30/11/2025
Unajua Ngoma ya Harmonize na Darassa inaitwa MAZOEA, kuna Mtu anasema Harmonize alioshwa ama Darassa ๐
Buda, Harmonize Kwa Kolabo Huwa msafi already Hata Msanii akuje na Sabuni Msafi Huyo huwa Ashang'ara. Wacha Turudi Kwa Kolabo amezifanya.
Wimbo wa NAOGOPA Akiwa na Marioo, Tuseme ukweli Hapo Marioo verse Yake ilikuwa Avarage, Ila Harmonize alipoingia Na kutema Mistari na Kuvuja Emotions, Vocal Nzuri na Shairi La kuonyesha kuvunjwa Moyo Mashabiki walisifia Ufundi wake Haswa anapovunjwa Moyo, Harmonize alimfunika Marioo Blanketi mchana Kweupe!
Wimbo wa MAZOEA Akiwa na Darassa, Kwenye Verse ya Darassa, alirap hiyo haimaanishi Kuwa Alimfunika Harmoze, Harmonize alileta Hiyo hisia Kwa vocal na uandishi mzuri Pia, eti, "Nakunywa Pombe nilewe sababu NI Wewe silewi zinanipalia, oooh uuuh," Mashaiiri ya Harmonize Kwa nyimbo za Heartbreak Mbonaa mwamba Anajua Tu. Hapa Sisemi Nani alimzidi mwingine Ila Mimi niliupenda huo Wimbo Kwa sababu ya Hisia za Heartbreak ilivyoletwa na Harmonize.
Taja Nyimbo zingine za Kolabo ambazo Harmonize aliwaonyesha Wasanii wenzake Kivumbi.