01/03/2026
Putin atoa rambirambi kwa Iran kufuatia ‘mauaji ya kikatili’ ya Khamenei
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ametuma rambirambi kufuatia kuuliwa kwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei, shirika la habari la serikali ya Urusi TASS linaripoti.
Putin amekitaja kifo cha Khamenei kuwa ni “mauaji ya kikatili yaliyokiuka misingi yote ya maadili ya kibinadamu na sheria za kimataifa.”