26/03/2024
Mgombea wa urais wa upinzani nchini Senegal Bassirou Diomaye Faye, ambaye ameshinda uchaguzi wa rais ameahidi kutawala kwa unyenyekevu na uwazi.
Faye, anayetarajiwa kuwa rais ajaye baada ya mpinzani wake mkuu kumpigia simu na kukiri kushindwa, amemshukuru Rais Macky Sall na wagombea wengine kwa kuheshimu utamaduni wa demokrasia wa Senegal kwa kutambua ushindi wake mapema kabisa kabla ya matokeo rasmi kutolewa.
Katika hotuba yake ya kwanza baada ya uchaguzi, Faye amewaambia waandishi habari kuwa katika kumchagua yeye, watu wa Senegal wameamua kuwachana na yaliyopita.
Tume ya uchaguzi imesema matokeo ya awali yalionyesha Faye akiwa na karibu asilimia 53.7 ya kura na Amadou Ba akiwa na asilimia 36.2 kwa kuzingatia hesabu kutoka asilimia 90 ya vituo vya kupigia kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi. Ba na Sall wote walimpongeza Faye, ambaye jana alisherehekea miaka 44 ya kuzaliwa kwake.
Wasiliana nasi 0712686894