30/07/2025
Mke anasema:
Baada ya kujifungua mtoto wangu wa kwanza, nilikwenda nyumbani kwa wazazi wangu na nikakaa huko kipindi chote cha siku arobaini.
Baada ya kumalizika kwa hizo siku arobaini, mume wangu alinipigia simu siku hiyo hiyo na akaniambia: "Nitakuja kukuchukua, kwa sababu nyumba haina thamani yoyote bila wewe."
Skiliza sauti hii mdundo.com/a/188105
Nikajaribu kumfanya aone k**a sijali sana, na dada zangu wanne ambao hawajaolewa walinishawishi nifanye hivyo. Nikamwambia: "Hapana, sitarudi nyumbani mpaka baada ya wiki mbili zaidi." (Haya yalikuwa ni maneno ya dada zangu na nilikuwa niliyasikiliza na kumuambia mume wangu).
Mume wangu alihuzunika na akajaribu kunishawishi, lakini nilikataa.
Siku iliyofuata alinipigia tena na kuniomba nirudi nyumbani, lakini nilisisitiza msimamo wangu. Baada ya hapo aliniacha, hakuendelea kuwasiliana nami wala kuuliza habari zangu.
Baada ya wiki mbili alikuja na kunichukua kutoka kwa wazazi wangu, akaniambia:
"Nimeoa mke wa pili na nimemweka kwenye sehemu ya juu ya nyumba yetu."
Nikajaribu kuzungumza naye lakini akaniangalia kwa hasira na kunikaripia:
"Ukihitaji kubaki kwa wazazi wako, baki. Na ukihitaji kuondoka nami, njoo twende."
Bila shaka nilichagua kwenda naye ili nimuone huyo mke wake wa pili na nilipize kisasi kibaya kabisa.
Nilipoingia nyumbani kwangu, nilihisi huzuni kali kiasi cha kuhisi k**a nitakufa, nikiwa nasikia harakati zake akipanda na kushuka na sauti ya visigino vyake ambayo ilinichoma masikioni na kuniuwa kwa uchungu.
Mume wangu alianza kupanda kwake mara kwa mara...
Kitu kilichouma moyo wangu zaidi na kufanya damu isimame kwenye mishipa yangu ni sauti ya visigino vyake yaani amevaa na kujipamba masaa 24 kila siku!
Baada ya siku mbili alikuja kwangu na akasema:
“Nimekuja kukuomba radhi. Nilifanya jambo hili kwa hasira na maumivu, kwa sababu nilikupenda sana, lakini ulinidharau na hukujali hisia zangu.”
Akaendelea kusema:
“Wakati nilipokuambia urudi nyumbani, nilikuwa ninahitaji uwepo wako. Lakini uliniambia usubiri wiki mbili zaidi… Sikuweza kuvumilia upweke, huzuni, na baridi ya nyumba bila wewe. Niliamua kumuoa mke wa pili si kwa sababu nilikuwa sitaki wewe, bali kwa sababu nilihisi sina thamani mbele zako.”
Kisha akaangalia chini na kusema:
“Lakini tangu nimwoe, sijahisi furaha. Sijapata utulivu moyoni. Nakuona wewe kila mahali. Hata sauti ya visigino vyake inanichosha, si kwa sababu ya kelele, bali kwa sababu inanifanya nikukumbuke wewe, na nikumbuke kosa langu.”
Moyo wangu ulipasuka kwa huzuni, na kwa mara ya kwanza nilijuta kwa kiburi nilichokionyesha… Nilijuta kwa kusikiliza maneno ya dada zangu badala ya kusikiliza sauti ya upendo wa mume wangu.
Akanishika mkono kwa upole na kusema:
“Nakuomba urudi moyoni mwangu, urudi kuwa malkia wa nyumba hii, na unisaidie kurekebisha yaliyoharibika.”
Nikajua sasa kwamba hasira haizai matunda, na mwanamke mwenye busara hulinda ndoa yake kwa hekima na upendo…
Mwisho wa hadithi: Mwanamke huyu alijifunza somo – kwamba mshauri bora kwa mke ni mume wake mwenyewe, si wale ambao hawajaonja ndoa wala changamoto zake.
Na mume wake – alijifunza kuwa upendo wa kweli ni wa kuvumilia na kuwasiliana, si wa kulipiza kisasi.
🌹Mafunzo:
1.Usisikilize kila sauti – sikiliza moyo wako, na uilinde ndoa yako kwa hekima.
2.Usikubali ushauri wa watu wasiokuwa na uzoefu wa ndoa
Dada zake walikuwa hawajaolewa, lakini walimshawishi kufanya uamuzi wa kiburi ulioharibu ndoa yake. Ndoa ni safari ya wawili; maamuzi yake yanapaswa kutoka kwa hekima, si shinikizo la nje.
2.Mume au mke ni kimbilio la mwenzake si mtu wa kushindana naye
Mume alimwambia “nyumba haina thamani bila wewe,” lakini mke badala ya kushukuru, alijifanya mgumu. Kiburi kwenye ndoa huvunja moyo wa mwenzako na kuharibu uhusiano.
3.Hasira huzaa maamuzi ya kujutia
Mume alimuoa mke wa pili kwa hasira na kujitoa kisasi, lakini baada ya muda alijuta. Vivyo hivyo mke alijutia kiburi chake. Uamuzi wowote wa hasira huzaa majuto.
4.Ndoa inahitaji mawasiliano ya wazi na huruma
Badala ya kushindana au kunyamaziana, wanandoa wanapaswa kuzungumza, kueleza hisia zao, na kusameheana. Ukimya na visasi hufanya ndoa kufa kwa taratibu.
5.Mwanamke mwenye busara hujenga nyumba yake kwa upendo, si kwa chuki
Mwisho wa hadithi, mke alijifunza kwamba kulinda ndoa yake kwa hekima na kujishusha ni bora kuliko kulipiza kisasi. Ndoa imara hujengwa na uvumilivu, si ushindi wa kihisia.
Endelea kufuatilia ukurasa wangu wa Darly G Kenya ili Ujifunze mengi zaidi
Share ujumbe huu na wengine wajifunze, like na comment ili uwafikie wengi zaidi
Allah atupe subra katika ndoa zetu🤲🙏