24/10/2025
🔥 NADIA — PART 11 💞
,🙆♂️💔🙆♂️ Wakati mwingine, ahadi hupimwa si kwa maneno, bali kwa maumivu yanayojaribu moyo uliowahi kuamini.” 💭
Asubuhi ilikua na utulivu wa ajabu. ☀️
Mvua ilikuwa imekoma, anga limejaa mawingu mepesi yanayoelea taratibu, kana kwamba dunia haijui k**a iendelee kutabasamu ama ilie.
Nadia alikuwa amevaa T-shirt yangu, ile nyeupe aliyoinunua siku tulipokutana kwa mara ya pili. Alionekana mrembo — simple but glowing, k**a mtu ambaye amepata amani ya moyo. 💫
Nilimtazama kwa upole, akiwa jikoni akicheka pekee yake huku akijaribu kuandaa kahawa.
Nilihisi moyo ukinicheka ndani… “Huyu ndiye kila kitu changu.”
Me: “Weeh mrembo, hiyo kahawa si utaichoma bana?”
Nadia: (akigeuka, akitabasamu) “Relax babe, najua kufanya. Si kila kitu lazima uogope k**a first date.”
Me: “Sio hofu, ni vile nataka kila kitu ikuwe perfect — k**a wewe.”
Nadia: (akicheka) “Na wewe unajua tu kusema maneno matamu. Umejifunza wapi hivo?”
Me: “Kwa moyo wako, every beat ni somo.” ❤️🔥
Tulicheka, tukanywa kahawa pamoja. Dakika kadhaa baadaye, Nadia alipokea simu — namba ambayo hakuitazama mara ya kwanza.
Alikaa kimya, akaiangalia tena, kisha akatoka nje taratibu.
Nilimsikia akisema kwa sauti ya chini:
> “Sijui bado... tafadhali usiniletee tena hii story, nimechoka…”
Sauti yake ilikuwa na huzuni, mchanganyiko wa hofu na maamuzi magumu.
Nilinyamaza, nikajifanya sijasikia, lakini roho yangu ilitetemeka. 😔
Baadaye, nilimkuta akikaa kitandani, macho yakiwa mbali.
Me: “Nadia, kuna nini?”
Nadia: (akitikisa kichwa) “Nothing serious, Amoro… ni mambo ya zamani tu.”
Me: “Mambo gani? Kuna kitu unaficha?”
Nadia: (kwa sauti ya chini) “Si kila kitu lazima ujue sasa. Kuna vitu nikivisema, vitaharibu utulivu huu mdogo tulionao.”
Nilinyamaza. Nilihisi k**a dunia ilibadilika ghafla — ile hewa safi ya mapenzi ikawa nzito.
Usiku ulifika. 🌙
Nilikaa nikiangalia mvua ndogo ikianza tena, nikisikiliza pumzi yake ikienda taratibu.
Moyo wangu ulihisi wingu lisiloeleweka.
Kisha alfajiri, nilipoamka — chumba kilikuwa kimya.
Kitanda baridi upande wake.
Meza ndogo ilikuwa na karatasi ndogo, iliyoandikwa kwa maandishi yake ya haraka:
Usinilaumu, Amoro. Kuna mambo hayawezi kukimbia kivuli cha jana.
Nilijaribu, lakini dunia yangu ina mzigo usiokuwa wako.
Ukinipenda kweli — nitazame tu nikitembea mbali.” 💔
Nilikaa pale nikiishika karatasi, mvua ikinyesha nje — k**a dunia nayo inalia nami. 🌧️
Nilicheka kwa uchungu kidogo, nikasema kimya kimya:
> “Nadia… niliahidi kukupigania, lakini siwezi kupigana na kivuli usichotaka nikione.”
Nilitazama dirishani, nikiona miale hafifu ya jua ikijaribu kupenya mawingu.
Jua ambalo lilikuwa letu jana — leo likawa shahidi wa upweke wangu. ☀️
🕯️ “Kuna mapenzi ambayo hayafi, lakini yanapotea kwa muda — ili moyo ujifunze kuvumilia maumivu ya kukumbuka.” 💭
🌧️❤️🔥