JAMVI TV

JAMVI TV Habari na vipindi vya Burudani kutoka kwa kituo cha kipekee cha Kiswahili Pwani ya Kenya. Kituo kinachomilikiwa na Jamvi Media Group.

28/05/2026

Katibu wa Chama cha UDA Hassan Omar Sarai matatani! Katibu mkuu wa chama tawala cha UDA Hassan Omar Sarai amejipata matatani baada ya viongozi wa chama hicho kutoka eneo la Mlima Kenya kumtaka ajiuzulu mara moja wadhfa huo kwa hiari la sivyo wamlazimishe kinara wa chama hicho Rais William Ruto kumuondoa uongozini.

26/05/2026

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amemtaka Rais William Ruto kufanya kazi yake ya kuwahudumia wananchi badala ya kuendeleza kampeni za ubaguzi wa kikabila na kisiasa, akionya kwamba uongozi huo unahatarisha mshik**ano wa taifa hasa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 unapokaribia. 𝘜𝘬𝘒𝘯π˜₯𝘒 𝘸𝘒 𝘷π˜ͺπ˜₯𝘦𝘰 𝘬𝘸𝘒 𝘩π˜ͺ𝘴𝘒𝘯π˜ͺ 𝘺𝘒 π˜•π˜›π˜.

24/05/2026

Watetezi wa haki za kibinadamu Pwani sasa wanataka amri ya mahak**a kuhusu kuondolewa kwa vizuizi katika barabara ya kuelekea Kaunti ya Lamu itekelezwe kikamilifu ili mbali na kuimarisha shughuli za uchukuzi katika barabara hiyo vile vile hatua hiyo iifungue Kaunti hiyo kiuchumi.

20/05/2026

Shughuli za uchukuzi zimeregelea hali yake ya kawaida mapema siku ya Jumatano baada ya wadau katika sekta ya uchukuzi wa umma na serikali kuafikiana kusitisha mgomo uliyodumu kwa siku mbili mtawalia. Hata hivyo afueni hiyo ni ya muda wa siku saba pekee, endapo majadiliano hayo hayatafua dafu kufikia siku ya Jumanne juma lijalo, mgomo huo utaanza upya.

18/05/2026

Wahudumu katika sekta ya uchukuzi wa umma, ile ya kibinafsi, wahudumu wa Bodaboda na watetezi wa haki za kibinadamu mapema leo wameandamana katika eneo la Mtwapa Kaunti ya Kilifi wakilalamikia kucheleweshwa kwa ujenzi wa barabara ya Mtwapa-Kwa Kadzengo inayounganisha Kaunti za Mombasa na Kilifi.

08/04/2026

Mbunge wa Nyali na mwaniaji wa Ugavana wa Kaunti ya Mombasa mwaka wa 2027 Mohammed Ali, amemkosoa vikali Gavana wa Kaunti hiyo Abdulswamad Sharif Nassir kwa kuyaondoa mabango yake yaliyolenga kuwahimiza wakaazi wa Kaunti ya Mombasa kujisajili kwa wingi k**a wapiga kura na kujitokeza siku ya uchaguzi mkuu ili kuwachagua viongozi wawajibikaji na waadilifu.

28/02/2026

Mwaniaji wa Ugavana Kaunti ya Mombasa katika kinyang'anyiro cha mwaka wa 2027 Ali Mbogo, amewataka wapinzani wake kujiandaa kwa kivumbi kikali katika uchaguzi huo.

24/02/2026

Changamoto nyingi zinazowasibu vijana Kaunti ya Mombasa na kwengineko Pwani kwa kiwango kikubwa zimechangiwa na wanasiasa. Mwanaharakati wa Vijana na Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Kenya Michael Nato, amewarai wanasiasa kukoma kuwatumia vijana kwa maslahi yao binafsi.

24/02/2026

Mbunge wa Embakasi mashariki Babu Owino amewakosoa vikali maafisa wa polisi kwa kufyatua risasi katika mikutano yake ya kisiasa, akiwataka kukoma mara moja kukiuka sheria. Owino ameyasema hayo alipoitembelea familia ya marehemu Vincent Oyamo aliyeuwawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi kwenye mkutano wa kisiasa wa 'Linda Wananchi' eneo la Kitengela Kaunti ya Kajiado mnamo Februari, 15.

Address

Mombasa
Mombasa
86605-80100

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when JAMVI TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share