
28/03/2025
Wanaume na wanaumess, leo nawaletea story ya vile nilichapwa hadi nikaona my past life na nikasikia sauti ya Pro Max akisema 'Come to me, my child!' 🤣
Sasa ilikuwa hivi...
Nikiwa pale Mundoli pryma, nilikuwa na talanta ya kusneak chuo after second break (break kubwa). Saa hiyo natoka k**a mwizi wa sadaka, natoa shati ya shule, nabaki na tisho na short juu k**a injili lazima uwe umevaa ndani. 🙏
Destination? Kwa Otoyo msale, pale hall ya movie kuwatch DJ Afro. 🎥🔥 Aisee, Afro alikuwa ananipandisha ndege hadi Vietnam, Hong Kong na Washing Tone DC, then anirudishe msale kabla my 5 bob iishe. Hiyo time DJ Afro anasema "Huyu jamaa anatembea k**a nguruwe alikanyaga sindano," na mimi nikiwa hapo nimebana shati kwa kwapa na kucheka k**a nitahepa school fees. 🤣
Timing yangu ilikuwa ya nusu bin nusu ya dondori. 🎯 Movie ikiisha, bell ya shule ya lunch ilikuwa inaring—na hiyo siyo kengele ya mchezo! Ilikuwa rim kubwa ya tractor inagongwa na mtu ako na roho mbaya, yaani ilikuwa inasikika location mzima ungedhani Yesu anarudi kwa round two. 🚜🔔
Sasa najua mnajiuliza hizi 5 bob za movie nilikuwa natoa wapi. 🤔 Well, madhe alikuwa mvugaji wa level ya Chief Poultry Officer. 🐔 Kuku zilikuwa home k**a thate! Nikaanza kugonga deal ya mayai na morio wa mini shop. Yaani biashara ilikuwa inaniingia kuliko CRE ya jioni. 😂💸
Standard procedure ya kuingia bomani:
1. First stop – kwa meko (three stones), nakanyage kwa jivu juu ukifika home ukiwa msafi unatoa ushahidi unnecessary. 🏃♂️🔥
2. Second stop – kabati, kuchungulia k**a uji umeiva ama naingia fasting ya Lazaro.
3.Third stop – k**a food haiko, nitafute mapera (hizi zilikuwa cryptocurrency ya childhood), alafu napitia kwa mabeshte wangu kula huko (shosh yao alikuwa na food program yenye haiku-experience budget cuts). 🍛
Yaani mambo ilikua smooth k**a chupi mpya hadi siku ya nyani kushikwa! 😭
Hiyo siku, miti yote iliteleza. Fence, mablanketi, choo cha shimo hakuna kitu kingeokoa hii mission. Ilikuwa siku ya ndovu kunikula, siku ya shetani kushine, siku ya kufinywa k**a dough ya maandazi. 🍩😩
Sasa ilihappen...
Nikafika shule kutoka lunch, nikapigwa na butwaa mbaya! Yaani nikabaki statue, jicho likiwa na network ya buffering, akili ikicheza slideshow ya mistakes zangu zote. 🤯
Sasa acha kwanza wasee, kuna beshte yangu amenitia form ya keg na mnajua leo ni Friday. Siwezi lalisha! 🍻 Part two nakam nayo kesho wengine waombee viuno visivunjike huko ndani! 🤣