14/01/2026
Ujumbe wa Aisha Gaddafi, binti wa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi, kwa wananchi wa Iran
Wananchi jasiri na wasiotetereka wa Iran!
Ninawaonya!
Msidanganywe na maneno matamu na kauli mbiu za mabeberu wa Magharibi.
Hawa ndio wale wale waliomwambia baba yangu: “Ukifunga programu zako za nyuklia na makombora, milango ya dunia itafunguliwa.”
Baba yangu alifungua mlango wa maridhiano kwa nia njema na imani katika mazungumzo;
lakini tulishuhudia jinsi mabomu ya NATO yalivyoigeuza Libya kuwa mavumbi na bahari ya damu,
na jinsi walivyowasukuma wananchi wetu kwenye utumwa, umaskini na uhamisho.
Ndugu zangu wa Iran!
Upinzani wenu, fahari yenu na msimamo wenu dhidi ya vikwazo, uongo wa vyombo vya habari na mashambulizi ya kiuchumi ni dalili za uhai na heshima ya taifa lenu.
Hakuna chochote kinachopatikana kwa kufanya maridhiano na mabeberu zaidi ya uharibifu, migawanyiko na maumivu.
Mazungumzo na mbwa mwitu hayaokoi kondoo — huamua tu ni nani ataliwa next!
Tumeona mataifa yaliyosimama kidete k**a Cuba, Venezuela, Korea Kaskazini (DPRK) na Palestina —
wamesimama mioyoni mwa watu na kuandika historia kwa heshima.
Na pia tumeona wale waliopiga magoti wakitoweka na kubaki majivu.
Kwa upendo na mshik**ano,
Aisha Gaddafi