Masomo ya Misa ya kila siku

  • Home
  • Masomo ya Misa ya kila siku

Masomo ya Misa ya kila siku This is a religious page that enables you to find daily Mass readings. Welcome all and God bless you. Spiritual counselor and Coach.

Motivation and spiritual Career Advisor.

03/10/2026

MASOMO YA MISA, OKTOBA 4, 2026
DOMINIKA YA 27 YA MWAKA

MWANZO:
Est. 13:9, 10-11
Ee Bwana ulimwengu wote u katika uweza wako, wala hakuna awezaye kukupinga ukipenda. Wewe umeumba yote, mbingu na nchi na vitu vyote vya ajabu vilivyomo chini ya mbingu; ndiwe Bwana wa yote.
________

SOMO 1
Isa. 5:1-7

Na nimwimbie mpenzi wangu wimbo wa mpenzi wangu katika habari za shamba lake la mizabibu. Mpenzi wangu alikuwa na shamba la mizabibu, Kilimani penye kuzaa sana; Akafanya handaki kulizunguka pande zote, Akatoa mawe yake, Akapanda ndani yake mzabibu ulio mzuri, Akajenga mnara katikati yake, Akachimba shinikizo ndani yake; Akatumaini ya kuwa utazaa zabibu, Nao ukazaa zabibu-mwitu.

Na sasa, enyi wenyeji wa Yerusalemu, nanyi walio wa Yuda, amueni, nawasihi, kati ya mimi na shamba langu la mizabibu. Je! Ni kazi gani iliyoweza kutendeka ndani ya shamba langu la mizabibu nisiyoitenda? Basi, nilipotumaini ya kuwa litazaa zabibu, mbona lilizaa zabibu-mwitu? Haya basi, sasa nitawaambieni nitakalolitenda shamba langu la mizabibu; nitaondoa kitalu chake, nalo litaliwa; nitabomoa ukuta wake, nalo litakanyagwa; nami nitaliharibu, wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinye mvua juu yake. Kwa maana shamba la mizabibu la Bwana wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
________

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 80:8, 11-15, 18-19, (K) Isa. 5:7

(K) Shamba la mizabibu la Bwana, ndilo nyumba ya Israeli.

Ulileta mzabibu kutoka Misri,
Ukawafukuza mataifa ukaupanda.
Nao uliyaeneza matawi yake hata baharini,
Na vichipukizi vyake hata kunako mto. (K)

Kwa nini umezibomoa kuta zake,
Wakuchuma wote wapitao njiani?
Nguruwe wa msituni wanauharibu,
Na hayawani wa kondeni wanautafuna. (K)

Ee Mungu wa majeshi, tunakusihi, urudi,
Utazame toka juu uone, uujilie mzabibu huu,
Na mche ule ulioupanda,
Kwa mkono wako wa kuume. (K)

Basi hatutakuacha kwa kurudi nyuma;
Utuhuishe nasi tutaliitia jina lako.
Ee Bwana, Mungu wa majeshi, uturudishe,
Uangazishe uso wako nasi tutaokoka. (K)
________

SOMO 2
Flp. 4:6-9

Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya staha, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo. Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
________

SHANGILIO
Yn. 10:27

Aleluya, aleluya!
Kondoo wangu waisikia sauti yangu, asema Bwana; Nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
________

INJILI
Mt. 21:33-43

Yesu aliwaambia wakuu wa makuhani na wazee wa watu, Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake. Wale wakulima wakawak**ata watumwa wake, huyu wakampigam na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe. Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza, wakawatenda vile vile. Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu. Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. Wakamk**ata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima? Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake. Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?

Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa linguine lenye kuzaa matunda yake.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo

03/10/2026

MASOMO YA MISA
JUMAMOSI, OKTOBA 03, 2026
JUMA LA 26 LA MWAKA

SOMO 1
Ayu. 42:1 – 3, 5 – 6, 12 – 17

Ayubu alimjibu Bwana na kusema, najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, nay a kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika. Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, mambo ya ajabu, ya kunishinda mimi, nisiyoyajua. Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; bali sasa jicho langu linakuona. Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu katika mavumbi na majivu.

Basi hivyo Bwana akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo kumi nan ne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng’ombe elfu, na punda wake elfu. Tena laikuwa na wana waume saba, nab inti watatu. Akamwita huyo wa kwanza jina lake Yemima; na wa pili akamwita jina lake Kesia; na wa tatu akamwita jina lake Keren-hapuhu. Katika nchi hiyo yote hawakuwapo wanawake waliokuwa wazuri k**a hao wana wa Ayubu; na baba yao akawapa urithi kati ya ndugu zao wana waume. Kisha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia na arobaini, naye akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hata vizazi vine. Basi Ayubu akafa, mzee sana mwenye kujawa na siku.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 119:66, 71, 75, 91, 125, 130 (K) 135

(K) Umwangazie mtumishi wako uso wako, Ee Bwana.

Unifundishe akili na maarifa,
Maana nimeyaamini maagizo yako.
Ilikuwa vema kwangu kuwa naliteswa,
Nipate kujifunza mari zako. (K)

Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki,
Ee Bwana, na kwa uaminifu umenitesa.
Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo,
Maana vitu vyote ni watumishi wako. (K)

Mimi ni mtumishi wako, unifahamishe,
Nipate kuzijua shuhuda zako.
Kufananisha maneno yako kwatia nuru,
Na kumfahamisha mjinga. (K)

SHANGILIO
Yn. 15:15

Aleluya, aleluya,
Bwana anasema: Siwaiti tena watumwa, lakini ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu, nimewaarifu.
Aleluya.

INJILI
Lk. 10:17-24

Wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni k**a umeme. Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.

Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza. Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.

Akawageukia wanafunzi wake, akasema nao kwa faragha, Heri macho yaonayo mnayoyaona ninyi. Kwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

21/09/2026

Celebrating my 4th year on Facebook. Thank you for your continuing support. I could never have made it without you. 🙏🤗🎉

13/09/2026

MASOMO YA MISA, JUMAPILI, SEPTEMBA 13, 2026
JUMA LA 24 LA MWAKA

MWANZO
YbS 36:15.16

Ee Bwana, uwape amani wakungojao, ili watu wawasadiki manabii wako; usikilize sala ya mtumwa wako, na ya taifa lako Israeli.

SOMO I
YbS 27:30-28:1-7

Hasira na ghadhabu, haya pia ni machukuzo na aliye mwenye dhambi yatampata. Mwenye kujilipiza kisasi ataona kisasi kutoka kwa Bwana; hakika Yeye atamfungia dhambi zake. Umsamehe jirani yako dhara alilokufanyia, hivyo nawe utasamehewa dhambi zako wakati utakaposali. Mwanadamu humkasirikia mwanadamu, je! atatafuta kuponywa na Bwana? Hamrehemu mwanadamu aliye mwenzake, je! atalalamika kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe? Aliye mwili na damu tu huilisha hasira yake, je! ni nani atakayempatanisha yeye kwa makosa yake? Basi kumbuka mwisho wako, uuache uadui; kumbuka uozi na mauti , ujiepushe na kutenda dhambi. Kumbuka zile amri, usikasirike na jirani yako; nawe ulikumbuke agano lake Aliye juu, umwachilie ujinga wake.

Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 103:1-4, 9-12

(K) Bwana amejaa huruma na neema,
si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa fadhili.

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Naam, vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi jina lake takatifu.
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Wala usizisahau fadhili zake zote. (K)

Ndiye anayekusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote.
Akomboa uhai wako na kaburi,
Akutia taji ya fadhili na rehema. (K)

Yeye hatateta siku zote,
Wala hatashika hasira yake milele.
Hatutendei kadiri ya hatia zetu,
Wala halipi kwa kadiri ya maovu yetu. (K)

Maana vile mbingu zilivyoinuka juu ya nchi,
Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao.
K**a mashariki ilivyo mbali ma magharibi,
Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. (K)

SOMO 2
Rum. 14:7-9

Hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake. Kwa maana k**a tukiishi, twaishi kwa Bwana, au k**a tukifa, twafa kwa Bwana. Basi k**a tukiishi au k**a tukifa, tu mali ya Bwana. Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.

Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu

SHANGILIO
Yn. 13:34

Aleluya, aleluya,
Amri mpya nawapa, asema Bwana,
mpendane, k**a vile nilivyowapenda ninyi.
Aleluya.

INJILI
Mt. 18:21-35

Petro alimwendea Yesu akamwambia, Bwana ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? hata mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.

Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi. Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, akalipwe ile deni. Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia; akamk**ata, akamshika koo, akisema, Nilipe uwiwacho. Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa deni. Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; nawe, je! haikukupasa kumrehemu mjoli wako, k**a mimi nilivyokurehemu wewe? Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote. Ndiyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

11/09/2026

MASOMO YA MISA
JUMAMOSI, SEPTEMBA 12, 2026
JUMA LA 23 LA MWAKA

KUMBUKUMBU YA JUMAMOSI YA BIKIRA MARIA

SOMO 1
1Kor. 10:14 – 22

Wapenzi wangu, ikimbeni ibada ya sanamu. Nasema k**a na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. Kikombe kile cha Baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. Waangalieni hao waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu?

Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilicholewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 116:12 – 13, 17 – 18 (K) 17

(K) Nitakutolea dhabihu ya kushukuru, Ee Bwana.

Nimrudishie Bwana nini
Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
Nitakipokea kikombe cha wokovu;
Na kulitangaza jina la Bwana. (K)

Nitalitangaza jina la Bwana;
Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana,
Naam, mbele ya watu wake wote.
Katika nyua za nyumba ya Bwana,
Ndani yako, Ee Yerusalemu. (K)

SHANGILIO
Yn. 8:12

Aleluya, aleluya,
Mimi ndimi nuru ya ulimwengu,
asema Bwana, yeye anifuataye
hatakwenda gizani kamwe,
bali atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.

INJILI
Lk. 6:43 – 49

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.

Na kwa nini mnaniita, Bwana, walakini hamtendi nisemayo?

Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri. Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba yakawa makubwa.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

05/09/2026

MASOMO YA MISA
JUMAMOSI, SEPTEMBA 5, 2026
JUMA LA 22 LA MWAKA

SOMO 1
1Kor. 4:6 – 15

Ndugu zangu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe. Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea? Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Naam, laity mngemiliki, ili sisi nasi tumiliki pamoja nanyi! Maana nadhani ya kuwa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho, k**a watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia; kwa malaika na wanadamu.

Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye akili katika Kristo; sisi tu dhaifu, lakini ninyi mna nguvu; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima. Hata saa hii ya sasa, tuna njaa na kiu, tu uchi, twapigwa ngumi, tena hatuna makao; kasha twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twastahimili; tukisingiziwa twasihi; tumefanywa k**a takataka za dunia, na tama ya vitu vyote hata sasa.

Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuwaonya k**a watoto niwapendao. Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 145:17 – 21 (K0 18

(K) Bwana yu karibu na wote wamwitao.

Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote,
Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.
Bwana yu karibu na wote wamwitao,
Wote wamwitao kwa uaminifu. (K)

Atawafanyia wamchao matakwa yao,
Nay atakisikia kilio chao na kuwaokoa.
Bwana huwahifadhi wote wammpendao,
Na wote wasio haki atawaangamiza. (K)

Kinywa change kitazinena sifa za Bwana;
Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu
Milele na milele. (K)

SHANGILIO
Zab. 119:18

Aleluya, aleluya,
Unifumbue macho yangu niyatazame
maajabu yatokayo katika sharia yako.
Aleluya.

INJILI
Lk. 6:1 – 5

Ilikuwa siku ya sabato moja Yesu alikuwa akipita katika mashamba, wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke na kuyala, wakiyapukusa-pukusa mikononi mwao. Basi baadhi ya Mafarisayo wakawaambia, Mbona mnafanya lisilo halali siku ya sabato? Yesu akawajibu akawaambia, Hamkulisoma, hata hilo alilolifanya Daudi, alipokuwa na njaa, nay eye na wale aliokuwa nao? Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaitwaa mikate ile ya Wonyesho, akaila akawapa na hao wenziwe, ambayo si halali kuila ila kwa makuhani peke yao. Akawaambia, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

29/08/2026

MASOMO YA MISA,
JUMAPILI, AGOSTI 30, 2026
JUMA LA 22 LA MWAKA
________

MWANZO
Zab. 86:3, 5

Ee Bwana, unifadhili maana nakulilia wewe mchana kutwa. Kwa maana wewe, Bwana, u mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitao.
________

SOMO I
Jer. 20:7-9

Ee Bwana, umenihadaa, nami nimehadaika; wewe una nguvu kuliko mimi, ukashinda; nimekuwa kitu cha kuchekesha, mchana kutwa; kila mtu hunidhihaki. Maana kila ninenapo napiga kelele; nalia, Dhuluma na uharibifu! Kwa kuwa neno la Bwana limefanywa shutumu kwangu, na dhihaka, mchana kutwa. Nami nikisema, Sitamtaja wala sitasema tena kwa jina lake; ndipo moyoni mwangu kumekuwamo k**a moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia.

Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu
________

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 63:1-5, 7-8 (K) 1

(K) Ee Bwana, Mungu wangu, nafsi yangu inakuonea kiu.

Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,
Nafsi yangu inakuonea kiu.
Mwili wangu wakuonea shauku,
Katika nchi kame na chovu, isiyo na maji. (K)

Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu,
Nizione nguvu zako na utukufu wako.
Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai,
Midomo yangu itakusifu. (K)

Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai,
Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
Nafsi yangu itakinai k**a kushiba mafuta na vinono,
Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha. (K)

Maana Wewe umekuwa msaada wangu,
Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.
Nafsi yangu imekuandama sana,
Mkono wako wa kuume unanitegemeza. (K)
________

SOMO 2
Rum 12: 1-2

Basi ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu
________

SHANGILIO
Lk 21: 36

Aleluya, aleluya,
Kesheni kila wakati, ili mpate kuokoka,
na kusimama mbele ya Mwana wa Adamu.
Aleluya
________

INJILI
Mt 16:21-27

Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema. Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. Akageuka, akamwambia Petro, nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.

Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

29/08/2026

*SOMANUTIKAP MISA NE TILIL NEPO JUMAPILI, TARIKIT 30/08/2026*

*JUMAPILITAP TIPTEM AK AENG' NEPO KENYITAP A NEPO KANISA*

*NGORYEETAP MISA: NE NYALIL 💚*
*YAUTIK CHEBO ROSARI 📿: CHEPO KALASUNET*

*SOMANET NE TAI*
*JEREMIAH 20: 7-9*

*_Somanet ne tai koyob kitabutap Maotyot Jeremiah_*

Ee Cheptalel, ki iberbera, ak ki aberberage: ii kiim isiira, ak ki iterteerisye: kaaegu ne kirorechin peetuut komugul, churochura age tugul. Amu kotugul ye ang'alaali, awaache; awaache ale, Koroomnateet ak luuleet: amu kagiyai ng'olyootap Kamuktaindet ne Toroor koek chotisyet eng' anee, ak aegu ne kirorechin eng' peetuut komugul. Ak ngot amwa ale, Ma mwaei kiy agobo ineendet, anan ang'alaal eng' kainennyi, kobiit anyun eng' muguleldanyu ko uu maat ne lalei eng' kawekyuk, ak ang'et eng' muitaet, ak ma muuchi asiis.

_*Ng'olyotab Cheptalel: Kiwekyini Cheptalel kongoi*_

*TYENDAP KALASUNET*
*TYENWOGIKAP KALASUNET 63: 2, 3-4, 5-6, 8-9 (W. 8bc)*

*WOLUNET: _Ee Cheptalel, iboorwech rireeneng'ung', ak igoonech yetuneng'ung'_*

Ee Kamuktaindet, inyee ko ii Kamuktaindennyu;
acheeng'in eng' kagiiletapkei;
Amei melelda saboondanyu amu machin, machin kot poortanyu

*WOLUNET: _Ee Cheptalel, iboorwech rireeneng'ung', ak igoonech yetuneng'ung'_*

Eng' emet ne yaamaat ne po ng'etatet, ole ma mi peek.
Ara uu nooto koageerin eng' ole-tiliil, si ageer kimnateng'ung' ak toroornateng'ung'.
Amu myee chamyeng'ung' ne tala kosiir saboondo;
ilasun anyun kutinnyu.

*WOLUNET: _Ee Cheptalel, iboorwech rireeneng'ung', ak igoonech yetuneng'ung'_*

amu ki iegu toretindennyu, abaibai anyun eng' urwetap kebebaiguk.
Isubotin saboondanyu miising';
nama eung'ung' ne po tai.

*WOLUNET: _Ee Cheptalel, iboorwech rireeneng'ung', ak igoonech yetuneng'ung'_*

*SOMANETAP AENG'*
*ROMANIK 12: 1-2*

*_Somanetap aeng' koyob baruetab koyoktoindet Paulo ne kisirjin Romanik_*

Nooto anyun che kitupche, asoomok miising', eng' rireenosyegap Kamuktaindet ale, ogoite poorwekwok koek tiseiywot ne sabei, ne tiliil, ne taachaksei eng' Kamuktaindet, nooto ko poisyeng'wong' ne nyolu. Amoyaniegei ateptap peetuusyechu: ago ingewalak eng' kaleelitetap kabwaatutikwok, si kobiit onai komyee mageet ne myee ne po Kamuktaindet, ne tachaksei ak kogesunotkei.

_*Ng'olyotab Cheptalel: Kiwekyini Cheptalel kongoi*_

*KATORORETAP LOGOIYWEK CHE MYACH*
*EPESOEK 1: 17-18*

_*Aleluya! Aleluya!*_

Ingogoonech Kamuktaindet ne po Kiptaiyandennyo Jeso Kristo, kokweng'ogis konyegap mugulelwekyok si kobiit kenai kiit ne uu k**ang'unetap kuursennyi

_*Aleluya! Aleluya!*_

✝️ *INJILI* 📖
*MATAYO 16: 21-27*

Logoiywek che myach kouu ye kisir Matayo ne Tiliil: Ilosunot ee Kiptaiyat

Kobooch yooto anyun, kotoi Jeso koboorchi kasubikyik kole wendi ineendet Jerusalem, ak nyooru kanyaliilet ne oo eng' eunegap poisyek, tisiik che eecheen ak siriik, ak kebar, ak eng' peetuutap somok, king'eet. Ki nam Petero ineendet komut taban ak kotoi koger kong' koleen, “Achicha Kiptaiyat! Ma nyoonjin niito agoi.” Ago kiweleljigei ak koleenji Petero, “Istoenongei, Setani! Ii kanagut eng' anee; amu ma ibwaati inyee tuguugap Kamuktaindet, ago ibwaati che po kipkosabei.”
Kingo pata koleenji Jeso kasubikyik, “Ngo machei chii kosubwo, ko nyolu koeesyogei, ak kosut koip kimurtoiyondennyi, ak kosubwo. Amu age tugul ne machei kosar saboondanyi, kobeeti, ak age tugul ne ibeeti saboondanyi agobo anee, konyooru. Keljino nee ne nyooru chii, ngo nyoor ng'wony komugul, ak kobeet saboondanyi? Anan tos igoito nee chii kowale saboondanyi? Tuun nyoonei Weeriitap chii eng' liilindap Kwandanyi kobooto malaikaisyekyik, ak kogoochi chii age tugul ko uu poisyonikyik. ”

Logoiywek che myach chebo Cheptalel: Neng'ung'et katororet ee Kristo

26/08/2026

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Stellah Jerop, Nancy Mamake Noly, Jecinta Cheruiyot, Kangwana Jeremiah, Catchy Cathy, Essy Faizer, Blessed Mike, Busienei Ruth, Jacinta Kukat

26/08/2026

MASOMO YA MISA, JUMATANO, AGOSTI 26, 2026
JUMA LA 21 LA MWAKA
________
SOMO I
2 The 3: 6-10, 16-18

Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.

Mwajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata; kwa sababu hatukuenda bila utaratibu kwenu; wala hatukula chakula kwa mtu ye yote bure; bali kwa taabu na masumbufu, usiku na mchana tulitenda kazi, ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote. Si kwamba hatuna amri, lakini makusudi tufanye nafsi zetu kuwa kielelezo kwenu, mtufuate.

Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.

Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.

Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila waraka, ndio mwandiko wangu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote.

Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu
________
WIMBO WA KATIKATI
Zab 128: 1-2, 4-5 (K) 1

(K) Heri kila mtu amchaye Bwana.

Taabu ya mikono yake hakika utaila;
Utakuwa heri, na kwako kwema.
Mkeo atakuwa k**a mzabibu uzaao,
Vyumbani mwa nyumba yako. (K)

Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana.
Bwana akubariki toka Sayuni,
Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako. (K)
________
SHANGILIO
Yn 10: 27

Aleluya, aleluya,
Kondoo wangu waisikia sauti yangu,
nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
________
INJILI
Mt. 23: 27-32

Yesu alisema, Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi.

Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki, na kusema, K**a sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika kumwaga damu ya manabii. Hivyo mwajishuhudia wenyewe, ya kuwa ninyi ni wana wa wale waliowaua Manabii. Haha imalizeni kazi waliyoianza Baba zenu.
Neno la bwana.....sifa kwako eeh bwana

Address

Nandi Hills

Telephone

+254716792020

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Masomo ya Misa ya kila siku posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share