30/07/2026
ZUCHU ATANGAZA UJAUZITO, DIAMOND PLATNUMZ ATHIBITISHA KUPOKEA MTOTO MPYA
Msanii maarufu wa Bongo Flava, Zuhura Othman Soud, maarufu k**a Zuchu, ameamua kuweka wazi ujauzito wake baada ya muda mrefu wa kuficha.
Leo Julai 30, 2026, Zuchu ameposti picha zake akiwa na nywele za pink na blue rollers, akiwa amevalia gauni jeupe, huku akiwa ameshikilia picha za ultrasound na tumbo lake likiwa wazi. Katika caption yake aliandika, "Growing Love and Eating for Two, pls be a chubby baby."
Taarifa hii inakuja wiki mbili tu baada ya Zuchu kutangaza kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu, msanii Diamond Platnumz. Mnamo Julai 12, Zuchu alikuwa ameandika ujumbe mrefu akisema safari yao ya miaka sita imefikia mwisho na sasa anataka kujikita kwenye afya na kazi yake.
Lakini leo, Diamond mwenyewe ndiye aliyethibitisha taarifa hiyo kwa kuposti picha za Zuchu na kuandika ujumbe uliovuma mitandaoni: "New heart beats in the family."
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya burudani, picha hizo zimepokelewa kwa hisia mchanganyiko. Watu wengi wamewapa hongera, huku wengine wakishangazwa na jinsi habari ya kuachana ilivyokuja wiki chache kabla ya tangazo la ujauzito. Diamond anatajwa kuwa anatarajia mtoto wake wa 5 na mpenzi wa 4 tofauti.
Mpaka sasa, Zuchu hajaweka wazi miezi mingapi ya ujauzito, lakini picha za ultrasound clinic zimeondoa mashaka yote yaliyokuwa yakiendelea kwa muda mrefu.
Zuchu , diamond platnumz