14/09/2025
MREMBO YATIMA NA KIJANA TAJIRI❣️
SEHEMU YA 01
Asubuhi na mapema mimi na mdogo wangu Poppy tulikuwa tunapalangana jikoni kuandaa chakula kwa ajili ya wateja..
Tunamiliki kimgahawa kidogo tulichozungushia mabati mabovu hicho ndo kinatumatia kula na ada..
Wazazi weshafariki waliniacha nikiwa chuo mwaka wa kwanza na mdogo wangu poppy alikuwa ndo yuko form two..
Kwetu tumezaliwa wawili tu mimi Bella pamoja na poppy mdogo wangu..
Wazazi baada ya kufariki kitu pekee walichotuachia ni kijumba kidogo tulichokuwa tunaishi..
Hatukuwa na uwezo mkubwa kimaisha tulikuwa tunaishi kawaida na wazazi wetu walikuwa wafanya vibarua vya hapa na pale hivo ndo vilikuwa vinatulisha na kutusomesha..
Mimi na poppy tulishauriana kila likizo tuwe tunajishugulisha kuuza chakula ili tuweze kupata pesa ya ada..
Siku moja asubuhi wakati tunaendelea na shughuli zetu mgahawani hapo tulipata ugeni wa wateja wengi kidogo..
Walikuja vijana 12 ni mafundi ujenzi waliagiza chakula kisha wakatuambia Boss anakuja kulipa muda si mrefu❤️❤️..
Hatukuwa na kipingamizi maana sehemu walikokuwa wanajenga ni karibu na pale kazini kwetu..
Walikunywa chai hiyo asubuhi na mchana wakala cha mchana ilipofika jioni mimi na poppy tulikwenda kuchukua pesa..
Tulifika pale tukawakuta mafundi ndo wanabadili nguo kwa ajili ya kuondoka..
Walituambia Boss yuko njiani tumsubilie kidogo..tuliketi pale pembeni baada ya muda ikaja gari fulani hivi kali sana🤗🤗🤗...
Wale mafundi walisogea kumpokea aliyekuwemo kwenye gari alikuwa mkaka mdogo dogo tu umri k**a miaka 30 mpaka 33..
Waliongea naye pale akawagawia pesa baada ya hapo akasogea tulipo tukasalimiana baada ya hapo akatuuliza tunadai sh ngapi..
Nilimtajia kiasi cha pesa tunazodai akachomoa waleti akatoa pesa nyingi zaidi ya ile tunayoidai baada ya kuzihesabu zile pesa nilishangaa😳😳
Nilitoa tunayoidai ingine nikamrudishia...yule kaka aliniambia it's okay itawasaidia hiyo..
Mdogo wangu aliipokonya ile pesa akasema asante kaka...mimi niliichukua nikamrudishi