Kambi Ya Wateule

Kambi Ya Wateule Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Kambi Ya Wateule, Digital creator, N/A, Nakuru.

Bwana Yesu Kristo asifiwe na karibu sana kwenye hii group,lengo kuu likiwa ni tujifunze Neno La Mungu litupe nuru maishani mwetu ,maarifa na hekima ya Mungu,kuimarisha uhusiano wetu na Mungu kupitia maombezi ,maombi na sadaka zetu [+254]0792593648 .

Marko 4:18-20 Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba; ni watu walisikiao lile neno,na shughuli za dunia, na udanganyifu...
17/09/2025

Marko 4:18-20 Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba; ni watu walisikiao lile neno,na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai.Na hawa ndio waliopandwa penye udongo ulio mzuri; ni watu walisikiao lile neno na kulipokea, na kuzaa matunda, mmoja thelathini, mmoja sitini, na mmoja mia.Halleluyah na habari ya sasa hivi mtu wa Mungu, leo biblia inatukumbusha kwamba Neno la Mungu si la kusikia tu, bali ni la kutenda.Kila mmoja wetu anaweza kuzaa matunda kwa kiwango kikubwa tukimruhusu Mungu alime udongo wa mioyo yetu.halleluyah na kuwa na siku ya baraka. 👇

Mark 4:18-20 The seed that fell among the thorns represents others who hear God’s word, 19 but all too quickly the message is crowded out by the worries of t...

1 Wathesalonike 2:13 Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la...
16/09/2025

1 Wathesalonike 2:13 Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si k**a neno la wanadamu, bali k**a neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.Halleluyah mtu wa Mungu popote pale ulipo, Bwana Yesu Kristo asifiwe na habari ya sasa hivi, leo biblia inatufundisha kwamba tulipokee Neno la Mungu si k**a Neno la wanadamu ,bali k**a neno la Mungu na hapo ndipo tutaanza kuona utofauti kwenye maisha Yetu Hallelujah na kuwa na siku ya baraka. 👇👇

1 Thessalonians 2:13 Therefore, we never stop thanking God that when you received his message from us, you didn’t think of our words as mere human ideas. You...

Yohana 15:3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.Halleluyah ,Bwana Yesu Kristo asifiwe mtu wa...
15/09/2025

Yohana 15:3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.Halleluyah ,Bwana Yesu Kristo asifiwe mtu wa Mungu na Habari ya sasa hivi, leo biblia inatukumbusha kwamba Neno la Mungu ni k**a maji safi—siyo matope. K**a halikufanyi uwe bora zaidi, msafi zaidi, au mwenye nguvu zaidi, basi huenda si Neno lake hata kidogo.Halleluyah ruhusu neno la Mungu likusafishe na kuwa na wiki ya baraka. 👇👇

Ephesians 5:25-27 For husbands, this means love your wives, just as Christ loved the church. He gave up his life for her 26 to make her holy and clean, washe...

Zaburi 138:8 BWANA atanitimilizia mambo yangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.hallel...
13/09/2025

Zaburi 138:8 BWANA atanitimilizia mambo yangu;
Ee BWANA, fadhili zako ni za milele;
Usiziache kazi za mikono yako.halleluyah ,Bwana Yesu Kristo asifiwe na habari ya sasa ,Mstari huu unatuhakikishia kwamba maisha yetu si ya kubahatisha bali ni sehemu ya mpango wa makusudi ya Mungu, ambao Amejitoa kuutimiza.halleluyah na kuwa na wikendi ya baraka. 👇👇

Psalm 138:8, NLT The LORD will work out his plans for my life—for your faithful love, O LORD, endures forever. ...

2 Wakorintho 5:7 Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.Halleluyah mtu wa Mungu ,Bwana Yesu Kristo asifiwe na habari ya...
12/09/2025

2 Wakorintho 5:7 Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.Halleluyah mtu wa Mungu ,Bwana Yesu Kristo asifiwe na habari ya sasa hivi, leo biblia inatufundisha kwamba Imani siyo upofu—ni kuona kwa macho ya Roho,inamaanisha imani inashikilia ahadi ya kesho na kuishi kana kwamba tayari imetimizwa.mpendwa, ni changamoto gani unayokabiliana nayo leo? Ni ugonjwa? Shida za kifedha? Au uhusiano uliovunjika? Kumbuka: si lazima uone suluhisho ndipo uamini. Mungu tayari anafanya kazi nyuma ya pazia.Halleluyah na kuwa na siku ya baraka.
👇👇

2 Corinthians 5:7 For we live by believing and not by seeing. #...

Waefeso 1:13 Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwam...
11/09/2025

Waefeso 1:13 Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.Halleluyah mtu wa Mungu, Bwana Yesu Kristo asifiwe na habari ya sasa hivi, leo biblia inatufundisha kuwa tumetiwa muhuri na Roho Mtakatifu – alama ya umiliki, ulinzi na urithi wa Mungu. Tayari tumekubalika, tumetengwa na kupewa nguvu kwa ajili ya utukufu.halleluyah na kuwa na siku ya baraka. 👇👇

Ephesians 1:13 And now you Gentiles have also heard the truth, the Good News that God saves you. And when you believed in Christ, he identified you as his ow...

Zaburi 34:15 Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao.halleluyah mtu wa Mungu popote ...
10/09/2025

Zaburi 34:15 Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao.halleluyah mtu wa Mungu popote pale ulipo, Bwana Yesu Kristo asifiwe na habari ya sasa hivi, leo neno la Mungu linatukumbusha kwamba Hakuna kitu kinachompita Mungu kuhusu maisha yako. Anaona hata yale usiyoyasema, anajua mawazo yako ya moyoni na hata kilio cha ndani kisicho na maneno. Yeye hujali na yuko tayari kujionyesha kwako k**a mwenye upendo, neema na rehema.halleluyah na kuwa na siku ya baraka. 👇

Psalm 34:15 The eyes of the Lord watch over those who do right;his ears are open to their cries for help. ...

Marko 10:35–38 Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu na kusema:“Mwalimu, tunataka utufanyie jambo moja.”Y...
09/09/2025

Marko 10:35–38 Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu na kusema:
“Mwalimu, tunataka utufanyie jambo moja.”
Yesu akawauliza, “Mnataka niwafanyie nini?”
Wakajibu, “Utujalie kukaa, mmoja mkono wako wa kuume na mmoja mkono wako wa kushoto, katika utukufu wako.”Lakini Yesu akawaambia, “Hamjui mnaloliomba! Je, mwaweza kunywea kikombe nitakachokinywea mimi, au kubatizwa kwa ubatizo nitakaobatizwa nao mimi?” hallelujah mtu wa Mungu, Bwana Yesu Kristo asifiwe na habari ya sasa hivi, leo biblia inatufundisha kuwa Kabla ya kumwomba Mungu akufanye mkuu, au akutumie kwa njia ya ajabu, chukua muda ujiulize, “Je, kweli ninaelewa ninachoomba?” Je, uko tayari kwa ukuaji, mchakato, na unyenyekevu unaohitajika kubeba kile unachokiombea? Hallelujah na kuwa na siku ya baraka. 👇 👇

Mark 10:35–38 (NLT): Then James and John, the sons of Zebedee, came over and spoke to him. “Teacher,” they said, “we want you to do us a favor.” “What is you...

Mwanzo 41:33 Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri.Halleluyah mtu wa Mungu popote...
08/09/2025

Mwanzo 41:33 Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri.Halleluyah mtu wa Mungu popote pale ulipo, Bwana Yesu Kristo asifiwe na habari ya sasa hivi, leo biblia inatukumbusha kwamba Huhitaji kupiga kelele ili uonekane, Mungu anakuaona.Huhitaji kushindana ili kuchaguliwa, Mungu analijua jina lako. Kwa hiyo, kaa mnyenyekevu, tumikia vizuri, na umwamini Mungu kufungua milango sahihi kwa wakati wake.Halleluyah ,kuwa na wiki na siku ya baraka . 👇👇

Genesis 41:33 “Therefore, Pharaoh should find an intelligent and wise man and put him in charge of the entire land of Egypt. ...

Mwanzo 22:17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako k**a nyota za mbinguni, na k**a mc...
07/09/2025

Mwanzo 22:17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako k**a nyota za mbinguni, na k**a mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;Hallelujah mtu wa Mungu, Bwana Yesu Kristo asifiwe na habari ya sasa hivi, leo Biblia inatukumbusha kwamba K**a uzao wa Abrahamu katika Kristo, tunaitwa kumiliki milango ya maadui zetu. Tuwe wajasiri, tuwe na uthabiti, na tutumie mamlaka tuliyopewa kwa jina la Yesu.halleluyah na kuwa na siku ya baraka. 👇

Genesis 22:17 I will certainly bless you. I will multiply your descendants[a] beyond number, like the stars in the sky and the sand on the seashore. Your des...

Yuda 1:20 Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,Hallelu...
05/09/2025

Yuda 1:20 Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,Hallelujah mtu wa Mungu,Bwana Yesu Kristo asifiwe na Habari ya sasa hivi ,leo biblia inatukumbusha kwamba tuendeleeni kulisha imani yetu kwa Neno la Mungu, kuitia kazini kwa matendo, na kuomba katika Roho Mtakatifu. Moto wa imani yako usiwahi kuzima. Kila siku jengeka juu ya imani yako takatifu, kwa maana imani yako ndiyo ushindi wako!Hallelujah na kuwa na siku ya baraka. 👇👇

Jude 1: 20But you, dear friends, must build each other up in your most holy faith, pray in the power of the Holy Spirit,WhatsApp---https://chat.whatsapp.com/...

Mwanzo 25:22 Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza BWA...
04/09/2025

Mwanzo 25:22 Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza BWANA.Halleluyah ,Bwana Yesu Kristo asifiwe mtu wa Mungu na Habari ya sasa, leo biblia inatukumbusha kwamba Wakati jambo fulani maishani mwako halihisi kuwa sawa—hisia zako, masomo yako, mahusiano yako—mwendee Mungu na uulize, “Bwana, hili ni nini?”Anataka kusema nawe.Anataka kukufafanulia mambo.Usishi kwa kukisia.Usitembee gizani kupitia hali zako.Nidhamu ya kuuliza ni sehemu ya ukomavu wa kiroho.Halleluyah na kuwa na siku ya baraka 👇 👇

Genesis 25:22 (NLT): "But the two children struggled with each other in her womb. So she went to ask the Lord about it. ‘Why is this happening to me?’ she as...

Address

N/A
Nakuru
N/A

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kambi Ya Wateule posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kambi Ya Wateule:

Share