
04/08/2025
SISI NI MABINGWA ❤ 🤍
Twamshukuru Manani, amejibu zetu dua,
Jambo tulolitamani, wengi wetu limekua,
Timu yetu ya moyoni, ubingwa imechukua,
Bumbani mabingwa wenu, heshima wapatieni.
Ubingwa wetu wa kwanza, sote tunajivunia,
Ndio mwanzo tumeanza, mengi tunatarajia,
Mitihani metufunza, kwa yetu hisitoria,
Sisi ni mabingwa wenu, heshima tupatieni.
Ni siku nyingi hakika, asali tulisubiri,
Wapo inzi walicheka, bila ya kutafakari,
Nyuki wetu wanasaka, maua yalonawiri,
Wachezaji wetu bingwa, heshima wapatieni.
Kwanza niwape hongera, hongera tena na tena,
Haya matokeo bora, nje tunayoyaona,
Ni uongozi imara, pamoja na kupambana,
Bodi yetu ni mabingwa, heshima ipatieni.
Mpira wanaocheza, sio wa hapa nchini,
K**a siwa wingereza, basi niwajarumani,
Edward anaweza, mwalimu wa uwanjani,
Kocha karanja ni bingwa, heshima mpatieni.
Kumi na mbili ugani, namba mumetupatia,
Uwepo wetu dimbani, pakubwa umechangia,
Ubingwa kuja nyumbani, tena wa kihistoria,
Mashabiki pia bingwa, heshima tupatieni.
Mwisho ombi kwenu bodi, naomba liwafikie,
Jambo moja maridadi, shabiki mtufanyie,
Tunaiomba paredi, ubingwa tushangilie,
Sisi ni mabingwa wenu, heshima tupatieni.
Mtunzi; Salim Amir
📞 +254 746 053 418