti cha kuzaliwa baada ya kupotea iondolewe kabisa. Kuongezwe vituo vya usajili n.k "Vyeti vyote kuanzia cheti cha kuzaliwa, kitambulisho na vyeti vingine muhimu vya mzazi sharti viweke kidijitali na mzazi, na pindi mtoto akifikisha umri wa kutuma maombi ya vyeti muhimu anapakua mtandaoni...hii itarahisisha kazi na ucheleweshwaji wa vyeti..."
Alisisitiza mchangiaji mmoja.

Kongamano hili litaendelea kwa siku mbili na linalenga kuhamasisha jamii kuhusu haki zao.

Haki Centre ambalo si geni kwa maswala haya limewahi kusimama kidete na kufaulisha utambulikanaji wa wapemba na wamakonde.


Wakanda 254 Wamjibu Magwaya Ndani ! "Hatujalalamika kutopangwa kwa tamasha, tuna uwezo wa kuandaa Tamasha letu wenyewe j...
18/09/2025

Wakanda 254 Wamjibu Magwaya Ndani ! "Hatujalalamika kutopangwa kwa tamasha, tuna uwezo wa kuandaa Tamasha letu wenyewe jiangalie unapopost vitu vyako."

Shabiki amuandama Mbunge wa Jomvu  Badi Twalib Kisa wasani wa kundi la Wakanda!!"Wape nafasi kwanza wasanii wa Jomvu wan...
15/09/2025

Shabiki amuandama Mbunge wa Jomvu Badi Twalib Kisa wasani wa kundi la Wakanda!!
"Wape nafasi kwanza wasanii wa Jomvu wanaofanya vizuri k**a Wakanda kwenye Shughli na Tamasha za Jomvu!"

^AN

Kelechi Africana yuko tayari kuzichapa na SUSUMILA !! Aomba wadau kujitokeza na kuandaa pambano.  ^AN
15/09/2025

Kelechi Africana yuko tayari kuzichapa na SUSUMILA !! Aomba wadau kujitokeza na kuandaa pambano.

^AN

Niaje Admin Naitwa Husna, Iko hivi! Niko kwenye ndoa mwaka wa  nne sasa nimejaaliwa mtoto mmoja, kiukweli mara ya kwanza...
15/09/2025

Niaje Admin Naitwa Husna, Iko hivi! Niko kwenye ndoa mwaka wa nne sasa nimejaaliwa mtoto mmoja, kiukweli mara ya kwanza kila kitu kilikua sawa ila kuanzia mwaka Jana Mambo yalibadilika, Mume wangu hanishughulikii kabisa, Nimejaribu kumuuliza labda sababu ni nini iliomfanya abadilike hivo hasemi chochote. Nimejaribu kuwahusisha wazazi wake lakini hasikii kabisa. Kiufupi ameshindikana. Natamani anipe talaka yangu ila tatizo hata nikiomba hiyo talaka naanzia wapi? Maana kwetu wazazi washakula mahari ya watu na hawataki kuelewa. Naomba Ushauri kutoka kwa Mashabiki wenu tafadhali.


^AN

Address

Along Dedan Kimathi Avenue
Mombasa
97378-80112

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sauti Ya Pwani Fm posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Sauti Ya Pwani Fm:

Share

Category

Introduction

Sauti ya Pwani FM is a progressive radio station that was established in 2017 with frequencies in Mombasa 94.2FM having coverage in Mombasa, Kilifi and Kwale counties respectively. The core principle of Sauti Ya Pwani FM is based on Culture, Doctrine, Customs and Civilisation of the coastal people.

Sauti Ya Pwani FM seeks to:

Β· Facilitate sustained growth and poverty reduction.