26/04/2026
Msanii kutoka Kenya, , ameibua mjadala mtandaoni baada ya kueleza kushangazwa na watu wanaomfuata kwenye DM kuomba msaada, ilhali hawajawahi kuonyesha sapoti kwa kazi zake za muziki.
Akizungumza kwa utani lakini kwa ujumbe mzito, Khaligraph amesema mara nyingi hupokea maombi kutoka kwa watu wanaojitambulisha k**a mashabiki wake, wakidai wanahitaji msaada wa kifedha. Hata hivyo, anachofanya kwanza ni kuchunguza kwenye profile zao ili kuona k**a wamewahi kushare au kupromote nyimbo zake.
Amesema mara nyingi anakuta watu hao wamekuwa wakipost kazi za wasanii wengine k**a Diamond Platnumz na Fally Ipupa, lakini si zake.
Kwa msisitizo, Khaligraph ameweka wazi kuwa haoni mantiki ya kumsaidia mtu ambaye hajawahi ku-support kazi zake, akiwashauri wale wanaopendelea kusapoti wasanii wengine kwenda kuomba msaada kwao pia.
"Mnakuja DM eeh Khaligraph Mimi ni shabiki Yako naomba nisaidie sijala kitu, kitu Cha kwanza Huwa nafanya naangalia profile Yako nione umeshawahi nipost nyimbo yangu kwenye profile Yako? napata umepost wakiona Diamond na Fally Ipupa Itabidi Fally Ipupa wakusaidie
Haiwezekani uje uniombe nikusaidie wakati hujawahi post Ngoma yangu mahala wafate kina diamond na Fally Ipupa" Amesema Khaligraph 😂
Kauli hiyo imezua hisia mseto mtandaoni, huku baadhi wakimuunga mkono kwa kusema sapoti ni kitu cha pande mbili, na wengine wakiona anapaswa kusaidia bila kujali nani anam-support.