27/05/2026
Maafisa wa Idara ya Upelelezi ya Jinai (DCI) wamemk**ata mshukiwa anayehusishwa na matamshi ya uchochezi yaliyosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, huku maudhui yake yakitajwa kuwa ya kuchochea vurugu na kuhatarisha mshik**ano wa wananchi pamoja na utulivu wa taifa.
Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 33, Evans Onyango Kawala maarufu k**a Kidero Jasuba, alik**atwa katika eneo la Shujaa Mall, Kayole, kufuatia operesheni maalum iliyotekelezwa na maafisa wa Kikosi cha Operations Support Unit (OSU).
Kwa sasa anazuiliwa na anaendelea kufanyiwa taratibu za kisheria kabla ya kufikishwa mahak**ani.
DCI imewaonya wananchi dhidi ya kutoa matamshi ya uchochezi au kusambaza maudhui yanayoweza kuchochea vurugu, kueneza chuki au kuhatarisha amani na umoja wa kitaifa. Idara hiyo imesisitiza kuwa vitendo vya aina hiyo ni makosa makubwa ya jinai, na wahusika watakabiliwa na hatua kali za kisheria kwa mujibu wa sheria.